@HildaNewton21 Hawa watu Lissu akiwafia magereza, hawatakuwa na jeshi la kuzuia hasira za Watanzania, na hawataweza kutembea hadharani maisha yao yote . Acha waendelee kucheza na hatari.
MHE LISSU AFIKISHWA MAHAKAMANI LEO
Leo Asubuhi, Mheshimiwa Lissu amefikishwa Mahakamani kusomewa uamuzi mdogo kufuatia Maombi yake ya kuunganishwa kwenye kesi ya Said Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya wadhamini wa Chama na Katibu Mkuu.
Kuna mambo mawili hapa ya kukumbuka; Mosi, Maombi ya Mhe Lissu yalisikilizwa na Mwanga hivyo kisheria yeye alipaswa kutoa uamuzi wa Maombi hayo.
Pili, Ikumbukwe kwamba jalada la kesi ya Said Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya wadhamini na Katibu Mkuu, lilishaondoka mezani kwake, lipo kwa Jaji Ngunyale.
Sasa, Jaji Mwanga katika uamuzi wake amekataa Maombi ya Lissu kuunganishwa kwenye hiyo kesi.
Ufafanuzi zaidi utatolewa na Chama.
Wakili @ShundoGaston ,
Mkurungenzi wa sheria wa CHADEMA HQ.
@MsigwaPeter Ila tukiondoa mambo yote, kwa kuhamia kwako ccm ulitakiwa kupata nafasi kubwa ya kiuongozi serikalini aidha ukurugenzi wa idara, taasisi au halmashauri fulani, si hivi kubakia kuwa mwanaccm wa kawaida halafu watu wasio na uzoefu wavkiuongozi wanapewa nafasi. Mimi sifurahishwi.
Ongoza watu kama ambavyo ungependa mtoto wako aongozwe.
Ondoa kwanza mambo yote yanayotufanya tusahau ubinadamu wa watu — mifumo, vyeo vya kazi, taratibu za ofisini na makaratasi ya tathmini ya utendaji. Mambo hayo yana nafasi yake, lakini hayapaswi kuwa moyo wa uongozi.
Badala yake jiulize swali moja la msingi:
Kama huyu angekuwa mwanangu au binti yangu, ningependa kiongozi wake awe mtu wa aina gani?
Ningependa azungumze naye kwa heshima au kwa dharau?
Ningependa amuone kama namba kwenye orodha ya wafanyakazi, au kama mtu mwenye ndoto na uwezo?
Ningependa amuamini hata wakati bado anajifunza?
Ningependa amsaidie kukua au amkatishe tamaa?
Kiongozi mzuri huwa anasukuma watu wakue, lakini pia analinda utu wao.
Anawapa changamoto ili wafikie uwezo wao mkubwa zaidi.
Anawafundisha badala ya kuwavunja.
Anarekebisha makosa bila kudhalilisha.
Anawafanya wajione wana thamani, si kwa sababu ni wakamilifu, bali kwa sababu wanaweza kuwa bora zaidi.
Huo ndio uwe kichujio cha uongozi wako.
Huo ndio uwe kiwango chako cha maamuzi.
Sio kwa sababu uongozi unapaswa kuwa laini au dhaifu.
La hasha. Uongozi wa kweli unaweza kuwa na nidhamu, uwazi na viwango vya juu.
Lakini pamoja na hayo yote, lazima uwe wa kibinadamu.
Kwa sababu ukweli ni huu:
Watu wako sio “rasilimali” tu za kampuni.
Sio namba kwenye payroll.
Sio nafasi tu kwenye muundo wa shirika.
Kila mmoja wao ni dunia nzima ya mtu fulani.
Ni mtoto wa mtu.
Ni mzazi wa watoto fulani.
Ni mtu ambaye familia yake inamtegemea, watu wanamwamini, na maisha yao yanahusiana naye.
Ukikumbuka hilo, utaanza kuongoza tofauti.
