

#ChangeTanzania
106.9K posts

@ChangeTanzania
This is #ChangeTanzania movement of citizens exercising their right to #FreedomOfExpression | for activism contact via WhatssApp & Telegram +1 (862) 438-3337






Mapendekezo ya 12 Tume ya Uchunguzi kwa Serikali ya JMT 1. Majeruhi wapatiwe matibabu na vifaa saidizi bure. 2. Itengwe siku ya maombolezo ya kitaifa ya kuwakumbuka waliofariki. 3. Kutolewe msaada wa kisaikolojia na kijamii kwa waathirika. 4. Katiba Mpya ipatikane ifikapo 2028 ili itumike katika Uchaguzi wa S/Mitaa 2029 na Uchaguzi Mkuu 2030 5. Serikali iunde Tume ya Maridhiano. 6. Liundwe Baraza la Wazee kuisaidia Tume ya Maridhiano. 7. Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi itekelezwe kikamilifu. 8. Iundwe tume ya uchunguzi ya kijinai ili kushughulikia tuhuma zilizopo. 9. Polisi waimarishe uhusiano wao na jamii. 10. Serikali na vyombo vya dola vitekeleze majukumu kwa kuzingatia misingi ya demokrasia. 11. Maadili na miiko ya viongozi na watumishi wa umma visimamiwe kwa karibu. 12. Baraza la Taifa la Vijana liundwe na litumike pia kama jukwaa la maridhiano.









