Ni kweli kuna makabila wanafanya kazi ila kuna wale jamaa wa kigoma wanaitwa waha ni mashine za kazi.
Sijawahi ona muha mzembe mzembe na ni kama waliambiwa ukiondoka Kigoma usirudi mpaka ufanikiwe.
Kwenye kupiga kazi tu nawapa maua yao sema ndio hivo wana ubishi mlima😁🙌
@safarimlevi Bahati nzuri mwanaharakati inasound vibaya kwa mafisadi na waziba rizki za wenzao.. neno harakati ni mapambano ya kutetea watu juu ya uminywaji wa haki zao katika mambo mbali mbali.. sasa ukiitwa mwanaharakati, hiyo bado ni credit kubwa maana wewe unasimama na wengi kwenye haki
@SkydiverTz@MkulimaKante Nilidate na limams la kiha sema nalikubali mpaka nitakapo fuliwa na kifusi ambacho nyie mnaita kaburi.. Lilikuwa real sana kama alarm ya saa, haliendi kinyume na makubaliano na ukilizingua linapiga mayowe.. Lilitaka linipe mtoto nikasema huu mtego siingii
@lifeofmshaba Meter 10 ni chini ya urefu wa kiduara cha penalty hadi ulipo mstari wa goli. Sasa chande sijui alikuwa anakaririshwaje madesa ya kitoto hivi
Hivi Chande anajua mita 10 zina urefu gani ?
Hiyo nyumba amesema ilikuwa na mfunzo kutoka kituo cha polisi anajua mita 10 ni kama kuwa chumba cha pili kwenye jengo moja ?
Sheikh Mussa Kundecha, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Maimamu na Viongozi wa Kiislam Tanzania
Baraza Kuu la Maimamu na Viongozi wa Kiislam Tanzania wanasema wanaopinga na kukosoa ripoti ya Chande ni wahalifu na walihusika katika matukio ya Oktoba 29, 2025. Nafikiri hawa watu hawajitambui kabisa.
Bahasha za kaki zimewalevya. Wamepagawa kabisa. Waelezwe. Watu hawapingi sura za watu wanaounda tume. Watu walipinga muundo wa tume, hadidu za rejea na sasa wanapinga na kukosoa maudhui yake.
Wameshindwa kusimamia ukweli (wanashangilia mauaji ya raia yaliyofanywa kikatili). Wameamua kuvunja mkataba wa kiimani baina yao, waumini, na Mungu. Huwezi kuombea amani wakati unashangilia mauaji.
Uhai ni zawadi ya juu (Sacredness of Life) kutoka kwa Mungu. Tofauti na makosa mengine ya kijamii, mauaji hayawezi kurekebishwa. kuukatisha uhai ni kosa ambalo halina fidia ya kutosha duniani (irreversible).
Kiongozi wa dini anapowatetea wauaji; Anahalalisha utamaduni wa mauti. Anapoteza uhalali wa kukemea dhambi ndogo kama wizi au uongo. Anageuza nyumba ya ibada kuwa kimbilio la watawala wenye nguvu.
Imani inapaswa kuwa mwanga unaotuongoza kuuona ukweli, na si pingu zinazotuzuia kuhoji au kuona uhalisia. Imani isiwe kifungo cha akili. Haki huinua taifa, bali dhambi ni fedheha kwa watu wowote.
@Balyx_ Leo lazima wataongezewa mshahara on paper tena itakuwa kati ya 8%-10% hapo. Ila kwenye slip zao wataona manyoya tu. Lengo la kutangaza nyongeza ya mshahara litakuwa lilelile kuzima mijadala kuhusu hotuba ya Chande na Mo29. Bahati mbaya tu, Kwasasa ile haifutiki kwenye vichwa
@WideEdson Red colour kwa Bajaj haijwahi kuchuja, alafu inapokea sticker ya aina yoyote ile.. pia sio rahisi kupauka kama nyeusi na blue.. kijani siitaji kwasababu ya kulinda heshima ya Watanzania wenzetu Mo29..
Kila jambo lina wakati wake!
Nilitafutaga TIN Number ya Biashara wakati flani nafukuzia maokoto ya Elon Musk, Mwisho wa siku nikafeli.
Huwezi amini leo Madam pale NMB kapinigia simu ananiomba Tin Number ya Bishara na Nichague rangi ya Bajaji yangu ya mkopo.!
Rangi ipi apo?