Utasema maneno kwa makini zaidi.
Utajenga watu badala ya kuwavunja.
Utawasukuma kufikia ubora bila kupoteza utu wao.
Na mwisho wa siku, hutakuwa tu kiongozi anayefanikisha kazi.
Utakuwa kiongozi anayeheshimiwa.
Utakuwa kiongozi anayekumbukwa.
Na zaidi ya yote, utakuwa kiongozi mwenye heshima na utu
Kufunga kwa Muislam kunahusiana vipi na kula kwa mkristo?🤔
Kwa lugha nyepesi, kwa nini imani ya Muislam inilazimishe mimi kuishi kwa taratibu za Kiislam ingali ni Mkristo?🤔
Kwa nini kila mmoja asiishi imani yake bila kumlazimisha mwingine?🤔
Taarifa zinasema likizo za polisi wote zimesitishwa. Kuna ishara za jambo flani but still not clear what it is. Pia chanzo kinasema "Ikulu ni tafrani tupu". Asked which one, "kotekote" said the source: Tunguu, Chamwino na Dar.
#Jasusi yupo Tz virtually kwa ufuatiliaji zaidi 😊
Based on the final scores in Group C matches (Tanzania 1-1 Tunisia and Uganda 1-3 Nigeria), Tanzania finishes third in the group with 2 points, a goal difference of -1, and 3 goals scored.
Comparing to third-placed teams across all groups:
• Group A: Comoros (2 points, -2 GD, 0 goals scored)
• Group B: Angola (2 points, -1 GD, 2 goals scored)
• Group C: Tanzania (2 points, -1 GD, 3 goals scored)
• Group D: Benin (3 points, 0 GD, 1 goal scored)
• Group E: Sudan (3 points, -2 GD, 1 goal scored)
• Group F: Mozambique (3 points, 0 GD, 3 goals scored)
The four best third-placed teams qualify for the round of 16. Benin, Sudan, and Mozambique take three spots with 3 points each. Among the teams with 2 points, Tanzania ranks highest due to superior goals scored (3) compared to Angola (2) and Comoros (0).
Therefore, yes, Tanzania qualifies for the round of 16.
Source: @grok
"Mimi kama kaka, kama mshika dau wa sanaa ninawaombea radhi [wasanii] kwa niaba yao ili kiwanda kiendelee kusonga mbele." - Francis Ciza (Majizzo), Mmiliki wa E-FM Company Limited
Media za BONGO zimechagua kupost “Hali ilivyo Dar” na kuacha kabisa kupost “HALI ILIVYO MWANZA”—utafikiri mwanza ni nchi jirani.
NB: MAANDAMANO HAYA HAYANA KIKOMO. #D9
Nyerere angekuwepo angeumia san! Uhuru alioupigania na wazee wetu sio huu wa kuteka, kuua na kutesana.
Nyerere aliamini kwenye uhuru wa fikra na hakutaka kuwa na taifa la wajinga.
Viongozi ni wajinga ndo maana tuna kila kitu lakini ni maskini.
Nyerere angekuwepo angeandamana!!
@HildaNewton21 Schedule ya attempt nyingine hii.. Serikali ya Samia inaweza ikajikuta inaenda hivi na GenZ kwa miaka yote mitano, ratiba inaruhusu, wanavyotaka tunataka..👇👇👇
Hatuna bunduki wala silaha yoyote ila tuna bundle tu lakin tumefanikiwa kuifanya Serikali isimamishe shughuli zote nchi nzima.
Guys!.. guys! guys! sisi ni washindi maana maandamano ya kuiparalyze Serikali haram yamefanikiwa kwa asilimia 200 na tumewakosesha mapato.
Tumefanikiwa kuiweka Serikali haram yote kwenye panic mode ndo maana leo wanahaha kama kuku mwenye kiu ya maji
NB. Maandamano yetu hayana kikomo leo ilikuwa uzinduzi so kesho tutaendelea mpaka madai yetu yote ya msingi yafanyiwekazi.
