Sabitlenmiş Tweet

🧵 UZI: Kwa Kijana Unayepambana na "Stress" za Maisha, Lakini Hukati Tamaa. Soma Huu Mstari kwa Mstari. 👇
1. Maisha ya utafutaji siyo lelemama. Kuna siku utaamka na buku mbili tu mfukoni, huku una mipango ya milioni kumi kichwani. Unajiona kama unachelewa, lakini ukweli ni kwamba unapita kwenye "process" ambayo wengi hawawezi kuimudu. #Utafutaji #Hustle
2. Kuna Hatua Tatu za Utafutaji:
Kupuuzwa: Utaonekana chizi, huna mbele wala nyuma.
Kusemwa: Wataanza kusema unapoteza muda, bora utafute kazi ya kuajiriwa.
Kuombwa msaada: Hii ndiyo hatua ya mwisho baada ya kutoboa. Usikate tamaa ukiwa hatua ya kwanza. 🧗♂️
3. Kumbuka: Siyo kila "Connection" inatoka kwa mtu unayemfahamu. Wakati mwingine, connection yako ipo kwenye nidhamu yako, jinsi unavyoongea na watu, na jinsi unavyofanya kazi yako hata kama huna msimamizi. Nidhamu ni Mtaji.
4. Usilinganishe saa yako na ya mtu mwingine. Kuna aliyetoboa akiwa na miaka 21, na kuna aliyetoboa akiwa na miaka 35. Wote walifika. Muhimu ni kwamba, kobe na sungura wote waliingia kwenye Safina ya Nuhu. Usiache kutembea. 🐢🏃♂️
5. Ushauri wa bure:
Punguza marafiki wa "starehe" wakati bado hujatulia.
Jifunze ujuzi mpya kila mwezi (Hata kama ni kupitia YouTube).
Usione aibu kufanya kazi yoyote halali; aibu haijengi nyumba wala hainunui mkate.
6. Mafanikio hayaji kwa miujiza, yanakuja kwa mfululizo wa maamuzi madogo madogo sahihi. Kila mara unapochagua kuweka akiba badala ya kutumia hovyo, unajisogeza karibu na uhuru wa kifedha. 💰
7. Leo inaweza kuwa ngumu, kesho ikawa ngumu zaidi. Lakini keshokutwa, jua litalazimika kuchomoza. Endelea kupambana, endelea kuomba, na weka juhudi. Mungu hamtupi mja wake anayewajibika. 🙏
8. Tag hapa chini mtafutaji mmoja unayemkubali sana na umwambie:
"Keep Pushing, Mwaka Huu Ni Wetu!" 🚀🔥

Indonesia















