
๐ซ๐๐๐๐ ๐ฑ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐ฑ.๐น๐ฟ
12.8K posts

๐ซ๐๐๐๐ ๐ฑ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐ฑ.๐น๐ฟ
@DaJaden255
SDGs:Environmentalist || passionate about Climate Change|| Climate Change Activist โป๏ธ||Former Assistant DCO-HJFMRI |WRP-Tz || @YUNA_Tz @UN-C. #climateAction



Mwanamziki, Malkia Karen kupitia ukurasa waka Wa IG. Ameshare picha na kusema kuwa amepigwa na Baba watoto wake au Mpenzi wake ambae pia ndio manager wake. Soma mwenyewe... Screenshot kwa Comments ๐












Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly, akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2026/27, amelitaka Bunge kukataa bajeti ya zaidi ya shilingi trilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali mpya ya Muhimbili akishauri fedha hizo zielekezwe katika ujenzi wa Hospitali za Mikoa ili kupunguza mzigo katika Hospitali hiyo. โHili jambo tusilikubali na nimuombe Waziri Mkuu kama lipo kwenye Wizara ya Afya, limekuja kwenye Kamati na kuna mambo yanafanyika, naomba Bunge hili liende likafanye utafiti tusikubali kwenda kujenga Hospitali ya Muhimbili kwa shilingi trilioni 1 na bilioni 400 haiwezekani na mimi niko hapa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi,โAeshi Hilaly - Mbunge wa Sumbawanga Mjini. Akitolea ufafanuzi suala hilo, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi amesema, โJambo linaloendelea kwa ajili ya Muhimbili si ukarabati ni ujenzi wa Muhimbili mpya ni kweli ujenzi huo utatumia trilioni 1.2 na ni mkopo lakini lengo ni kuwa na hospitali bora zaidi Muhimbili ya sasa imeshindwa kupata ithibati kutokana na majengo kusambaa na kutumia eneo kubwa. Mpango huu ni mahsusi kwa ajili ya kujenga Muhimbili mpya yenye uwezo wa kulaza wagonjwa 1,300, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa majengo na usimikaji wa mitambo yote, na itatekelezwa kwa awamu saba.โ #MillardAyoUPDATES



























