Abdulmajid Nsekela

482 posts

Abdulmajid Nsekela banner
Abdulmajid Nsekela

Abdulmajid Nsekela

@amnsekela

Group CEO @CRDBBankPlc | Chairman of @ushirika_tcdc | Former Chairman of @tba_forbankers

Dar es Salaam, Tanzania Katılım Aralık 2019
55 Takip Edilen14.3K Takipçiler
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Leo nimeshiriki katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Bagamoyo Diaconic Lutheran Centre kinachojengwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Katika harambee hiyo iliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Benki ya CRDB na kampuni zake tanzu pamoja na mimi na familia yangu tumetoa ahadi ya jumla ya Shilingi Milioni 220 kusaidia ujenzi wa kituo hiko. Kipekee sana nimshukuru Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa kwa kutupa heshima ya kushiriki baraka hii kwa watoto hawa ambao wanahitaji kutazamwa kwa jicho la kipekee.
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
Indonesia
10
13
72
4.4K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Alhamdulillah siku ya jana tulikamilisha kwa mafanikio makubwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 30 wa Benki ya CRDB ikiwa ni tukio la kujivunia tunaposherehekea “Miaka 30 ya Kukua Pamoja na Wanahisa Wetu.” Miongoni mwa mambo muhimu yaliyoidhinishwa katika mkutano mkuu ni gawio la Shilingi 65 kwa kila hisa, ishara ya mafanikio yetu thabiti kwa mwaka wa fedha 2024 na dhamira ya kutoa thamani endelevu kwa wanahisa wetu. Tulipata pia fursa ya kuchagua wajumbe wapya wa Bodi, ambao watatoa mchango wao katika kuongoza benki kuelekea hatua inayofuata ya maendeleo. Kipekee sana natoa shukrani za dhati kwa wajumbe wa Bodi wanaomaliza muda wao kwa mchango wao mkubwa na uongozi madhubuti kwa miaka yote. Mmeacha alama isiyofutika katika historia ya mafanikio yetu. Kwa wajumbe wapya wa Bodi, hongereni sana na karibuni! Naahidi ushirikiano wangu wa dhati tunapoendelea kuimarisha nafasi ya Benki ya CRDB kama kinara wa sekta ya fedha na kuchochea ukuaji shirikishi na endelevu. Asanteni wanahisa, wateja, na wadau wote kwa kuwa sehemu ya safari yetu ya miaka 30. Tunaamini kuna mambo makubwa zaidi huko mbeleni tukikua pamoja nanyi. #CRDBAGM2025 #Miaka30YaUkuajiwaPamoja
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
Indonesia
11
19
128
5.8K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Leo tumekua na semina nzuri ya wanahisa wetu kuelekea katika Mkutano Mkuu wa 30 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB. Kipekee sana nimshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. @dr_mpango kwa kukubali mwaliko wetu na kutufungulia semina yetu. Vilevile niwashukuru viongozi mbalimbali wa Serikali na taasisi zake aliombatana nao wakiwemo Naibu Spika, Mhe. @zungumussa , Waziri wa Elimu @professoradolfmkenda , Naibu Gavana wa Benki Kuu, Bi. Sauda Msemo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere na viongozi wa Mkoa wa Arusha. Kuelekea katika mkutano wetu siku ya kesho niendelee kuwakaribisha wanahisa wetu kuhudhuria kwa wingi katika mkutano wetu wa kihistoria tunaposheherekea miaka 30 ya uwepo wa Benki ya CRDB kwani ushiriki wao una mchango mkubwa katika maendeleo ya Benki yetu.
