NON EMPLOYED TEACHERS ORG
46 posts

NON EMPLOYED TEACHERS ORG
@NETO_TANZANIA
Akaunti rasmi ya umoja wa walimu wasio na ajira Tanzania

VIDEO: Serikali imetangaza jumla ya nafasi 41,500 za ajira katika kada mbalimbali zikiwemo elimu, afya, ulinzi, kilimo, mifugo na uvuvi, huku ikiagiza Sekretarieti ya Ajira kukamilisha mchakato wa kuzijaza zote ifikapo Novemba mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi, Oktoba 11, 2025, katika Ofisi za Utumishi zilizopo Mtumba jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Mkomi, amesema ajira hizo zimetengwa mahsusi kwa ajili ya kujaza upungufu mkubwa wa watumishi wa umma nchini. Kwa mujibu wa Mkomi, kada zitakazonufaika ni pamoja na: Elimu: nafasi 12,176 Afya (Serikali za Mitaa): nafasi 10,280 Kilimo: nafasi 470 Mifugo: nafasi 312 Uvuvi: nafasi 47 Vyombo vya Ulinzi (Polisi, Magereza, Zimamoto na Uhamiaji): nafasi 7,000 Aidha, kada nyingine mbalimbali nazo zitapewa kipaumbele. Mkomi ameielekeza Sekretarieti ya Ajira kukamilisha pia mchakato wa ajira 45,000 ambazo hazikujazwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025, sambamba na ajira mpya za mwaka 2025/2026, kabla ya kufika Novemba mwaka huu. Ameongeza kuwa kwa sasa Serikali inakabiliwa na upungufu wa watumishi takribani 280,000, na kwamba juhudi zinaendelea kufanyika kwa kutoa vibali vipya vya ajira ili kupunguza pengo hilo.























