OfficialBBTYIA

392 posts

OfficialBBTYIA banner
OfficialBBTYIA

OfficialBBTYIA

@BBTKilimo

Updates on Building Better Tomorrow Project - YIA under @wizarakilimo

Katılım Nisan 2023
10 Takip Edilen920 Takipçiler
OfficialBBTYIA
OfficialBBTYIA@BBTKilimo·
Building a Better Tomorrow - Block Farm visit - Chinang’ali. Tunaendelea kukaribisha wageni mbali mbali waje kujifunza na sisi kwa vitendo. #KilimoNiBiashara
Indonesia
4
11
11
1.7K
OfficialBBTYIA
OfficialBBTYIA@BBTKilimo·
Tunaendelea kukaribisha wageni mbali mbali ambao wangependa kujifunza kuhusu BBT Block Farm. Asanteni sana @lamataleah1 Village na @mkandamizaji kwa kututembelea Waambieni BBT tuko POA na tunaendelea na Kilimo Biashara.
Filipino
1
17
19
1.8K
OfficialBBTYIA
OfficialBBTYIA@BBTKilimo·
Uzinduzi rasmi wa benki hii utafanyika tarehe 28 Aprili 2025, ukiongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. BBT Amcos tuna imani benki hii itakua kiungo muhimu katika uwezeshwaji wa kiuchumi kwa wakulima nchini. Cc @WizaraKilimo @HusseinBashe
Indonesia
1
4
12
2K
OfficialBBTYIA retweetledi
Hussein M Bashe
Hussein M Bashe@HusseinBashe·
Asante sana kwa maswali ambayo naamini yanalenga kuhabarisha umma kuhusu maendeleo ya mradi. Awali ya yote nichukue nafasi hii kusisitiza tena, hata mradi huu ni jitihada za maksudi za Mhe Rais Dr. @SuluhuSamia katika kuleta mapinduzi kwenye Sekta ya Kilimo. Hili pia limedhihirika kupitia bajeti ya Wizara ya Kilimo Hadi kufikia trilioni 1.2 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na sote tunafahamu kilimo ni UWEKEZAJI. Kujibu maswali yako… Project ya BBT imefikia wapi? Kwanza ni muhimu tuelewe components za mradi wa BBT ni zaidi ya block farms. Ina components hizi 5 zote zinazolenga vijana na wanawake - 1) Mashamba Makubwa ya Pamoja (BBT Block Farms), 2) Utoaji wa Mitaji kwa Vijana na Wanawake 3) Uchimbaji wa Visima kwa Wakulima Wadogo 4) Huduma za Ugani, na 5)Uongezaji Thamani wa Mazao. Hadi kufikia Januari 2025 - Jumla ya ekari 340,244.98 zimetengwa kwa ajili ya kilimo cha vijana, kutoka ekari 300 zilizokuwa wakati wa uzinduzi wa programu. - Vijana 686 tayari wanazalisha kwenye mashamba ya Chamwino Dodoma (Chinangali na Ndogowe) mnakatibishwa kutembelea na hivi karibuni tutakua na site visits za kujionea kwa makundu mbali mbali na kujifunza - Programu imeendelea na uwekezaji wa umwagiliaji, usambazaji wa pembejeo, na utoaji wa mikopo. Ni vijana wangapi wameshafaidika na hii project mpaka sasa? - Hadi Desemba 2024, jumla ya vijana na wanawake 43,163 kupitia component zote 5 wamenufaika moja kwa moja kupitia programu ya BBT, ikiwa ni kupitia Wizara ya Kilimo, taasisi zake na Wadau wa Maendeleo. Awamu ya kwanza imeleta matokeo gani mpaka sasa? - Ingawa awamu ya 1 haijaisha- Vijana 686 wameanza uzalishaji katika mashamba ya Chamwino, Dodoma. - Shamba la Chinangali (ekari 1,772) limeanza kuzalisha mazao mbalimbali kama mbegu za alizeti, pilipili, mtama, maharagwe kunde, na mahindi. - Vijana 249 wamepata mafunzo ya usambazaji mbolea na uzalishaji mbegu. - Katika shamba la Ndogowe, vijana 418 wamekabidhiwa ekari 10 kila mmoja kwa ajili ya kilimo. - Kituo atamizi cha Mkonge Tanga na Zanzibar kimewezesha vijana 344 kuzalisha bidhaa za mkonge. Kuhusu Investment na Value for Money - Serikali na wadau wamewekeza jumla ya TZS 2.64 trilioni kwa kipindi cha 2022-2030, ambapo 24% ya bajeti inatoka serikalini na 76% kutoka kwa sekta binafsi na washirika wa maendeleo. Katika msimu wa 2024/2025, kipato tarajiwa ni faida ya TZS 1.94 bilioni baada ya gharama za uendeshaji. Kwa kiasi gani? Tunajivunia uwekezaji huu uliotengeneza ajira, kuimarisha uzalishaji wa kilimo, na kuwezesha vijana kumiliki mashamba na mitaji. Uwekezaji katika umwagiliaji, upatikanaji wa ardhi, na huduma za ugani umeleta tija kubwa katika uzalishaji wa mazao. Licha ya mafanikio haya, bado kuna changamoto za upatikanaji wa masoko na ushirikishwaji wa vijana wengi zaidi ila hili najibu hapo chini Tumefika hatua gani na tunaelekea wapi? BBT inaendelea kupanua wigo wake kwa kuanzisha mashamba mapya kama Mapogoro-Chunya (ekari 51,528.5) na kuendelelea na Ujenzi wa miundombinu kama mabwawa ya umwagiliaji, barabara, na minara ya mawasiliano unaendelea. Mikopo kwa vijana kupitia mfuko wa pembejeo inaendelea kutolewa, ambapo hadi Desemba 2024 maombi ya mikopo yenye thamani ya TZS 21.3 bilioni yalipokelewa, na TZS 5.24 bilioni ziko kwenye hatua za kutolewa. Tumefika ngazi ya halmashauri na ekari 148,563.91 zimetengwa kwa ajili ya programu ya BBT. Natumai nimejaribu kujibu maswali yako. Salaam Aleikum.
(---) Onesmo Mushi@EduTalkTz

