Chiggs
61.7K posts








VIDEO: Marekani imeshuhudia moja ya maandamano makubwa zaidi ya kiraia katika miongo ya hivi karibuni, huku vuguvugu la "No Kings" likiwaunganisha maelfu ya wananchi katika miji mbalimbali nchini humo kupinga sera za Rais Donald Trump kuhusu vita, uhamiaji, na hali ngumu ya maisha. Kuanzia miji mikubwa kama New York, Los Angeles, na Washington DC, hadi miji midogo ya mashambani, waandamanaji wameonekana wakiwa na mabango yenye ujumbe mkali dhidi ya kile wanachokiita "utawala wa mkono wa chuma" na maamuzi ya kijeshi yanayoigharimu nchi hiyo. Waandamanaji wameainisha maeneo makuu matatu yanayochochea hasira zao ambayo ni sera za vita, na hapa wakiwa na pingamizi dhidi ya ushiriki wa Marekani katika mivutano ya Mashariki ya Kati na uwezekano wa kuingia kwenye vita vya moja kwa moja na Iran, uhamiaji ambapo kuna ukosoaji mkubwa wa hatua kali za kisheria na ukamataji wa wahamiaji unaoendelea nchini kote na kilio cha kupanda kwa bei za bidhaa, nishati, na huduma muhimu, jambo linalowaumiza raia wa kipato cha chini.

























I am proud to join Americans across the country today to say loudly and clearly: We will not accept authoritarianism. We will not accept oligarchy. And we will not accept a president who undermines the Constitution every single day. twitter.com/i/broadcasts/1…

















