Benjamin
18K posts

Benjamin
@buganzi_
Digital Developer | Computer Engineer



@Positivenga1 @anthony_nyello I support this 100% ila from the original post shida yangu ni kuwa tuna matatizo mengi basic ambayo sidhani kama yanahitaji exposure kuwa solved nahisi ni kuwa tuna watu wasio sahihi. Mfano Kujua kwamba tunahitaji mitaro kuzuia maji yasijae barabarani hili nalo tumeshindwa.


Hii dhana kwamba viongozi wa serikali wanasafiri sana na kupata exposure ya kutosha wala siyo rahisi kama watu wanavyodhani na hata wakisafiri ni kwa kujibana sana na kuwa na predestinated itinerary😬 Pia, kama jamii, hatuna utamaduni mpana wa kusafiri na kujifunza kutoka nje. Lakini hata hivyo, hoja yangu ya msingi haikuwa “kusafiri” pekee. Kusafiri hakumpi mtu exposure. Exposure inakuja pale ambapo kuna intentional learning. Unaweza kusafiri mara nyingi na usibadilike chochote. Na unaweza kusafiri mara chache lakini ukarudi na mabadiliko makubwa ya fikra na utekelezaji. Ndiyo maana katika kujenga taifa, exposure haiwezi kuachwa kwenye bahati, lazima ipangwe kwa makusudi. Utawala wa Nyerere (mnisamehe ninamzungumzia sana) ulielewa hili kwa kiwango fulani. Kulikuwa na jitihada za makusudi za kupeleka Watanzania kusoma katika vyuo bora duniani kwa lengo la kurudi kujenga nchi. Hii si nadharia, ni historia hai maana hata kwenye familia yetu kuna mtu alisomeshwa Harvard. Wapo watu wengi walipelekwa nje kwa dhamira hiyo. Hicho ndicho kinachoitwa closing the exposure gap through design. Ukichunguza nchi nyingi za Asia, hasa China, utaona consistency ya mkakati huu. Kwa zaidi ya nusu karne, wamekuwa wakipeleka vipaji bora kusoma nje, kujifunza mifumo bora, na kurudi nyumbani kutekeleza na wanapewa uwanja wa kutekeleza, pamoja na rasilimali. Hii siyo ajali, ni mfumo wa makusudi mno! Sasa, hata kama hatuwezi kufanya kwa scale hiyo, angalau tunahitaji kuwa na intentionality. Basi tupeleke watu kujifunza kwa muda mfupi, tujenge mifumo thabit ya knowledge transfer na tuhakikishe wanaorudi wana nafasi ya kutekeleza wanachojifunza Bila hilo, exposure inabaki kuwa individual benefit, si national asset. Tukirudi kwenye uhalisia wa Tanzania leo, swali linabaki, kwa nini bado hatuna miji iliyopangiliwa vizuri, safi, na yenye ustaarabu wa hali ya juu? Jibu la swali hili haliwezi kuwa rasilimali pekee. Ni ukosefu wa utamaduni wa learning and benchmarking. Na utamaduni hauji kwa bahati mbaya. Unajengwa kwa makusudi. Kupitia kuona mifumo mingine, kujifunza, na kuamua kuitekeleza kwa mazingira yako. Bila kufanya hivyo, tutazidi kuboresha ndani ya kile tulichokizoea, badala ya kufikia kile kinachowezekana.

Action feem!!! The Night Agent is back. Season 3 is now playing







Good Morning Ma country people🇹🇿






