
mzalendo🇹🇿
35.1K posts

mzalendo🇹🇿
@Hamadbakari2
mjasiriamali wa Mtaani , ( BABA) muumini wa democrasia na utawala bora, ndio msingi wa maendeleo🙏






#BREAKING: MWILI WA BAHARIA WA KITANZANIA ALIYEUAWA KATIKA SHAMBULIO LA STRAIT OF HORMUZ WAREJESHWA NYUMBANI Mwili wa baharia wa Kitanzania Mchama Maregesi Mongu, aliyeuawa tarehe 3 Mei 2026 kufuatia shambulio la bomu dhidi ya meli iliyokuwa ikipita katika Mlango wa Strait of Hormuz, umefika nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mongu alikuwa akihudumu kwenye meli ya kuvuta VOLANS (IMO No. 929856), iliyosajiliwa chini ya bendera ya Falme za Kiarabu (UAE), wakati iliposhambuliwa ikisafiri kutoka UAE kuelekea Oman. Mamlaka ya Usafirishaji wa Baharini Tanzania (TASAC) ilithibitisha utambulisho wake na kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuratibu urejezwaji wa mwili wake. Mashirika ya kimataifa ya baharini, yakiwemo IMO, yameonya kuwa mashambulio ya aina hiyo yanaonyesha hatari kubwa kwa mabaharia na biashara ya kimataifa, yakisisitiza umuhimu wa kulindwa kwa haki ya kupita bila kuingiliwa chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria za Bahari (UNCLOS).






