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
Indonesia
6
12
68
5.6K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Nikiwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bara @ushirika_tcdc , jana nilipata heshima ya kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya makabidhiano rasmi kutoka Bodi ya Mpito kwenda kwa Bodi Mpya ya Benki ya Ushirika Tanzania @coopbanktanzania. Nimeipongeza sana Bodi ya Mpito ya Benki ya Ushirika chini ya uongozi wa Prof. Gervas Machimu kwa kazi kubwa ya kuweka misingi imara ya uongozi na usimamizi bora wakati wa mchakato wa mageuzi ya Benki za KCBL na TCBL zilizoungana na kuunda Benki ya Ushirika Tanzania. Vile vile nimeipongeza Bodi Mpya chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Joseph Witts kwa imani kubwa iliyowekwa juu yao katika kuongoza Bodi ya Benki hii mpya nchini. Nimewaahidi ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha tunasimamia vyema dhamira njema ya Serikali katika kuanzisha Benki ya Ushirika nchini.
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
Filipino
5
2
25
1.3K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Ni heshima kubwa kwangu kutajwa katika orodha ya viongozi 25 bora wa Afrika katika sekta ya fedha na jarida la "African Leadership Magazine". Mafanikio haya si yangu binafsi, bali ni ushahidi tosha wa kazi kubwa inayofanywa na Benki yetu ya CRDB katika kubadilisha maisha ya watu na kutoa mchango katika uchumi wa bara letu kupitia uvumbuzi wa bidhaa na huduma bunifu, sera madhubuti na ujumuishaji wa huduma za fedha. Kila uchao historia ya bara la Afrika imekua ikiandikwa upya na viongozi wenye maono, taasisi zenye uthubutu na jamii yenye udhabiti. Nafarijika kuwa sehemu ya historia hii ambayo imejidhatiti katika kuwezesha kukuza uchumi wa bara la Afrika kwa mikakati endelevu. Utambuzi huu ni kwa familia yote ya Benki ya CRDB, washirika wetu wa kibiashara, wateja na wananchi wa Tanzania, Burundi na DRC ambapo tunafanya biashara. Kwa pamoja tuendelee kuwa vinara katika kuongoza kwa dhamira ya kuleta mabadiliko chanya. #Top25FinanceLeaders #GameChangers
Abdulmajid Nsekela tweet media
Indonesia
20
12
83
3.1K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Leo imekuwa siku muhimu kwangu baada ya kukabidhiwa ofisi na vitendea kazi kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Chai Tanzania (TBT) katika mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika jijini Dodoma. Nimeyapokea kwa unyenyekevu mkubwa maelekezo ya Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe ya kuwashirikisha wadau wote wa tasnia ya chai kuziondoa changamoto zilizopo ili wakulima wetu na kila mmoja aliyepo kwenye mnyororo wa chai anufaike na fursa zilizopo. Tumeanza kuyafanyia kazi maelekezo ya mheshimiwa waziri kwa kuunda kamati ya wadau. Ni imani yangu kwamba tutapata ushirikiano wa kutosha katika kila mlango tutakaobisha kwa ajili ya msaada tutakaouhitaji tunapoelekea katika utekelezaji. #ChaiYetuFahariYetu
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
Indonesia
8
11
61
2.5K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
I had the pleasure of meeting with the team from the African Development Bank (AfDB) for an insightful discussion on deepening our collaboration to accelerate inclusive finance. A key highlight of our conversation was the Affirmative Finance Action for Women in Africa (AFAWA) initiative, which aligns closely with our mission at CRDB Bank to empower women entrepreneurs and drive gender-inclusive economic growth. By unlocking greater access to capital and capacity-building support, we can uplift thousands of women-led businesses across our markets. Together with AfDB, we are committed to building a stronger, more inclusive financial ecosystem for Africa’s future. Cc: @afdb_group #CRDBBank #AfDB #AFAWA #PartnershipForGrowth #InclusiveFinance
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
English
8
14
113
3.4K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Tumekua na mazungumzo mazuri na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania, Bi. Beatrice Banzi alienitembelea leo ofisini. Nikiwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo, nimempongeza kwa jitihada zinazoendelea kufanywa katika kukukuza sekta ya chai nchini na kumhakikishia ushirikiano wa kutosha katika utendaji wake. Nimemshukuru pia kwa zawadi ya chai kwa kuzingatia matumizi yake katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan. #BodiyaChaiTz #futarikanachai
