
Pharmacoreuben ( pharm Cinkey)
3K posts

Pharmacoreuben ( pharm Cinkey)
@pharmacoreuben
Registered pharmacis ( in ❤ with medicaments.💊💊) ensuring better safety of drugs to a patient. Ambassador of AMR with a great interest in public health.








Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kushangazwa na kitendo cha Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina kutoa kero ambazo zimelenga kupata umaarufu wa kisiasa kwa Wananchi na sio kulisaidia Jimbo lake ambapo amesema aliyosema Mpina yanaonesha hajalitendea haki Jimbo lake na hafai kuwa Mbunge wa Jimbo labda awe Mbunge wa kuteuliwa. Akiongea na Wananchi wa Meatu Mkoani Simiyu leo June 17,2025, Rais Samia amesema ““Ndugu yangu Mpina aliomba barabara, madaraja matatu na kuwepo Halmashauri ya Wilaya ambayo Waziri alishasema lakini uwepo wa Halmshauri ya Wilaya huanza na mchakato wa ndani ombi linapelekewa TAMISEMI na huku juu tunamalizia lakini hatoki Mtu kuomba kwa Rais wakati ndani mchakato haujaanza, kwahiyo anzeni mchakato” “Ameomba madaraja na barabara, Ndugu zangu maombi kama haya leo huyu angewasilisha Bungeni na Mawaziri wakatekeleza ombi lake kuleta maombi haya kwa Rais ni kujitafutia umaarufu na kuthibitisha kwamba Mbunge hakulifanyia haki Jimbo lake, angesema Bungeni kazi hii ingefanyika” “La pili kwa sifa alizotoa SGR, Mwl Nyerere, Daraja la Busisi, MV Mwanza huyu sio Mbunge bali Mbunge wa Taifa kwahiyo nadhani tunapokwenda huko muache nimchukue kwenye nafasi zangu 10, mwenzie Leah amesema kila kilichofanyika Jimboni na amaount ya fedha lakini Mbunge wa Kisesa (Mpina) ni kurukaruka na kwamba Kisesa tunakudai lakini ukifuata rekodi za Serikali tumefanya mengi sana Kisesa, amenishangaza kusema Kisesa ipo kama Mwanamke aliyesuka nywele ina maana amedharau Jimbo lake, Ndugu zanvu nadhani mngekuwa serious kutuletea Wabunge wa kukutoleeni huduma kwenye Majimbo yenu, kwahiyo huyu ni Mbunge wa Taifa na sio Mbunge wa Jimbo” #MillardAyoUPDATES




















