
Halafu kesho anakuwekea mikono kichwani😂😂😂. Bora mapepo yaniue!
WHITE HOUSE
12K posts


Halafu kesho anakuwekea mikono kichwani😂😂😂. Bora mapepo yaniue!

Mimi sio muoga na naona kila kitu ila busara zangu zimenituma nisiongee chochote,sitaki kuzua mjadala mwingine katika kipindi hiki kigumu(watu hawajapona bado)..Mungu atatuvusha salama na ipo siku tutaongea vizuri kabisa





Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema imesikitishwa na taarifa za upotoshaji kuhusu matamshi yasiyo sahihi yanayosambazwa kupitia Mitandao ya Kijamii kufuatia Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo iliyowasilishwa Bungeni Jijini Dodoma Mei 26, 2026. Miongoni mwa mijadala iliyoibuka mitandaoni ni kuhusu msimamo wa Serikali juu ya kutokuingiliwa katika mambo ya ndani ya Nchi. Katika taarifa iliyotolewa leo Mei 28, 2026 na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara hiyo imesema taarifa zinazosambazwa mitandaoni zimepotosha maudhui halisi ya hotuba hiyo kwa makusudi kwa lengo la kuleta mkanganyiko kwa Umma na kuathiri taswira ya Nchi pamoja na misingi ya Diplomasia, Uhuru na Mshikamano wa Kitaifa. Kutokana na hali hiyo, Wizara imesema itaendelea kutoa ufafanuzi rasmi kupitia Vyombo vya Habari na majukwaa mbalimbali ya mawasiliano ili kuhakikisha Wananchi wanapata taarifa sahihi na zenye muktadha stahiki wa Serikali kuhusu masuala yaliyojadiliwa katika hotuba hiyo. “Wizara inatoa wito kwa watumiaji wa Mitandao ya Kijamii, wadau wa Habari na Wananchi kwa ujumla kutumia Uhuru wa kujieleza kwa kuzingatia Weledi, Maadili, Sheria za Nchi pamoja na wajibu wa kulinda amani, mshikamano na heshima ya Taifa letu,” imeeleza taarifa hiyo. Bajeti hiyo iliwasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo. #MillardAyoUPDATES










Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema Tanzania inathamini mchango wa washirika wa maendeleo katika kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali, lakini ameeleza kuwa ushirikiano huo unapaswa kujengwa katika misingi ya heshima, nidhamu na kuthamini uhuru wa Taifa. Nape amezungumza hayo Jumanne Mei 26, 2026 bungeni Dodoma wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Aidha, amesema Tanzania imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na marafiki zake wa kimataifa, hivyo changamoto za muda mfupi haziwezi kuwa msingi wa kupima mahusiano hayo.