Dr Godwin .O.Mollel retweetledi

Historia imeandikwa kwa Sekta ya Afya Nchini! Hatimae leo tumeweza kuhitimisha safari tuliyoianza mwaka 2016! Haikuwa safari rahisi lakini waswahili wanasema "kawia ufike"! Hakika Tumeitendea haki sekta ya Afya; Tumewatendea haki watanzania. Na tumeitendea haki nchi yetu. #BimaYaAfyaKwaWote #UniversalHealthInsurance #UHI #Tanzania
---
Mapema leo niliwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote wa mwaka 2022. Kipekee ninawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa kujadili na kupitisha Muswada huu. Hakika Bunge la 13 chini ya Uongozi imara wa Spika Dkt @tulia.ackson Dkt limeweka historia ya kuweka msingi madhubuti na endelevu wa kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za afya bila ya kikwazo cha Fedha. Asante kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge wa Afya na masuala ya UKIMWI chini ya Mhe @stanslaus_nyongo Mb. kwa kazi kubwa na nzuri ya kuuchambua Muswada huu na kutoa ushauri mzuri wa kuuboresha.
Kipekee, ninamshukuru Rais wetu Dkt @samia_suluhu_hassan kwa dhamira yake na utashi wake wa kisiasa wa kuhakikisha tunatunga Sheria hii ili kuwezesha watanzania kupata huduma za afya bila kikwazo cha fedha pindi wanapohitaji huduma hizo na hatimae kuepuka kuingia katika maradhi zaidi, ulemavu wa kudumu, vifo au umaskini kutokana na kukosa fedha za kulipia huduma za afya papo kwa papo.
Shukrani za kipekee kwa Waziri wa Fedha Mhe Dkt @mwigulunchemba kwa ushirikiano mkubwa aliotupatia katika mchakato huu. Aidha ninamshukuru Naibu Waziri wa Afya @dr_mollel na Watendaji wote wa Wizara ya Afya na Taasisi zake, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mchango wao ktk kuandaa na kuwezesha kupitishwa kwa Mswada huu. Sasa ni rasmi Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote namba 8 ya Mwaka 2022 ni sehemu ya Sheria za Tanzania.
Hatubweteki! Tutafanyia kazi maoni na ushauri uliotolewa na Wabunge ili kuhakikisha tunatengeneza mfumo imara wa Bima ya Afya kwa wote. Na pia kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za Afya katika ngazi zote kuanzia ngazi ya Msingi.
#KaziIendelee.




Dodoma, Tanzania 🇹🇿 Indonesia
















