Antidote

29.8K posts

Antidote banner
Antidote

Antidote

@Mentidote

Brown skin girl who loves beauty and lives with confidence. 🤎

Dar es salaam Katılım Mart 2020
358 Takip Edilen13.7K Takipçiler
Antidote
Antidote@Mentidote·
Serikali inaendelea kuonyesha dhamira ya dhati katika kulinda urithi wa taifa. Kupitia uongozi wa Samia Suluhu Hassan, mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti ya uchunguzi wa Ngorongoro Conservation Area yatafanyiwa kazi kwa kina ili kuhakikisha Tanzania inalinda mazingira yake
Indonesia
0
4
6
89
Antidote retweetledi
Mabrouk Mabrouk
Mabrouk Mabrouk@mabrouk0161·
Tanzania inaendelea kusimamia kwa umakini rasilimali zake za kipekee. Rais Samia Suluhu amesisitiza kuwa mapendekezo yote yaliyotolewa kwenye ripoti ya uchunguzi wa Ngorongoro Conservation Area yatafanyiwa kazi ili kupata suluhisho lenye haki,uwiano na manufaa kwa wananchi
Indonesia
0
3
4
49
Antidote retweetledi
Belinda Mutashobya
Belinda Mutashobya@BMutashoby6080·
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea na kupokea maelezo ya kina ya Taarifa za Tume za Rais kuhusu tathmini ya mgogoro wa ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na zoezi la uhamaji wa hiari wa wakazi wa eneo hilo, Ikulu ya Chamwino, Dodoma, tarehe 12 Machi 2026
Belinda Mutashobya tweet mediaBelinda Mutashobya tweet media
Indonesia
0
4
4
40
Antidote retweetledi
George mtei
George mtei@Georgemtei78977·
Kupitia mradi wa Bwawa la Kidunda, juhudi za kuboresha huduma ya maji nchini zinaendelea kuonekana. Uwezo wa kuzalisha lita bilioni 20 za maji kwa siku utasaidia kupunguza uhaba wa maji na kuboresha maisha ya wananchi pamoja na kusaidia shughuli za kiuchumi.
George mtei tweet media
Indonesia
0
3
3
34
Antidote retweetledi
Purity Magesa
Purity Magesa@purity1978·
Kulinda rasilimali za taifa ni jukumu la kila MtanzaniaKupokea ripoti ya uchunguzi wa masuala ya Ngorongoro Conservation Area,Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito wa ushirikiano kutoka kwa wananchi wote ili kuhakikisha urithi huu wa kipekee unaendelea kuhifadhiwa kwa manufaa yetu
Indonesia
0
4
5
21
Antidote retweetledi
Osward Mussa
Osward Mussa@OswardMussa·
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye hafla ya kupokea Taarifa za Tume ya Rais ya Kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi
Osward Mussa tweet mediaOsward Mussa tweet mediaOsward Mussa tweet media
Indonesia
1
4
4
30
Antidote retweetledi
Dira Ya Samia
Dira Ya Samia@DiraYaSamia·
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia akizungumza kwenye hafla ya kupokea Taarifa za Tume ya Rais ya Kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Ameeleza kuwa Ngorongoro ni urithi wa dunia, si wa Tanzania pekee, na umetambuliwa kimataifa chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Kutokana na hadhi hiyo, Watanzania wana wajibu mkubwa wa kulinda na kuhifadhi urithi huo muhimu ambao tumejaariwa na Mwenyezi Mungu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo. Rais amefafanua kuwa Ngorongoro ni eneo la kipekee duniani lenye kreta kubwa iliyotokana na miujiza ya kiasili ya kijiolojia, yenye kina cha takribani mita 600 kutoka juu kwenda chini, jambo linalolifanya kuwa kivutio cha kipekee duniani. Rais Samia ameongeza kuwa eneo hilo lina utajiri mkubwa wa banuai, likiwa na wanyama wa aina mbalimbali wanaokula majani pamoja na wanaokula wenzao, wakiwemo wanyama wakali. Aidha, ameelezea uwepo wa ndege wa aina nyingi wakiwemo flamingo pamoja na vivutio vingi vya asili ambavyo ni nadra kupatikana sehemu nyingine duniani ndani ya eneo moja. Pia amesisitiza kuwa eneo la Olduvai lililopo ndani ya ukanda huo lina umuhimu mkubwa wa kihistoria, kwani lina ushahidi wa uwepo wa mwanadamu wa kale uliokadiriwa kuwepo takribani miaka milioni tatu iliyopita. Kutokana na umuhimu huo wa kiikolojia na kihistoria, Rais Samia amesisitiza kuwa Ngorongoro ni rasilimali muhimu inayopaswa kulindwa na kuhifadhiwa kwa manufaa ya taifa na dunia kwa ujumla. @ikulumawasliano #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Indonesia
11
24
26
1.1K
Antidote retweetledi
Dira Ya Samia
Dira Ya Samia@DiraYaSamia·