1. Project ya BBT imefikia wapi mheshimiwa Bashe? 2. Report ya utekelezaji wake tunaipata wapi na sisi tuipitie? 3. Ni vijana wangapi wameshafaidika na hii project mpaka sasa? 4. Awamu ya kwanza imeleta matokeo gani mpaka sasa? 5. Thamani ya fedha iliyowekezwa inaendana na matokeo yaliyopatikana? 6. Kwa kiasi gani? 7. Tumefika hatua gani na tunaelekea wapi? Umma wa watanzania ungetamani kufahamu haya Mheshimiwa.🙏🏿

Indonesia
105
68
275
53.7K
OfficialBBTYIA retweetledi
Hussein M Bashe
Hussein M Bashe@HusseinBashe·
#3rdG25AfricanCoffeeSummit 21-22 February 2025 Dar es Salaam Declaration 2025 - Tamko la Dar es Salaam linaweka mkazo kuwekeza kwa vijana na kahawa. Leo Nchi 10 zimetoa ahadi za kuungana na tamko hili linalolenga kuimarisha sekta yetu na kuwapa vijana ajira.
Hussein M Bashe tweet mediaHussein M Bashe tweet mediaHussein M Bashe tweet mediaHussein M Bashe tweet media
Filipino
8
35
103
4K
OfficialBBTYIA retweetledi
Hussein M Bashe
Hussein M Bashe@HusseinBashe·
3rd G25 African Coffee Summit. 21-22 February, Dar es Salaam Tanzania.
Hussein M Bashe tweet media
English
8
22
71
4.1K
OfficialBBTYIA
OfficialBBTYIA@BBTKilimo·
Uvunaji huo unatumia teknolojia ya kisasa ambapo mashine yenye uwezo wa kuvuna zaidi ya ekari 25 kwa siku inatumika. Utekelezaji wa Programu ya BBT ulianza na kilimo cha Alizeti katika shamba la Chinangali mwezi Februari 2024. Uvunaji huo unaendelea kwa takriban siku 15.
OfficialBBTYIA tweet mediaOfficialBBTYIA tweet media
Filipino
1
0
0
156
OfficialBBTYIA
OfficialBBTYIA@BBTKilimo·
Utekelezaji wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) umeanza kutoa matokeo chanya kwani wanufaika wa BBT wameanza uvunaji wa zao la Alizeti katika shamba la Chinangali, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kwenye shamba lenye ukubwa wa ekari 620.
OfficialBBTYIA tweet mediaOfficialBBTYIA tweet mediaOfficialBBTYIA tweet mediaOfficialBBTYIA tweet media
Filipino
3
0
1
261
OfficialBBTYIA
OfficialBBTYIA@BBTKilimo·
hii ya BBT,” alisema Bw. Joseph John mnufaika wa mradi huo wa BBT. Programu ya BBT hivi sasa imeanza kutekelezwa kwa kuanza na kilimo cha alizeti katika shamba la Chinangali mwezi Februari 2024 na tayari uvunaji umeanza, na kuendelea kwa takriban siku 15.
OfficialBBTYIA tweet media
Filipino
1
0
0
101
OfficialBBTYIA
OfficialBBTYIA@BBTKilimo·
BBT YAANZA NA UVUNAJI WA ALIZETI KATIKA SHAMBA LA CHINANGALI Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (Building a Better Tomorrow -BBT) imeanza kuneemesha wanafuika wa programu hiyo kwa kuanza uvunaji wa zao la alizeti tarehe 19 Juni 2024 katika shamba la Chinangali mkoani Dodoma.
OfficialBBTYIA tweet mediaOfficialBBTYIA tweet mediaOfficialBBTYIA tweet mediaOfficialBBTYIA tweet media
Filipino
2
0
4
224
OfficialBBTYIA
OfficialBBTYIA@BBTKilimo·
Waziri @HusseinBashe mapema wiki hii amepata fursa ya kukagua uchimambaji wa mabwawa, hali za mazao yaliyozalishwa na kuzungumza na viongozi wa wanaushirika wa wanaufaika wa BBT Chinangali pamoja na wataalam wa Wizara ya Kilimo wanaosimamia utekelezaji programu ya BBT kwa ujumla.
OfficialBBTYIA tweet mediaOfficialBBTYIA tweet mediaOfficialBBTYIA tweet media
Indonesia
1
0
3
311