

Liberatus Mwang'ombe
35.9K posts

@Liberatus80
Center-Right. Human Rights Activist. Retweets are not endorsements. Values: Ujasiri (Courage), Uhuru (Freedom), Umoja (Unity).












Leo tarehe 23 Machi 2026, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa Wanu Hafidh Ameir (Mb) amewasili nchini Afrika Kusini kwa Ziara ya Kikazi. Mara baada ya kuwasili alipokewa na Balozi James G. Bwana pamoja na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania. Dhumuni la Ziara hiyo ni kuimarisha na kudumisha zaidi wigo wa ushirikiano wa kielimu kati ya Taasisi za Elimu ya Juu za Tanzania na Afrika Kusini. Akiwa jijini Cape Town hii leo, Mheshimiwa Naibu Waziri Ameir (Mb) amepata fursa ya kukutana na Wawakilishi wa Wanafunzi Watanzania wanaosoma katika Vyuo Vikuu vilivyopo Cape Town wa Shahada za Uzamivu (PhD); Uzamili (Masters) pamoja na Shahada za Kwanza katika Tahsusi mbalimbali. Wakati wa Mkutano wake na Wanafunzi hao Mheshimiwa Naibu Waziri Ameir (Mb) ameelezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ili kuboresha mazingira ya elimu na kujifunza katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwaasa kuwa Mabalozi wazuri wakati wote wa masomo yao nchini Afrika Kusini.













