Dkt. Resha
24.8K posts






Kuna mtu kakamatwa na Nyama Pori ya Nguruwe kala mvua ya 20yrs,,, wakali wa kupiga Mabilioni wako Uraiani wanaitwa Waheshimiwa Wananchi wa Malawi watafika Mbinguni HOI

Polisi nchini Malawi, wamemkamata Waziri wa zamani wa Fedha kwa tuhuma za utakatishaji fedha na matumizi mabaya ya ofisi. Simplex Chithyola, Kiongozi wa upinzani katika bunge la sasa, alijisalimisha kwa Polisi baada ya kusikia kwamba anatafutwa na wachunguzi. Chithyola alikuwa Waziri wa Fedha kati ya 2023 na 2025 katika Serikali ya Rais wa zamani Lazarus Chakwera. Angalau Mawaziri nane wa zamani wa Baraza la Mawaziri au viongozi wa ngazi za juu wa zama za MCP wamezuiliwa au kuhojiwa na mamlaka kwa shutuma mbali mbali. Wanajumuisha Katibu wa zamani wa Rais na Baraza la Mawaziri Colleen Zamba na Mawaziri wa zamani wa Biashara, Serikali za mitaa, Habari na Kilimo. Sosten Gwengwe, ambaye alimtangulia Chithyola kama Waziri wa Fedha, pia alizuiliwa na kuachiliwa kwa dhamana. Polisi hawajaeleza ni lini Chithyola atafikishwa mahakamani. Waziri huyo wa zamani hajazungumza hadharani kuhusu mashtaka hayo. #KitengeUpdates





