#D9#SamiaMustGo
@Nnauye_Nape Sasa hii nchi itakuwaje, wameshindwa tarehe 9, watapanga tena tarehe 25xmas, tarehe 1 new year. Bila akili huko serikalini GenZ wataenda na hii serikali miaka yote mitano kwa mtiririko huu👇👇, Wajibisheni waliohusika iteni meza ya mazungumzo, wapeni watu katiba mpya.
@MpaleMpoki@Advocate_Jebra@MariaSTsehai Hii ni ngumu kukwepeka hata azungumze na mizimu ya Dar es salaam haimfutii kuwajibika ICC.. anajaribu kuziba jua kwa ungo.
Nimeangalia kamusi za kiswahili ili kuona maana na neno WAZEE !! Hii imekuja baada ya kuona BISIMBA na JENERALI ULIMWENGU hawajaalikwa. Nikatafuta atlasi ili kuona kama mipaka ya jiji imebadilishwa nikaona wanaishi Dar es salaam @Advocate_Jebra@MariaSTsehai
WAZEE NI WATU GANI
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima amesema anashangazwa kuona Mamlaka zinathamini vitu kuliko uhai wa Watu ambapo wametoa takwimu za vitu vilivyoharibiwa October 29,2025 lakini idadi ya waliouawa haijatajwa.
Akiongea leo December 01,2025, Padri Kitima amesema “Tanzania sasa hivi tunaongea tu, una taarifa za vitu vingi vilivyopotea, vilivyoharibika lakini uhai unazidiwa na vitu, uhai wa Binadamu hauna thamani kuliko vitu!, hata katika zile haki vitu vya umiliki vipo Ibara ya 20 na ngapi kwenda chini huko lakini haki ya uhai ni vitu namba moja vya mwanzo mwanzo kabisa haki za Binadamu zinavyoanza kwenye Ibara ya 12,13, 14 ya Katiba ya Tanzania”
“Unapoanza kuongelea vitu kuliko uhai wa Mtanzania, Tanzania hii Watu wanajali uhai kuliko kitu chochote, na tukumbuke haya yote tumejilea vibaya kutokana na yaliyofanywa ndani ya miaka miwili mitatu iliyopita juu ya kuteka na kupoteza Watu, Watu wanaongea wanalalamika hawasikilizwi”
“Watu wamepoteza Ndugu zao hawasikilizwi, uhai upo hatarini, yaliyotokea October 29 ni ishara Tanzania imefika wapi tusipokiri hatutosamehewa na anayesamehe hapa ni Watanzania, anayepaswa kuombwa msamaha ni Mtanzania huyo Mnyonge unayemuona hana maana usipomuomba msamaha itakugharimu tu maisha yote hata kama miaka 100 ijayo itakugharimu, ni kama Mungu usipomuomba msamaha ukimkosea utakaa motoni tu, Mwananchi usipomuomba msamaha hawezi kukusamehe”
“Na katika maongezi yetu na Serikali kama itatokea hayo ndio tutakayoongea itabaki hivyohivyo hatutoka nje ya tafakari iliyofanywa na Maaskofu na wameanza na kulaani mauaji, Watu kutekwa n.k “
#MillardAyoUPDATES
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hata kama atakuwa Waziri Mkuu kwa muda wa wiki moja atahakikisha anawasemea Watanzania wa hali ya chini na hatokubali taifa liwe na matabaka bali atahakikisha Watanzania wote wanakuwa sawa na kunakuwepo na usawa wa kisheria.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo hii leo novemba 26, 2025 wakati akizungumza katika Ufunguzi rasmi wa Wiki ya Usafiri endelevu Ardhini uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa JNICC jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa ataendelea kuwasemea watu wa hali ya chini kwani hata pale ambapo atakuwa hana cheo ataendelea kuwa nao.
