Jackson
5.8K posts


Iraq ilipigwa na US ndani ya wiki moja tu walikuwa hawana hata uwezo wa kurusha mshale nje ya Iraq.Lakini Iran hadi leo wiki ya 3 wanashambuliwa na wao wanashambulia tena kwa nguvu kama vita ndo inaanza.
Ninini kinaitofautisha Iran ya sasa na Iraq ya kipindi kile?
#BilaGanzi


Indonesia

@Sativa255 Ubunge kwa miaka 31? Ndio maana kila siku walikua wakisema vijana waende veta
Indonesia
Jackson retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_MGAWANYO_MALI_ZA_CHADEMA
Part 8
Anasimama Wakili Hekima Mwasipu kutoka upande wa waleta maombi.
Anasema kuhusu haki ya kusikilizwa tunaomba kusema kwamba respondents baada ya Jebra kujiondoa hawakuambiwa chochote.
Descretion tunasema inapaswa kuzingatia haki na Katiba ya nchi sasa alichokifanya Jaji Mwanga ni kuendelea na kesi kinyume na Matakwa ya kuexercise judiciously hiyo descretion.
Anasimama Dr. Nshala Ruge anasema sisi tulisema cause of action ilianza lini na sisi tulisema walianza 2016
Para zote walizosema ukianza na Para ya 7 wanasema wamemaliza kujenga jengo la Chama hawajasema kama kulikuwa na ugomvi.
Wanasema hadi tarehe fulani chama kilikuwa na mali hizi, sasa mgogoro ni nini?
Hakuna mahali walisema walikuwa na migogoro au mgogoro wao ulianza lini? Hawajasema chochote.
Dr. Nshala nina miaka 30 nafanya haya masuala ya sheria ndio nimesikia hizi paragraph ni contexual tu. Sasa hakuna kitu kama hicho.
Hoja yetu ni hizi para zao zinazungumzia mambo ya Kikatiba.
Pia nahisi wenzetu hawasikilizi nilisema S. 22(1) ya Political Party Act Msajili anajukumu la kuhakikisha sheria inatekelezwa. Sect. 4 the function and implemention of this Act amepewa Msajili wa Vyama vya siasa.
Dr. Nshala yuko moto sana.
Anaendelea kuwa huwezi kutoa injuction dhidi ya Chama cha siasa kesi ya Lyatonga Mrema imesema hivyo.
Wakati mwingine unaweza kupata ugonjwa wa moyo ukiwa unafanya hizi kazi.
Jaji sasa Dr. Nshala nikushauri jambo
Dr. Nshala samahani Jaji naomba niache.
Jaji sasa sikiliza nataka kukushauri mimi.
Dr.Nshala sawa Nishauri hakuna shida.
Jaji nataka usubmit hapa Mahakamani ukiwa umerelax ili usipate ugonjwa wa moyo.
Dr. Nshala sawa Ahsante nimepokea.
Watu wanacheka.😂
Dr. Nshala anaendelea
Huyu Marijan amesema conditions za Attilio vs Mbowe hazijawa met hata moja kabisa. Hata ku attach ile petition hawajafanya hivyo. Naweza kutumia maneno mazito lakini naomba niseme hili ni jambo la hovyo sana.
Chama cha siasa kinazuiwa kufanya siasa mwaka wa uchaguzi. Naomba Mahakama ya Rufani ilirudie tena uamuzi wake kuhusu Chama cha siasa hakipaswi kuzuiwa.
Naomba pia Mahakama ya Rufani iseme Jambo fulani juu ya huyu Jaji Mwanga maana mambo aliyofanya ni ya hovyo sana. Naomba mtufungulie hata leo tu.
Jaji sasa tunawashukuru sana.
Tunaenda kutafakari na tutawaambieni ni lini tutawapatieni huo uamuzi. Mtajulishwa. Tunawashukuru sana.
Tunaahirisha hadi kikao kijacho.
Mahakama imehairisha mpaka hapo tutakapoitwa tena kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa Majaji.
Naomba repost yako.
Indonesia
Jackson retweetledi

Imeanzishwa media ya kuwakumbuka ndugu zetu waliouwawa Tarehe 29.10.2025.
Media hii itapost kumbukizi zote za uovu WOTE wa Serikali.
Media inatwa @Mo29Tv

Indonesia

@YerickoNyerereT Wewe ndio mpumbavu na mpotoshaji wa kifala kuliko ufala wenyewe
Indonesia