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
Indonesia
12
16
104
3.6K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Today, I participated in the High-Level Conference on Scaling Finance for Smallholder Farmers in Africa, where I shared insights on Innovative Banking and how CRDB Bank is driving financial inclusion in agriculture. @CRDBBankPlc, we believe innovation isn’t just about new solutions—it’s about rethinking models, policies, and partnerships to make finance accessible, affordable, and impactful. Through digital banking, strategic partnerships, de-risking mechanisms, and value chain financing, we are unlocking opportunities for smallholder farmers. With these approaches, we have successfully reached 10,000+ farmers across the country, facilitating over TZS 2.2 trillion in financing. By embedding fintech solutions and extension services, we ensure smallholders get the right support at the right time. Scaling finance for agriculture starts with reimagining what already works! #InnovativeBanking #FinanceForSmallholders #AgriFinance
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
English
4
11
67
2.3K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
I'm honored to participate in the High-Level Conference on Scaling Finance for Smallholder Farmers in Africa at JW Marriott, Nairobi, organized by @AfDB_Group and #PAFO. I will also join a panel discussion on innovative financing models for agriculture and share @CRDBBankPlc’s approach to supporting smallholder farmers. Join the conversation live! 👇 youtube.com/live/_HquTMwBd…
YouTube video
YouTube
Abdulmajid Nsekela tweet media
English
1
1
14
472
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Leo katika maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani nikiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB ambae ni mmoja kati ya viongozi mahiri wanawake katika sekta ya fedha nchini, Ruth Zaipuna pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB, Adam Mihayo. Mbali ushindani wetu katika biashara lakini sote tunatambua wajibu wetu kwa Taifa letu na kuwa Taifa letu limejengwa katika msingi ya umoja na mshikamano. #TanzaniaKwanza🇹🇿
Abdulmajid Nsekela tweet media
Indonesia
13
16
116
12.7K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Tunapoendelea na maadhimisho ya mwezi wa wanawake ambao kilele chake ni Machi 8, leo nikiambatana na viongozi wengine wa Benki yetu nimepata nafasi ya kutembelea Idara yetu ya Mageuzi ya Biashara na kukutana na watendaji wanawake ambao wapo ndani ya Idara hii. Nimewapongeza kwa mchango wao mkubwa katika kusimamia mpango mkakati wa Benki kibiashara na kuhakikisha kuwa utekelezaji wake unafanyika inavyostahili na kwa muda uliopangwa. Vile vile nimewakumbusha juu ya imani kubwa ambayo Bodi na Menejimenti yetu ipo nayo juu yao na kuwataka kutumia maadhimisho ya mwezi wa wanawake kutafakari yafuatayo. ✅️Kujifunza kujisheherekea mafanikio yao wenyewe bila kusubiri kusheherekewa na mtu mwingine. ✅️Kutambua nguvu kubwa waliyonayo katika kuleta mabadiliko katika taasisi yetu, jamii na dunia kwa ujumla. ✅️Kulinda nafasi ya wanawake katika jamii yetu bila kujali mafanikio waliyonayo katika maisha.
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
Indonesia
4
5
45
2K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Tunapoanza mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, napenda kuwatakia Waislamu wote nchini funga yenye heri na kupokelewa na Mwenyezi Mungu. Tudumishe upendo, amani na mshikamano na kuendelea kuwakumbuka wenzetu wenye uhitaji. #ramadhankareem
Abdulmajid Nsekela tweet media
Indonesia
16
23
375
9.8K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Umekua wakati mwingine mzuri siku ya leo kukutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa TBA (Tanzania Bankers Association), Bi. Tuse Joune. Tumepata wasaa ya kuzungumza mengi kwa maendeleo ya sekta ya benki nchini na kukumbushana wakati ambao tulifanya kazi pamoja nikiwa Mwenyekiti wa taasisi hiyo muhimu kwa mabenki nchini. Vile vile nimepokea na kumshukuru kwa mwaliko wa kushiriki kongamano la tatu linaloandaliwa na TBA kuhusu ujumuishaji wa huduma za kifedha kwa wananchi ambapo nitashiriki katika mjadala kama kiongozi na mdau wa sekta ya fedha nchini.
