#NIPENI_MAUA_YANGU💐@Roma_Mkatoliki
Nionavyo mimi!!
Tunao Rappers/Mc’z
and HipHop heads wazuri wengi tu!
Lakini ni wazuri tu kwenye ufundi wa kucheza na maneno tu, kupanga vina na flow tamu!!
Lakini hupati exactly maana ya anacho-rap!!
Ni kama anacho rap hakina maana au you can’t relate na maisha ya msikilizaji!!
Unakuta mtu anarap
Mfano…anaweza akasema
🗣️ Midondoko,Mikong’oto,Misokoto
yetu kanga moko/
Dry peku kama mpoto, masai yechu
hii namba nyoko/
Ukimsikiliza na alivyonata na mdundo utapenda, BUT YOU CANT RELATE!!
Ni kundi dogo sana linaweza relate na ulichosema
(Wasanii wenzako na wenye ndoto za kuwa wasanii)
Ni lines zinaweza kuwa tamu lakini hata yeye ukimbana kwa interview afafanue alimaanisha nini…..
HE CANT!
Ataishia tu kusema….
Si umeona hiyo Dry Peku, halafu kule mwanzo nilisema misokoto!
Kwahiyo misokoto 🚬 yani dry….yani peku😁….halafu Mpoto si ndo’ anatembeaga peku na rasta zake kama misokoto😁 YANI HIZO NDO’ METAPHOR’s kaka!!
Skillz za rap hizo!!
Ndio kashafafanua hapo kamaliza!!
Haya we umemuelewa!??🤔🤷🏿
Wito wangu, tengeneza maudhui (Content) ya nyimbo ambayo audience can relate with!!
Hasa na maisha yao ya kila siku, iwe mapenzi,bata,siasa,inspiration.
Na uiandike katika namna msikilizaji anaweza kuvaa uhusika!!
Utapata fans wengi, utasikilizwa na watu wengi na fanbase yako itakuwa!!
Ukiendelea na hizi za
michomoko, miporomoko/
Tamathali za semi, na stanza sijui za banza kama stone na jiwe ndo magu chato/ na iwe manjagu couple!!
Hizi watasikiliza tu kundi chache la wanaopenda Rap au wenye ndoto za kuwa Rappers!!
Ndio maana Rappers wa dizain hii wengi wana struggle kupata fanbase kubwa, coz wanawaimbia wasanii wenzao na sio mashabiki!!
Hakikisha Rap yako
anaweza aka relate Mtoto/
Mama mtu mzima/Muhuni/Sista du/Padre/Ustaadh/Kiongozi/Babu/Bibi
Hadi shabiki ambaye hafatilii muziki, Kama Padre anaweza sikia line moja na aka relate na maisha yake!!
NA HIYO NDIYO HIP HOP!!
Tusiwajaze sana vichwa hawa na kuwaambia wao ni wakali sana, kwa sababu tu wanaweza kucheza na maneno wakatengeneza vina!!
HipHop/Rap Hakikisha inaleta maana!!
GUSA MAISHA YA WATU!