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia akizungumza kwenye hafla ya kupokea Taarifa za Tume ya Rais ya Kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Ameeleza kuwa kutokana na umuhimu mkubwa wa eneo la Ngorongoro, kuna mchanganyiko wa masuala mbalimbali yanayohitaji kuzingatiwa, ikiwemo uwepo wa wananchi na mifugo yao pamoja na wajibu wa kulinda urithi wa dunia uliopo katika eneo hilo. Ameeleza kuwa hali hiyo imekuwa ikiibua swali muhimu la namna bora ya kukabiliana na mahitaji hayo yote; kwa upande mmoja watu na mifugo yao ni sehemu ya jamii ya nchi, na kwa upande mwingine Ngorongoro ni rasilimali muhimu inayopaswa kulindwa kwa manufaa ya taifa na dunia kwa ujumla. Rais Samia amesema tume imefanya kazi kubwa na kutoa mapendekezo muhimu ambayo Serikali itayafanyia kazi kwa umakini ili kupata suluhisho endelevu kwa masuala ya eneo hilo. Aidha, ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wenyeviti pamoja na wajumbe wa tume hizo kwa kukubali kubeba jukumu hilo kubwa na nyeti kwa maslahi ya taifa. Ameeleza kuwa kazi waliyopewa haikuwa rahisi kutokana na wingi wa masuala yaliyohitaji kujadiliwa, mikutano mingi waliyofanya pamoja na maoni tofauti kutoka kwa wadau mbalimbali waliokutana nao. Rais Samia amewapongeza kwa kazi yao kubwa ya kizalendo waliyoifanya kwa bidii, uadilifu na weledi mkubwa ili kutimiza kwa mafanikio jukumu walilokabidhiwa kwa manufaa ya nchi. @ikulumawasliano #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Indonesia
14
21
22
918
Antidote retweetledi
Dira Ya Samia
Dira Ya Samia@DiraYaSamia·
SERIKALI YATOA RUZUKU YA SHILINGI BILIONI 1.63 KUTEKELEZA MRADI WA UMEME WA MAJI IJANGALA NJOMBE Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 1.63 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Maji wa Ijangala uliopo wilayani Makete, mkoani Njombe. Mradi huo wa Ijangala Mini Hydropower Plant wenye uwezo wa kuzalisha kilowati 360 tayari umeunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji na uimara wa nishati ya umeme hususan katika maeneo ya vijijini. Kupitia ruzuku hiyo, miundombinu muhimu ya mradi imejengwa ikiwemo transfoma chochezi yenye uwezo wa KVA 500 pamoja na njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolt 33 yenye urefu wa kilomita 0.6 inayounganisha mradi huo na Gridi ya Taifa. Aidha, mradi huo ulipata mkopo nafuu wa shilingi milioni 922 kupitia programu ya Tanzania Rural Electrification Expansion Program (TREEP) inayosimamiwa na REA, uliosaidia kugharamia baadhi ya shughuli za utekelezaji wa mradi. Mradi huu unatekelezwa na Dayosisi ya Kusini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kupitia Kituo cha Udiakonia cha Tandala, kwa kushirikiana na Serikali katika kukuza uwekezaji kwenye nishati jadidifu na kuimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo ya vijijini. @ikulumawasliano #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Dira Ya Samia tweet mediaDira Ya Samia tweet media
Indonesia
7
25
29
1.3K
Antidote retweetledi
Dira Ya Samia
Dira Ya Samia@DiraYaSamia·
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia akizungumza kwenye hafla ya kupokea Taarifa za Tume ya Rais ya Kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma Ameeleza kuwa katika miaka ya nyuma kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu suala la Ngorongoro, ukiambatana na taarifa mbalimbali katika mitandao ya kijamii, malalamiko ya wakazi wa eneo hilo, pamoja na mashtaka yaliyowasilishwa katika taasisi tofauti za kimataifa. Rais Samia amesema hali hiyo ilimfanya mwezi Desemba mwaka 2024 kutafuta nafasi ya kukutana na viongozi wa kimila wa kabila la Wamasai pamoja na wazee wa jamii ya Ngorongoro ili kuzungumza nao moja kwa moja na kusikiliza kwa kina changamoto zinazowakabili. Amesema katika mazungumzo hayo, viongozi hao walieleza changamoto zao hususan zinazohusiana na matumizi ya ardhi, uhifadhi wa mazingira pamoja na utekelezaji wa zoezi la uhamaji wa hiari kutoka ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda maeneo yaliyotengwa na Serikali. Rais Samia amefafanua kuwa zoezi la uhamaji wa hiari lilianzishwa na Serikali kwa lengo la kutoa fursa kwa wakazi wa eneo la hifadhi waliokuwa tayari kuhama, kwa kuwapatia maeneo mbadala ya makazi pamoja na mazingira bora ya kuendeleza shughuli zao za kijamii na kiuchumi. @ikulumawasliano #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Indonesia
10
23
27
1.3K
Antidote
Antidote@Mentidote·
