Eazy E
2.3K posts

Eazy E
@ImmvReal22
Survived too many storms to be bothered by raindrops 🌧️







#HABARI Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam linachunguza kifo cha James Temba mkazi wa Tabata Chang’ombe Wilaya ya Ilala. Taarifa Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Jumanne Muliro aliyoitoa leo Jumapili, Mei 3, 2026 imesema linachunguza kifo cha mtu huyo ambaye Aprili 30, 2026 saa 09 :00 Alasiri mwili wake ulikutwa unaelea kwenye maji yaliyokuwa yanatiririka katika Mto Msimbazi eneo la Kipawa Wilaya ya Ilala. Kamanda Muliro amesema mwili huo ambao haukuonekana kuwa na kichwa baadaye uchunguzi wa awali umeonesha unaweza kuwa wa mtu aitwaye James Temba. Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo cha kifo hicho na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuhusika. #HABARI #EastAfricaTV