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
Indonesia
8
7
84
3.7K
Bixen
Bixen@heisbixen·
Ameuliza swali "Bank gani ina customer care mbovu kuliko zote ?" Watu wazitaja Bank zote 😁 thread..
Bixen tweet media
44
20
469
87.7K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Umekua wakati mzuri leo kukutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA Nicodemus Mkama pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Peter Nalitolela. Mazungumzo yetu yamejikita katika kuboresha mahusiano baina ya taasisi zetu ili kuweza kutoa mchango zaidi katika masoko ya mitaji na dhamana. Sambamba na hilo tumeweza kushiriki katika fainali za Shindano la Utafiti chini ya uratibu wa CFA Society E.A(Chartered Financial Analysts Society East Africa). Shindano hili la kila mwaka linatoa fursa kwa wanafunzi wa vyuo kupata mafunzo ya vitendo katika uchambuzi wa masuala ya fedha ambapo kwa mwaka 2024/25 Benki ya CRDB imechaguliwa kuwa taasisi ambayo shindano hilo litajikita katika kufanyia utafiti. Shindano la mwaka huu litahusisha wanafunzi wa vyuo kutoka Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda ambapo mbali na kudhamini shindano hilo, kwa niaba ya Benki yetu nimeahidi kutoa nafasi 5 kwa wanafunzi kutoka Tanzania watakaofanya vizuri kupata ajira. Nimshukuru kaka yangu, CPA Nicodemus Mkama kwa kuahidi kuwa CMSA itawapa mafunzo ya ziada ya vitendo wanafunzi hao watano kabla ya kuajiriwa na Benki yetu.
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
Indonesia
5
7
42
2.4K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Nimekua na mazungumzo mazuri na Mhe. Shaib Hassan Kaduara, Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya namna gani Benki yetu na Wizara yake zinaweza kufanya kazi kwa pamoja ili kuboresha sekta ya maji, nishati na madini visiwani Zanzibar. Benki ya CRDB imekua mdau mkubwa wa maendeleo visiwani Zanzibar kupitia mtadao wetu wa matawi katika visiwa vya Unguja na Pemba ambapo mbali na kutoa huduma za fedha, tumekua tukishiriki katika uwezeshaji wa jamii ambapo kwa miaka 5 iliyopita tumewekeza zaidi ya Bilioni 3.5 katika miradi ya kijamii.
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
Indonesia
1
0
13
806
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
Today, I had an opportunity to attend the second day of the Energy Summit at JNICC in Dar Es Salaam, where I had the pleasure of meeting the esteemed Ambassador of Denmark, Mr. Jesper Kammersgaard, along with his dedicated delegates, Mr. Anders Ørnemark and Ms. Karin Poulsen. Our discussions were inspiring and forward-looking, as we explored the immense potential for collaboration between Denmark and Tanzania. I was truly moved by their enthusiasm for seeking opportunities in our beautiful country and connecting with strategic partners. Together, we can pave the way for sustainable energy solutions and foster meaningful partnerships that benefit both nations. 🇹🇿🤝🇩🇰 #EnergySummitinDar #TanzaniaDenmark #SustainableFuture #GlobalPartnerships
Abdulmajid Nsekela tweet media
English
6
15
128
6.9K
Abdulmajid Nsekela
Abdulmajid Nsekela@amnsekela·
It is an honour to participate and engage with different stakeholders in the Africa Head of State Energy Summit in Dar es Salaam. Collaboration in expanding energy access and expediting the continent's clean energy transition is crucial for our collective future. Through concerted efforts, we can achieve sustainable energy solutions for Africa. #EnergySummitinDar
Abdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet mediaAbdulmajid Nsekela tweet media
English
7
10
97
5.9K