Msamaria retweetledi

Je, wale waliopoteza viungo vyao vya mwili? Waliokatwa masikio? Waliogongwa misumari miguuni? Waliofanya ukatili wa kutisha kama kulawitiwa wakati wakimtetea Mzee MBOWE akiwa mbunge wa HAI, wamepewa faraja au kuombwa msamaha? Wengine walilazimika kutelekeza familia zao na kuwa wakimbizi kwa kuhofia usalama wao. Hali hii inajenga picha kuwa Mzee MBOWE ameweka maslahi yake binafsi mbele na kusahau gharama kubwa waliyolipa wafuasi wake. Hii ni dhihaka kwa watu wote ambao waliwahi kuamini katika njia zake. Hii inatuogopesha ambao tumewahi kumpambania hadharani. Hata hivyo, SABAYA anatakiwa kuomba msamaha mwenyewe, siyo kuombewa msamaha. Kimsingi, msamaha ni jambo la kibinafsi na la kimaadili kati ya mtu aliyekosea na yule aliyekosewa. Msamaha wa kweli unahitaji sauti ya mkosaji mwenyewe.


Indonesia