Chadema ni rasmi wameamua kuwa chama cha kutetea Ushoga na Usagaji nchini, Wakati serikali ikipambana kulinda maadili ya jamii kwa kuzuia kila viashiria vya Ushoga nchini.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya chama hicho Ndugu @godblessjlema1 ameamua kujitokeza hadharani na kutetea msimamo wa chama hicho juu ya ushoga na usagaji kufuatia amri ya serikali kupiga marufuku taasisi ya kishoga iliyoingia mkoani Tabora kwa mgongo wa dini.
Chama cha siasa kikifikia hatua ya kutetea ushoga na usagaji mbele ya jamii ya Kitanzania yenye maadili ya kweli, Basi chama hicho kimeamua kujitenga rasmi na umma huo na tukitangaze kama chama adui wa taifa letu…..
Katika hili nimeumizwa sana, kwa miaka mingi chama hicho hakijawahi kuunga mkono mambo ya kishenzi na kidharimu kama hayo, lakini leo Chama kimegeuka kuwa taasisi ya ushoga na usagaji?
Watanzania kataeni kuviunga mkono vyama vya aina hii ya CHADEMA vitaharibu kizazi chetu na vijana wetu, Ungeni mkono vyama vyenye sera nzuri za kimaadili kama vile CHAUMMA. Chaumma tunaupinga ushoga kwa vitendo na kwa maneno na katika hili hatung’ati maneno! Ushoga na usagaji uishie hukohuko!
Nina laani kwa nguvu zote msimamo huu wa Chadema!
Na Yericko Nyerere



Indonesia

@winstone_nnko Kitu nzuri sana iyo hapo utawachukua picha wakiwa kwenye ilo kochi Kisha unawahifadhia wakiwa watu wazima iwe story kwao
Indonesia

@HildaNewton21 Uyu amekwenda kama yule wakwetu tu mpka Leo hatujamuona sio mtu wala maiti ila Mungu ni wawote
Indonesia

HABARI MBAYA
Huyu kijana anayeonekana kwenye hii picha akiwa amewashika Polisi mabega akijaribu kujikongoja anaitwa Emmanuel Bernard Msele,
Mara ya mwisho alionekana katika video hii iliyopostiwa na BBC 29 October majira ya asubuhi maeneo ya ubungo Maji.
Huyu ni kati ya watu Waliokamatwa siku hiyo asubuhi kabisa wakati maandamano yanaanza na kupakiwa kwenye gari hilo la Polisi tangu siku hiyo hajaonekana tena.
November 6, 2025 Mwezi wa 11 familia yake ilipata taarifa kwamba ndugu yao yupo Hospital ya Mzena anatibiwa, walifika hapo na kuambiwa ni kweli alitibiwa hapo lakin baada ya kupata nafuu Polisi walimchukua na kuondoka nae.
Ndugu zake wametafuta vituo vyote vya Polisi bila mafanikio.
#FreeEmanuelMsele