“Nimemsikia Mwanaharakati mmoja huko ughaibuni anasema huyu ndio atakayekuwa Waziri Mkuu wa muda mfupi zaidi, sawa! Hata niwe Waziri Mkuu kwa wiki moja kwenye wiki hiyo sitaruhusu Watanzania waishi, iwe nchi ya mabwana na Watwana, katika muda huo huo sitaruhusu Watanzania wawe na madaraja. Kwamba kuna sheria imetungwa ya kuwalinda wa daraja la juu na kuwatweza wa daraja la chini. Kwamba akikosea wa daraja la chini anaadhibiwa palepale na wa daraja la juu anapita, analindwa”____Amesema Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba
#MillardAyoUPDATES
@Chahali@mwigulunchemba1 Siasa zake za kizamani sana huyu mtu haram.. Jasusi mimi napenda sana kusoma na kusikiliza watu wenye akili kubwa, alipotoweka polepole niliumia sana, lakini sasa kaibuka HABIL.. Huyu anatoa mpaka details za ushahidi.. ninaburudika sana na huduma zake.
.@mwigulunchemba1 anukuu ubashiri wa kiintelijensia wa #Jasusi uliotanabaisha kuwa yeye Mwigulu atakuwa PM wa muda mfupi kuliko wote. Ubashiri ni huu hapa "INTELLIGENCE FORECAST: Tanzania Prime Minister Mwigulu Nchemba - Political Longevity Assessment" ujasusi.com/p/intelligence…
VIDEO:
Akizungumza katika Mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, leo Novemba 25, 2025, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema baada ya uchaguzi kulitokea msukosuko uliohusisha kupoteza maisha ya Watanzania hata ambao hawakushiriki
Dkt. Mwigulu ametoa pole kwa familia zote zilikumbwa na madhila hayo akisema kwenye imani yake “kumwaga damu ya mtu mmoja asiye na hatia siyo baraka katika ardhi husika”
Aidha, Dkt. Mwigulu ametoa wito kwa kila Mwananchi kwenye dhamira yake kunuia jambo la aina hiyo lisitokee tena Nchini, kwani si baraka na linatengeneza makovu yasiyopona na linatupa gharama
VIDEO:
Shura ya Maimamu na Viongozi wa taasisi za Kiislamu Mkoani Arusha imetoa tamko la kulaani machafuko ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, na kutaka hatua madhubuti zichukuliwe ili kurejesha na kulinda amani ya nchi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Arusha, mlezi wa Shura hiyo, Sheikh Juma Ikusi, amesema machafuko yaliyotokea yameacha majereha na kuchafua taswira ya taifa lililojengwa kwa misingi ya umoja na mshikamano tangu enzi za waasisi wa taifa.
Katika tamko hilo, Sheikh Ikusi pia alionyesha kukerwa na baadhi ya matamko kutoka kwa viongozi wa dini ya Kikristo kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), akidai kuwa baadhi ya kauli zao zilichochea Mazingira ya vurugu wakati wa uchaguzi.
“Maaskofu wa TEC sasa wameingia katika mrengo wa kisiasa nchini? Inasikitisha sana pale ambapo maaskofu wanaomba watu kutoka nje ya nchi, ambao waliwahi kututawala na kutunyonya, waje kufanya uchunguzi,’” Sheikh Ikusi alisema
Aidha, Sheikh Ikusi amesema kuwa katika dini ya Kiislamu, amani ndiyo msingi mkuu unaopewa kipaumbele zaidi kuliko haki, na hivyo amewasisitiza Watanzania kuendelea kudumisha amani ya nchi.
Nilitamani kuishi nikiona ‘Mapacha wa Kariakoo’ siyo agenda mbele ya agenda zinazohusu maslahi ya umma. Nimeishi nyakati hizo mara ya kwanza. Tuendelee kujishikilia. Mali za mbogamboga zisizoweza kutoa pole kwa mashabiki wao waliouwawa kikatili haziwezi kuwa timu zetu. Tuzikatae.