Uamuzi makini hutokana na ukweli na utafiti. Rais Samia Suluhu Hassan ameipokea ripoti ya uchunguzi kuhusu changamoto na mustakabali wa Ngorongoro Conservation Area, akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kutafuta suluhisho lenye kulinda rasilimali za asili huku ikizingatia haki
Indonesia
0
1
1
43
Antidote retweetledi
Dira Ya Samia
Dira Ya Samia@DiraYaSamia·
SERIKALI YATEKELEZA UJENZI WA KM 206.33 ZA BARABARA ZA LAMI NA MIRADI 76 YA MADARAJA Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia kupitia Wizara ya Ujenzi inaendelea kuimarisha miundombinu ya barabara na madaraja nchini kwa lengo la kurahisisha usafiri, kukuza biashara na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi. Hadi kufikia Februari 2026, Wizara ya Ujenzi imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa kilomita 206.33 za barabara kwa kiwango cha lami, hatua inayochangia kuimarisha mtandao wa barabara na kuboresha mawasiliano kati ya maeneo mbalimbali ya nchi. Aidha, wizara imekamilisha miradi 76 kati ya 81 ya dharura ya ujenzi wa madaraja yaliyoharibiwa na mvua kubwa za El-Niño pamoja na Kimbunga Hidaya katika mikoa 22 nchini, huku miradi mitano (5) iliyobaki ikiwa katika hatua za mwisho za kukamilishwa. Kwa upande wa maendeleo ya ujenzi wa madaraja makubwa yanayoendelea kujengwa nchini, utekelezaji wa miradi hiyo umefikia hatua mbalimbali ambapo Daraja la Pangani limefikia asilimia 70, Jangwani asilimia 26, Mbambe asilimia 44, Sukuma asilimia 76, Simiyu asilimia 73, Mirumba asilimia 50, na Mitomoni asilimia 85 ya utekelezaji. Hatua hizi zinaendelea kuonyesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuimarisha miundombinu ya usafiri nchini, kurahisisha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo ya wananchi. @ikulumawasliano #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Dira Ya Samia tweet mediaDira Ya Samia tweet media
Indonesia
9
25
31
1.2K
Antidote
Antidote@Mentidote·
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akipokea Taarifa za Tume za Rais zilizoundwa kutathmini mgogoro wa ardhi na zoezi la uhamaji wa hiari wa wakazi wa Hifadhi ya Ngorongoro, Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma, tarehe 12 Machi 2026.
Antidote tweet mediaAntidote tweet media
Indonesia
0
6
7
56
Antidote
Antidote@Mentidote·
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akipokea rasmi Taarifa za Tume ya Rais zilizoundwa kutathmini mgogoro wa ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na zoezi la uhamaji wa hiari wa wakazi wa eneo hilo, Ikulu ya Chamwino, Dodoma, tarehe 12
Antidote tweet mediaAntidote tweet media
Indonesia
1
4
5
61
Antidote retweetledi
Zuhura Abdallah
Zuhura Abdallah@zuhura73·
Ujenzi wa Bwawa la Kidunda ni hatua kubwa ya maendeleo inayolenga kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa uhakika. Mradi huu wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 335 utakuwa suluhisho la muda mrefu kwa changamoto ya maji katika ukanda wa pwani na maeneo ya jirani
Zuhura Abdallah tweet media
Indonesia
0
2
2
20
Antidote retweetledi
Belinda Mutashobya
Belinda Mutashobya@BMutashoby6080·
Kupitia ujenzi wa Bwawa la Kidunda, Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa mamilioni ya wananchi. Mradi huu mkubwa unaotarajiwa kuzalisha lita bilioni 20 za maji kwa siku utakuwa suluhisho la kudumu kwa changamoto ya maji
Belinda Mutashobya tweet media
Indonesia
0
1
1
17
Antidote retweetledi
PT
PT@PaschalTemu·
Utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) umefikia asilimia 81 huku ujenzi wake ukitarajiwa kukamilika Julai 2026,
PT tweet media
Indonesia
0
5
5
31
Antidote retweetledi
Osward Mussa
Osward Mussa@OswardMussa·
Gharama za kupika chakula katika shule 13 za msingi Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam zinatarajiwa kupungua baada ya shule hizo kuanza kutumia majiko ya umeme badala ya kuni. Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Nishati, Idara ya Elimu ya Awali na Msingi Temeke
Osward Mussa tweet media
Indonesia
1
3
4
47
Antidote retweetledi
Belinda Mutashobya
Belinda Mutashobya@BMutashoby6080·
Utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) umefikia asilimia 81 ya ujenzi wake, hatua inayoonesha kasi ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati, huku matarajio yakiwa ni kuukamilisha ifikapo Julai 2026 na kuanza kutoa manufaa makubwa kiuchumi
Belinda Mutashobya tweet media
Indonesia
0
2
2
19