Simba🦁
510 posts


VIDEO:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa wito kwa Watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii, akisema baadhi ya watu wanaposhiriki mitandaoni huonekana kama wanajua yote, wakati kwa kweli hawana uhusiano wala ufahamu wa kweli.
Akizungumza katika Misa ya kuaga mwili wa marehemu William Lukuvi, bungeni jijini Dodoma, Dkt. Nchemba amesema:
"Siku hizi tunatumia vibaya mtandao. Sisi hapa mitandaoni, wapo wengine wakiandika utadhani ni Mungu kaandika. Ukimwangalia mtu mwenyewe anayeandika hivyo, ameshadhulumu dhulumu tu; hata sio msafi, ana madeni kibao na utapeli mwingi. Somo la leo, Baba Paroko, limetusaidia sana kuturudisha binadamu, tuone sisi ni binadamu na safari yetu ni moja."
Ameongeza kuwa, kupata masahihisho ya kuweza kujua nani ananufaika au nani amekosea, ni jambo linalobaki kwa Mungu peke yake.
Filipino

@BlackSingapore2 Hapo unakuta mwana awambia watu ana sister wake yupo Bangkok ni mjasiriamali😄😄
Indonesia

Wafanyakazi wa Gerwill Hotel, iliyopo nyumbani kwa marehemu William Lukuvi, eneo la Area D, Dodoma, wameangua vilio baada ya kupata fursa ya kuuaga mwili wa marehemu ulipofikishwa nyumbani jioni ya leo.
Inaelezwa kuwa jina la hoteli hiyo ya kifahari, Gerwill, limetokana na mchanganyiko wa majina ya marehemu William Lukuvi na mkewe Germina Lukuvi.
Indonesia

MSANII Wakazi kaamua kukata Rufaa ya kesi ambayo hukumu ilitoka anatakiwa kumlipa BABA LEVO MILIONI 100.
This time WAKAZI kampa kazi WAKILI KIBATALA—anyooke nae mahakamani. Kiufupi hii KESI ishaisha kabla haijaanza.😂
Wakazi kaamua kushusha PAPAI NA GOBOLE. Baba LEVO alijinadi anataka hizi hela za wakazi akapelekee watu wa Kigoma mjini wakatengenezewe MADAWATI, nafikili wanafunzi wataendelea kukaa CHINI mpaka yesu ARUDI.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎


Indonesia

@MrDepalitto9 Haya mbona kama matako yako? Tunayajua vzr mno
Indonesia
Simba🦁 รีทวีตแล้ว

@Innocen89950594 @bonifacejoseph_ Watu wanavichwa vigumu kuelewa hilo
Indonesia

@bonifacejoseph_ Hii Biblia Kaiandika Mungu Au Binadamu? Hizi Dini Kazianzisha Mungu Au Binadamu 🤔
Indonesia

Mathayo 28 : 19
“Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.”
2 Wakorintho 13 : 14
“Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu viwe nanyi nyote.”
Hakuna miungu 3, Bali ni Mungu mmoja aliye kwenye nafsi 3.
Yesu kabla ya kupata mbinguni alitupa ahadi ya kutuachia Roho mtakatifu, Matendo ya Mitume 1 : 5, Roho mtakatifu baada ya kushuka watu wote wakajazwa ( wale mitume) Matendo ya Mitume 2 : 4.
Nafsi ya Mwana ndo ilitumwa duniani kuja kutukomboa kwenye utumwa wa dhambi Yohana 3 : 16,
Hapo Mwanzo alikuwapo neno, naye neno akafanyika mwili, akakaa kwetu Yohana 1 : 14., hapo maana yake Yesu alikuja duniani kama Mwanadamu.
Mungu baba yeye kazi yake ilikuwa ni uumbaji, ukisoma kitabu cha Mwanzo
Ray Asel@rayasel94
@bonifacejoseph_ @Makaveli_255 Biblia imethibitisha haya unayosema?
Filipino

Mwigizaji Mkongwe na Mwanamichezo wa Sanaa za Mapigano (Martial Arts) Chuck Norris amefariki dunia hii leo Machi 20, 2026 akiwa na umri wa miaka 86, wakati akipatiwa matibabau katika Hospitali ya Hawaii nchini Marekani.
Taarifa za kifo chake zimethibitisha na Familia yake kupitia Mitandao yake ya Kijamii ambapo imeeleza “Kwa huzuni kubwa, Familia yetu inawataarifu kutokea kwa kifo cha ghafla cha mpendwa wetu Chuck Norris, na tungependa sababu za kifo chake zibaki kuwa za siri, tungependa mfahamu kuwa amefariki akiwa amezungukwa na Familia yake na alikuwa katika hali ya amani.”
Aidha Chuck Norris alijipatia umaarufu katika filamu kwanzia miaka ya 1970 mpaka 80 akiigiza Filamu maarufu zilizofanya vizuri duniani kama vile Walker, Texas Ranger, The Delta Force, Missing in Action, Good Guys Wear Black (1978), The Octagon (1980), Lone Wolf McQuade (1983), Code of Silence (1985) na Firewalker (1986), The Expendables 2 (2012) na nyinginezo nyingi.
#MillardAyoUPDATES

Filipino

HABARI:
📍IRINGA - Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imemhukumu Askari Polisi namba F.4987, Sajenti Rogers Mmari wa Kituo cha Polisi Ipogolo, kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia kijana Nashon Kiyeyeu, mkazi wa Ipogolo, Manispaa ya Iringa, Desemba 14, 2024
Hukumu hiyo imetolewa jana Machi 19, 2026 na Jaji Angaza Mwipopo baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na kujiridhisha bila shaka kuwa mshtakiwa alihusika na tukio hilo.
Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa Mahakamani, Sajenti Rogers alipokea taarifa kutoka kwa mwananchi Beatrice Kimata aliyedai kuwa marehemu aliiba simu yake. Kufuatia taarifa hiyo, askari huyo alimtafuta Kijana huyo na alipompata alianza kumpiga akimtaka arejeshe simu hiyo.
Ilielezwa mahakamani kuwa kipigo hicho kilisababisha majeraha makubwa kwa marehemu hadi kupoteza fahamu. Baadaye alipelekwa katika hospitali binafsi kwa matibabu, lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya na hivyo kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Iringa, ambako alithibitishwa kufariki dunia.
Mahakama pia ilibaini kuwa, licha ya kumshambulia marehemu, mshtakiwa hakuwahi kufungua kesi rasmi kuhusiana na tuhuma za wizi dhidi yake.
Katika utetezi wake, Sajenti Rogers alikiri kumpiga marehemu, akidai kuwa kijana huyo alikuwa akimjibu vibaya wakati wa mahojiano.
Baada ya kusikiliza mashahidi sita wa upande wa Jamhuri na watatu wa upande wa utetezi, Mahakama ilimtia hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia, kinyume na vifungu vya 195 na 198 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu, na kumhukumu kifungo cha miaka miwili jela.
Hata hivyo, baba mzazi wa marehemu Nashon Kiyeyeu ameonyesha kutoridhishwa na hukumu hiyo, akidai kuwa tukio hilo lilifanywa kwa makusudi na kuomba serikali pamoja na wadau wa haki kuingilia kati ili kuhakikisha haki inatendeka kikamilifu.

Indonesia

