Indonesia
Jackson retweetledi

AFCON na Migogoro ya Uongozi Afrika: Tafsiri ya Sheria Inapochukua Nafasi ya Ukweli Haki na Busara.
Uamuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuinyang’anya Senegal ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 na kuutunuku Morocco utaingia katika historia kama moja ya matukio ya kutatanisha zaidi katika michezo barani Afrika. Si kwa sababu sheria imetekelezwa, bali kwa sababu katika kudai kuitekeleza, CAF imeonekana kubadili ukweli na kuuweka katika kile kinachoweza kuitwa hali ya kisheria iliyobuniwa (legal fiction).
Tuwe wazi kuhusu ukweli. Senegal haikuacha mchezo kwa maana ya kawaida inayotambulika katika soka. Wachezaji wake walitoka uwanjani kwa muda mfupi kupinga uamuzi, walirejea, wakaendelea na mchezo, na wakaukamilisha. Mwamuzi aliruhusu mchezo uendelee hadi mwisho wake wa kawaida. Senegal ilifunga katika muda wa nyongeza na kushinda.
Hata hivyo, CAF sasa inadai kuwa Senegal ilipoteza kwa kuacha mchezo.
Hapa ndipo tatizo linaanzia.
Katika sheria na michezo, dhana fulani zina maana wazi. Kupoteza kwa kuacha mchezo kunamaanisha kuwa mchezo haukukamilika, kwamba upande mmoja ulikataa kuendelea, na hivyo hakuna matokeo ya uwanjani. Lakini katika tukio hili, mchezo ulikamilika. Matokeo yalipatikana. Yalishuhudiwa na mamilioni. Senegal ikashinda uwandani. Ikapongezwa.
Kwa hiyo, uamuzi wa CAF unatutaka tukubali hali mbili zinazokinzana: kwamba Senegal ilicheza na pia haikucheza, ilishinda lakini pia ilipoteza kwa kuondoka. Hii si tafsiri kali tu ya sheria. Ni uundaji wa hadithi ya kisheria, simulizi inayotofautiana na ukweli ulioshuhudiwa ili kuhalalisha uamuzi wa kiutawala.
Hadithi za kisheria zina nafasi yake katika sheria. Lakini zinapotumika kubadili matokeo ya wazi na ya umma, zinahatarisha uhalali wenyewe unaokusudiwa kulindwa.
Ndiyo maana suala hili linazidi mipaka ya soka. Linaakisi moja kwa moja mgogoro mpana wa uongozi Afrika. Na hata wazee limetushangaza na tukalazimika kuweka neno.
Katika taasisi nyingi barani, tunaona mtindo unaojirudia: mamlaka inapopingwa, majibu hayawi ya uwiano bali ya nguvu tena za ziada. Sheria hutumika si tu kurekebisha vijana, bali kuthibitisha mamlaka juu yao. Kukomoa.
Hatua ya muda mfupi ya Senegal kutoka uwanjani, iwe ilikuwa sahihi au la, ilikuwa ni changamoto kwa mamlaka. Jibu la CAF likawa si la kukosoa kwa kutoa adhabu stahiki, bali kufuta matokeo ya mchezo na kuwakomoa vijana. Kwa kufanya hivyo, jibu limevuka mstari kati ya nidhamu na kupitiliza kwa kiburi cha mamlaka.
Uongozi bora haujengwi tu juu ya sheria, bali juu ya busara. Inahitajika taasisi kutofautisha kati ya kurekebisha tabia na kulinda uaminifu. Faini au adhabu zingine zingeweza kudumisha nidhamu bila kubadili matokeo ya mchezo. Badala yake, CAF imechagua hatua kali zaidi.
Matokeo yake ni wazi. Imani inapotea.
Kwa mashabiki wa soka Afrika, swali si tena nani alishinda AFCON. Ni kama matokeo ya uwanjani yanaweza kuaminika tena. Ikiwa yanaweza kubadilishwa baadaye kwa tafsiri za kiutawala, basi uadilifu wa mashindano wenyewe unahojiwa. Unakuwa wa mashaka.
Kwa maana hii, CAF inaweza kuwa imeshinda hoja ya kisheria, lakini imepoteza kitu muhimu zaidi:
Uaminifu na Uhalali wake.
Na uaminifu ukipotea, si rahisi kuurudisha.
Suala hili sasa litapelekwa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS). Lakini bila kujali matokeo, madhara tayari yameonekana. Soka la Afrika haliwezi kustawi katika maamuzi yanayoonekana kuwa ya kiholela au yasiyo na uwiano na busara. Yanayofutwa na watawala wa taasisi kwa kisingizio cha sheria.
Walioshindwa kweli katika tukio hili huenda si Senegal wala Morocco, bali ni AFCON yenyewe. Uhalali wake nahata uadilifu tayari vimetiliwa mashaka na walio wengi. Hata na wazee ambao hatufuatilii michezo kila siku, tukio hili limetugusa. Tukaweka neno.
Itambulike kwamba nguvu ya mashindano yoyote iko si tu katika sheria zake, bali katika imani kwamba sheria hizo zitatumika kwa haki na kwa kuendana na ukweli na busara.

Indonesia

@ayubu_madenge Irani masnich ni wengi kwenye mfumo wao ndio feli inakoanzia
Indonesia

Tunajivunia kuwa seheri ya mawakili wanaopigania mabadiliko ya kisheria na ki katiba ya taifa letu pendwa!
Mwananchi Newspapers@MwananchiNews
Usipitwe na mambo ya msingi‼️ Pakua app ya #MwanaClick kwenye #GooglePlay ama #AppStore, au tembelea mwanaclick.com kupata nakala yako ya kidijitali. Mtandaoni mpaka mtaani, #TunawezeshaTaifa
Indonesia

@AlexSamoja Familia ya castor imeshapita waliobaki ni mapandikizi hapo lazma Cuba iende
Indonesia

@TravellerVoman Hawamu hii nimuendelezo tu chanzo ni yeye sikuwahi kumkubali alale kunakostahili
Indonesia


















