Sabitlenmiş Tweet
Khaled
21.2K posts

Khaled
@meetkhaled_
Travel & Lifestyle Content Creator | Brand Influencer ✈️ I Help You Travel 🇹🇿🇰🇪 📸 Let's Create Good Moments
Katılım Aralık 2021
280 Takip Edilen2.9K Takipçiler
Khaled retweetledi

Usajili wa YouTube Automation Masterclass bado unaendelea. Zimebaki nafasi 15 tu!
Tutaanza 20 April 2026 hadi 23 April 2026, ambapo tuta jifunza kwa kina namna ya kutengeneza faceless YouTube channels, kutumia AI kwenye content creation, kukuza channel, na kila kitu kuhusu monetization ya YouTube kwa mfumo unaoeleweka.
duka.habaritechnology.com/book.php?slug=…
Filipino
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi

Ukweli ni kwamba: . Watakaonunua Bidhaa zako kupitia WhatsApp yako sio watu Mnaojuana nikimaanisha… . …Ndugu & Marafiki . Ukweli Mchungu ni kwamba: . Watakaonunua Bidhaa 
Yako kupitia WhatsApp yako ni watu “USIOWAJUA”
28 April 2024 @NyandaAmosi 🙏
Indonesia
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi

Watanzania kukosa maji liwe ni kosa la jinai.
Dar es Salaam mahitaji yake ya maji kwa siku moja ni lita milioni 570. Uwezo wa uzalishaji wa maji kwa siku moja katika jiji la Dar es Salaam ni lita milioni 530.
Huu mgao mkubwa wa maji mkubwa unaendelea Dar es Salaam ni kwa sababu kuna upungufu wa lita milioni 270 za njia ya mitambo ya Ruvu chini kutoka Mto Ruvu.
Mradi wa maji Kimbiji, Kigamboni unachangia lita milioni 70 pekee. Hivyo, Ruvu Chini unatoa lita milioni 270 + Kigamboni lita milioni 70. Jumla ni lita milioni 340.
Lita za maji zilizobaki zinachangiwa na mitambo ya Ruvu Juu. Kigamboni ndiyo backup iliyobakia kwa sababu inaleta lita milioni 70 kutoka ardhini, siyo mtoni.
Mwaka 2006 kulifanyika utafiti wa kutambua vyanzo vya maji vinavyoweza kutumika kutoa huduma ya maji Wilaya ya Kigamboni ili kukidhi mahitaji ya watu.
Walitafiti uwezekano wa kutoa maji baharini, kutoa maji katika mtambo wa Ruvu juu au chini, na tafiti nyingine iliangalia uwezekano wa kutumia maji kutoka ardhini.
Tafiti iliitwa ‘Future Water City’ ilibainisha, matumizi ya maji yaliyopo ardhini ndio njia pekee sahihi, nafuu na yenye ufanisi itakayoweza kufikisha maji kwa wakazi.
DAWASA iliipa kazi kampuni ya Serengeti kuchimba visima 3, vya majaribio vyenye kina cha mita 600 kwenda chini kubaini eneo linalotoa maji kwa wingi.
Kupitia utafiti wa Future Water City, walibaini eneo la Kimbiji–Kigamboni lililoonekana kuwa na kiwango kikubwa cha maji chini ya ardhi (ground water).
Machi 2013, DAWASA ilisaini mkataba na kampuni ya Serengeti kuchimba visima 20 vya kuzalisha maji kwa gharama ya TZS 26 Bilioni kata ya Kimbiji na Mpera.
DAWASA ilitilia saini na M/s Advent construction Ltd kwa ajili ya ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhi maji la lita milioni 15 linalojengwa kwenye eneo la Kisarawe II,
Pamoja na kazi ya ulazaji wa bomba lenye urefu wa kilomita 5.7 kutoka kituo cha kusukuma maji hadi kwenye tanki kubwa la maji ambalo lipo Kimbiji.
Ujenzi wa tanki la maji Kimbiji, Kigamboni uligharimu kiasi cha TZS 26 bilioni. Mradi huu ukazinduliwa 11 November 2022. Ndiyo unaosambaza lita milioni 70.
Dar es Salaam yenye wakazi 5,383,728 (8.7% ya watanzania wote) kutegemea maji ya mto Ruvu ni kosa kubwa ambalo Serikali timamu ilitakiwa kufikiria.
