
God Chuma
2.5K posts





Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Francis Chalamila, leo March 30,2026 amewasilisha taarifa ya mwaka ya utendaji kazi wa TAKUKURU kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo amesema TAKUKURU kupitia oparesheni zake za uchunguzi imefanikiwa kuokoa Tsh. bilioni 14.5 kwenye maeneo mbalimbali. Chalamila amesema “Mh. Rais kupitia oparesheni mbalimbali za uchunguzi TAKUKURU imefanikiwa kuokoa Tsh. bilioni 14.5 ambapo kati ya fedha hizo Tsh. bilioni 10.1 ni fedha taslimu ambayo iliwekwa kwenye akaunti za Taasisi na Idara za Serikali na Tsh.bilioni 4.4 ilidhibitiwa na kurejesha vifaa na mali zilizoelekezwa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo” #MillardAyoUPDATES

Pumzika kwa amani Kaka Bwege!! Huu ni msiba mkubwa kwa wapigania haki!! Tutakupa heshima unayostahili Mzee Wetu!! Heshima umeilinda!


























