pilipili nyingi limao kwa mbali
231 posts








ONCE A TRAITOR, ALWAYS A TRAITOR. Waliondoka kwa mbwembwe nyingi wakakitukana sana Chama pamoja na Viongozi wetu matusi ya kila aina. Wengine wakaenda mbali zaidi wakaanza kusema #NoReformsNoElection ni uhaini, wakawa wanasema wanashangaa inakuaje Serikali haimkamati Mhe. Lissu wakati anahamasisha UHAINI hata haikuchukua muda Mhe. Lissu akakamatwa na kupewa kesi ya Uwongo mpaka leo ni zaidi ya Mwaka mmoja yupo jela. Walisema CHADEMA imepoteza mwelekeo mara sijui CHADEMA ishajifia bora waende huko wakatimize ndoto zao kisa waliambia watapewa majimbo 20 na Viti maalum 25. Mungu alivofundi walikula kofi la uso wakaangukia pua sasa baada ya kukosa Ubunge kama walivoahidiwa leo wanajifanya wameweka mikono nyuma, wanaomba kurudi kwenye CHAMA as if sio wao waliokua wanatukana mitusi na kudhalilisha Viongozi wetu. Hawa watu sio wakuwachekea maana msaliti ni msaliti, kama waliweza kutusaliti jana unadhan nini ambacho kitamzua kutusaliti leo/kesho..?


Mkandarasi anaendelea na kazi ya kuvunja mawe eneo la Kitonga 🫡 Mitambo iko site





