Population growth ya Dar es salaam inazidi kasi na uwezo DAWASA katika kutafuta suluhusho la kudumu kwa mahitaji ya maji kwa wakazi wa Dar es salaam.
Mabadiliko ya tabia nchi hayatoi uhakika wa kupatikana kwa mahitaji ya maji sasa na miaka inayofuata. Mvua zinaweza kupotea kwa muda mrefu, mito itakauka.
Kama Dar es Saalam inaishi kwa mradi mmoja wa Kimbiji unaozalisha lita milioni 70, uliojengwa kwa TZS 26 bilioni? Vipi ingelikuwepo miradi 10 kama hiyo?
Kukosa vipaumbele. Uwekezaji mdogo Kigamboni visima 15 pekee vinavyotoa lita million 70 kwa siku. Vipi kama wangelikuwa na visima 200 vya kuzalisha maji?
Tanki kubwa la kuhifadhi maji la lita milioni 15. Hivyo, wanajaza tanki hilo kwa siku mara 5 ili kupata ujazo wa maji lita milioni 70, ambazo ndiyo tunapata mgao.
Ujenzi wa Jengo jipya la DAWASA umegharimu TZS 48 bilioni. Kama kipaumbele kingelikuwa ni maji kwa watu wa DSM, pesa zingejenga matanki mawili ya maji.
ATCL na TRC wamesababisha HASARA ya TZS 315.8 bilioni kwa mujibu wa taarifa ya CAG. Hii hasara ingeliweza kujenga matanki 12 kama ya Kimbiji.
Hasara jumuifu (accumulated losses) ya (ATCL) kutoka mwaka mwaka 2014/2015 hadi mwaka 2023/2024 jumla ni TZS 671.98 Bilioni iliyosababishwa na ATCL.
TZS 671.98 Bilioni unajenga matanki 25 kama hayo ya Kimbiji - Kigamboni na miaka 1,000 inayofuata huwezi kusikia Dar es Salaam kuna mgao mkubwa wa maji.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umelipa vituo vya afya huduma HEWA ya Sh14 bilioni. Unalipa huduma hewa wakati wananchi hawana visima vya maji?
Taarifa ya CAG 2021/22 (NHIF) ulipata hasara ya zaidi ya TZS 204 bilioni kwa kufanya malipo hewa na marudio ya malipo huduma kwa mtu mmoja kwa wakati mmoja.
Hizi TZS 204 bilioni ambazo ni hasara ya NHIF, zingelielekezwa kujenga matanki ya maji kama ya Kimbiji, tungefanikiwa kupata matanki 7 ya maji
Mradi wa maji Kigamboni – Kimbiji ulilenga kusambaza huduma ya maji kwa wakazi wapatao 250,000 pindi mradi huo utakapokamilika mwezi Disemba 2022.
Lakini sasa mradi huo ndiyo unalazimika kusambaza huduma ya maji kwa wakazi wapatao 5,383,728 (8.7% ya watanzania wote). Lazima mgao wa maji uwe mkali.
Mahitaji ni lita milioni 570. Maji yanayopatikana sasa ni lita milioni 70, ambayo yalitakiwa kuhudumia watu 250,000 lakini sasa yanahudumia watu milioni 5.4
Inakadiriwa kwamba, ifikapo mwaka 2050 kutakuwa na watuamiaji wa maji milioni 17 kutoka watumiaji wa maji milioni 7.4 waliopo sasa kwa Dar es Salaam pekee.
DAWASA wameshindwa kuhudumia watu milioni 7.4 wataweza vipi kuhudumia watu milioni 20 ifikapo 2050 kwa kutegemea mvua kunyesha wapate maji?
Katika nchi ambazo watawala wanafikiria ustawi wa watu, wananchi kukosa maji kiwango hiki tu cha miezi mitatu mfululizo, walitakiwa KUWAJIBIKA wote.
DAWASA, kuliko kuleta ratiba yenu ya upatikanaji wa huduma ya Maji kwa mpango wa dharura, ilitakiwa DAWASA kuvunjwa, Wizara ya Maji kufutwa kabisa.
Serikali ya CCM miaka 64 baada ya uhuru imeshindwa kuwapa watanzania maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Karne ya 21 maji ni kitu cha anasa. Loh!
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.


Indonesia
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi
Khaled retweetledi















