Tukikosoa, tukishauri na kuikemea serikali tukiwa mbali, mnasema fimbo ya mbali haiui nyoka.
Wewe ulioko hapo Kongowe umeshaua nyoka wangapi na fimbo yako ya karibu?
Mahakama ya Shanzu, Mombasa nchini Kenya imepanga Juni 17, 2026 kuanza kusikiliza rasmi Kesi ya Ubakaji inayomkabili Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva, Sefu Shaban maarufu kama Matonya.
Hatua hiyo imekuja baada ya kesi hiyo kutajwa leo na kuahirishwa hadi Juni 3, 2026 kwa ajili ya kutajwa tena, baada ya kukamilishwa kwa baadhi ya stakabadhi muhimu kutoka pande zote mbili ambapo hatua za awali za Kisheria zinaendelea kabla ya kuanza kwa usikilizwaji rasmi wa shauri hilo.
Matonya alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Aprili 9, 2026, akikabiliwa na shtaka la ubakaji linalodaiwa kutokea Aprili 7, 2026 katika eneo la Josy Joka Apartments, Kaunti ndogo ya Nyali ambapo anadaiwa kumuingilia kimwili Mwanamke aliyetajwa kwa herufi J.G bila ridhaa yake.
Mbali na shtaka hilo kuu, msanii huyo pia anakabiliwa na shtaka mbadala la kushika sehemu za siri za mtu mzima bila ridhaa ambapo Mahakama ilimpa dhamana ya Shilingi 500,000 za Kenya (takribani Shilingi milioni 10 za Tanzania), kwa sharti la kuwa na mdhamini mmoja Raia wa Kenya mwenye uwezo huo huo.
Aidha, Passport yake imeamriwa kubaki Mahakamani, huku mamlaka za uhamiaji zikipewa taarifa ili kumzuia kusafiri bila kibali ambapo Upande wa mashtaka uliomba kuwekwa kwa masharti magumu zaidi ya dhamana, ikiwemo kuzuiwa kusafiri nje ya nchi bila kibali maalum, wakati upande wa utetezi uliomba masharti nafuu, ukisisitiza kuwa mshtakiwa yuko tayari kushirikiana na Mahakama.
#MillardAyoUPDATES
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema hakujisikia vizuri Watanzania kumsifia refa wa Kenya ingali kuna marefa nchini, akisisitiza kuwa hiyo inamaanisha kuna tatizo kwa marefa wazawa.
🚨 Chelsea have made contact with Andoni Iraola as they step up their search for a new manager. 🔵
Initial talks were described as informal, with the club sounding out his situation and summer plans rather than making a concrete move at this stage. 👀
Iraola is seen as a serious candidate after impressing in the Premier League, but discussions remain at an early stage with no agreement in place yet. ⏳
(Source: Football London)
Mwanasiasa mkongwe na aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Maulidah Anna Valerian Komu, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, huku akitarajiwa kuzikwa kesho.
Marehemu Komu alijiunga na CHADEMA mwaka 1993 akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM), na tangu wakati huo alijijengea nafasi katika siasa za upinzani nchini kupitia majukumu mbalimbali ya uongozi. Akiwa ndani ya chama hicho, aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Waziri Kivuli wa Maendeleo ya Jamii, pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini.
Baada ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Sylvester Masinde, marehemu Komu alikaimu nafasi hiyo kwa muda, akiendelea kushiriki katika maamuzi ya juu ya chama.
Hata hivyo, katika kipindi cha hivi karibuni, jina la Komu liliibuka tena katika mijadala ya kisiasa kufuatia hatua yake ya kufungua kesi mahakamani dhidi ya CHADEMA. Mwaka 2025, kwa kushirikiana na wajumbe wenzake wa Bodi ya Wadhamini, Ahmed Rashid Khamis na Said Issa Mohamed, waliwasilisha shauri la madai namba 8960 wakipinga matumizi ya mali za chama na kuomba zuio la shughuli za kisiasa.
Mahakama Kuu ilitoa amri ya muda iliyozuia CHADEMA kufanya shughuli za kisiasa, hatua iliyosababisha kusimama kwa shughuli nyingi za chama hicho. Katika kipindi hicho, baadhi ya viongozi walikamatwa walipodaiwa kukaidi amri ya mahakama, huku mali za chama zikiripotiwa kuathirika kutokana na kutotumika kwa muda mrefu.
Zuio hilo lilidumu kwa takribani mwaka mmoja kabla ya kuondolewa na Mahakama ya Rufani mwezi Aprili mwaka huu, hatua iliyorejesha shughuli za kawaida za chama hicho.
Aidha, Oktoba 4, 2025, Komu pamoja na wenzake waliwasilisha shauri jingine wakitaka viongozi kadhaa wa CHADEMA, akiwemo Makamu Mwenyekiti John Heche na Katibu Mkuu John Mnyika, wachukuliwe hatua kwa madai ya kukaidi amri ya mahakama. Shauri hilo lilisikilizwa na Jaji Hamidu Mwanga.
@George_Ambangil Mkuu ukiangalia Game kama Ya leo Mzee ukarud ukachek Timu Yako aseee unagundua kumbe tunashabikia watoto sio timu Mzee kazi zinapigwa watu wapo Technical vzr
Ukiacha ufundi wa wachezaji wa timu hizi , hakuna mvivu uwanjani , muda wote wapo on the move , they are so fit .! Run a lot
Athletes with super technical ability