
Ntibha Jackson🎙️
95.8K posts

Ntibha Jackson🎙️
@icon___08
mcee and Song writer ✍️




Huyu mwanachuo amejiua huko kenya 🥹🕊️😭💔

Kanisa la Anglikana Duniani limempata Askofu Mkuu Mwanamke kwa mara ya kwanza baada ya Dame Sarah Mullally, kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo wa juu unaoongoza Waumini takribani milioni 85. Hafla ya kuapishwa imefanyika ikiwa ni hatua rasmi ya kuanza kwa Uongozi wake, licha ya kuwa tayari alianza majukumu hayo tangu Januari mwaka huu. Uteuzi huo wa kihistoria unamfanya Mullally kuwa Mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo tangu kuanzishwa kwa Kanisa la Anglikana, jambo linaloashiria mabadiliko makubwa katika Uongozi wa kidini. Tukio hilo limehudhuriwa na Watu wapatao 2,000, wakiwemo Viongozi waandamizi wa Uingereza kama Waziri Mkuu na Mwanamfalme wa Wales, likionesha umuhimu wa nafasi hiyo kitaifa na kimataifa. Katika hotuba yake ya kwanza, Mullally amesisitiza matumaini na mshikamano, akihimiza jamii kukabiliana na changamoto za dunia yenye migogoro, huku akichukua nafasi hiyo kufuatia kujiuzulu kwa mtangulizi wake, Justin Welby, mwaka 2024 baada ya kukosolewa kuhusu usimamizi wa kesi za unyanyasaji ndani ya kanisa. #MilardAyoUPDATES













