Martin Maranja Masese@IAMartin_
Kulinganisha bei ya bidhaa kama mafuta (petroli/dizeli/mafuta ya taa) kati ya nchi iliyoendelea na nchi inayokua bila kuangalia uwezo wa kununua (Purchasing Power) ni kujaribu kupotosha ukweli halisi wa hali ya maisha.
Tofauti ya Kipato cha Wastani (GDP per Capita) ndiyo kigezo kikubwa zaidi kinatumika hapa. Hata kama lita ya mafuta Norway ni ghali mara mbili ya Tanzania, kipato cha raia wa Norway ni kikubwa mara hamsini zaidi.
Uwezo wa Kununua Mafuta (Fuel Affordability); hapa utapaswa kuangalia asilimia ya kipato cha kila siku kinachohitajika kununua lita moja ya mafuta kwa nchi hizo ulizotaja (Mfano Netherlands) na Tanzania.
Mtu wa kawaida Norway au Netherlands ana mapato mara 50 au 70 zaidi ya mtu wa Tanzania. Hii inamaanisha kuwa gharama yoyote (hata ndogo) inachukua sehemu kubwa zaidi ya bajeti ya familia ya Kitanzania.
Tanzania (data 2018–2022, bado inatumika kama kiashiria) na inaonyesha 51.3% ya watu wanaishi chini ya $2.15 kwa siku (umaskini mkali wa kimataifa). Karibu 70% wanaishi kwa kipato cha chini ya $3.65 kwa siku.
Katika nchi za Norway, Sweden au Netherlands raia wa kawaida katika nchi hizo anatumia chini ya 1% ya kipato chake cha siku kununua lita moja ya mafuta. Kwao, mafuta ni gharama ndogo sana (pocket change).
Mtanzania wa kawaida anayepata kipato cha wastani wa Tsh 15,000 kwa siku, akitakiwa kununua lita moja ya mafuta kwa Tsh 3,800, anatumia zaidi ya 20% ya kipato chake cha siku kwa ajili ya kununua lita moja tu.
Kwa akili ya kawaida tu, maumivu anayoyasikia Mtanzania wa kawaida kwa kununua lita moja ya mafuta ya petrolo na dizeli ni makubwa mara 20 zaidi ya anayoyasikia raia wa Netherlands au Norway.
Katika nchi kama Sweden, Norway na Netherlands, mfumo wa kodi unarudisha huduma bora za kijamii (shule bure, bima ya afya ya uhakika, usafiri wa umma wa kisasa). Hii kitaalam inaitwa ‘disposable income’
Tanzania, raia wa kawaida anapaswa kutoa fedha mfukoni kwa ajili ya kugharamia ada ya shule, matibabu (ambayo ni gharama kubwa), na usafiri binafsi kwa sababu usafiri wa umma haujitoshelezi.
Wakati raia wa Norway akimaliza kununua mafuta, anabakiwa na pesa nyingi ya ziada (disposable income). Mtanzania wa kawaida akimaliza kununua mafuta na chakula, mara nyingi anabaki na deni au sifuri
Ulaya, mifumo ya hifadhi ya jamii inawalinda masikini. Tanzania, mfumuko wa bei wa bidhaa za chakula una athari ya moja kwa moja, zaidi ya 50% ya kipato cha kaya Tanzania huishia kwenye chakula pekee.
Kujaribu kulinganisha bei ya bidhaa za mafuta ya Tanzania (Tsh 3,900) na ya Netherlands (Tsh 6,000) bila kuhusisha GDP per Capita ni sawa na kulinganisha uzito wa chungwa na uzito wa basi la abiria.
Pamoja na kwamba mnafanya kazi ya kuitetea Serikali katili ya mbogamboga, jitahidini kuwaonea watanzania huruma. Mafuta yakipanda bei katika pampu, athari za kiuchumi katika maisha ya kawaida ni kubwa.