@TBoundBuses Wana masharti magumu sana wachina hapo, Nchi yetu ila wanatupangisha kwa masharti,
Ofisi za mabasi wanataka 10 tu, halafu kila BUS Route 1, so nasisi tumekosa kwa sababu Route zimejaa,
Kwa sasa wanahitaji Msafirishaji anayekwenda Congo tu
@SamsonErnest_ Kila safari ya KiMungu lazima iwe na misukosuko japokua wengi misukosuko huwa haituitaki, na angetuonesha mapema kuwa kutakua na misukosuko hakuna mtu angeikubali huduma/UTUME
Mungu alimwambia Musa aende nchi ya ahadi ila hakumwambia habari za migogoro itakayomkuta njiani na changamoto iliopo kwenye nchi ya ahadi, unaweza kupata maelekezo ya Mungu ya kwenda eneo lenye kila kitu unachokihitaji, ila asikuambie changamoto utakazokutana nazo.
Moto ulioanza nao katika usomaji wa neno la Mungu na kutafakari, hakikisha unautunza siku zote. Na kama umezima ndani yako, uwashe tena. Mungu yupo tayari kukusaidia.
MJARIBU SHETANI HAMWOGOPI MWOMBAJI MZURI
Mt 4:3 SUV
[3] Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.
Yesu akiwa kwenye maombi ya siku 40 ya kufunga, alikutana na mjaribu shetani. Tukio ambalo linatupa mshangao na kushtuka kidogo, maana tulitegemea mtu akiwa kwenye maombi mazito namna hiyo asingeweza kusogelewa na Shetani.
Nataka ujifunze jambo hapa, hasa ukiwa mwombaji mzuri, baadhi hufikiri shetani hawezi kutusogelea na kutujaribu wakati tupo kwenye maombi makali.
Ukiwa mwombaji Sana, utakutana na mjaribu, tena wakati ambao upo karibu sana Mungu wako.
Kukutana na mjaribu shetani haimaanishi kuna mahali umekosea mbele za Mungu.
Mjaribu anakuja kwako ili umkosee Mungu wako, na si kana kwamba umekosea ndio maana amekusogelea.
Tunapata funzo kubwa sana hapa kuwa tunapaswa kujaa neno la Mungu, ndipo tutaweza kukabiliana na mjaribu.
Mt 4:4 SUV
[4] Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Mtu asiye na neno la Mungu la kutosha, anaweza akaingia kwenye mtego wa mjaribu, na akiwa kwenye maombi yake.
Nasema hivyo kwa sababu sio ajabu ukamkuta mwombaji amenasa kwenye mtego wa dhambi.
Narudia shetani haogopi waombaji kama unavyofikiri, anaogopa mwombaji mwenye neno, ambaye hawezi kumdanganya na kumwingiza kwenye mitego yake miovu.
Mjue Mungu unayemwomba na kumwamini kupitia neno lake, ili ajapo mjaribu asiweze kukutoa kwenye mstari wa ki-Mungu.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Hii nchi kuna barabara ya kutoka Dumila pale feri kwenda hadi madizini Turiani sijui ni contractor gani alijenga pale. Oya ni bonge la barabara bwana. Hongera yake.
Usiwakorofishe watoto wako kila mara bila sababu za msingi, ukiwa kama mzazi/mlezi epuka uchokozi kwa watoto. Unaweza kuwavunja moyo na kuwakatisha tamaa, na wakakosa heshima kabisa kwako.
Binti kama una tumbo la kuzaa zaa kwa juhudi sana.
Mimi na mke wangu mwaka wa tano huu tunahangaika kutafuta mtoto mpaka kwa sasa tuna mpango wa kwenda kuadopt tu maana kama mahospitali yote tushamaliza, mpaka dawa za kienyeji wapi.
Walaaniwe wanaotupa watoto💔