
MSHAURI MKUU
878 posts

MSHAURI MKUU
@annamatari995
Upcoming great Industrial Investor,follower of @chaummatz


Sherehe Ndio kwanza inaanzaa








Ili taifa liendelee linahitaji Wanaharakati wa kweli, Lakini aina ya Wanaharakati tulio nao ni hatari kwa mstakabali wa siasa na taifa letu kwa ujumla, kwakuwa wengi ni wafanyabiashara ya harakati na Siku Watanzania wakifanikiwa kuwafahamu wanaharakati wetu hawa hakika tutajitenga nao mbali sana! Haya Wanaharati wenu hao hapo wanapokea mabilioni toka kwa Wazungu kwakutumia kinachoitwa matatizo yetu…. Na wengi wameingiza mabilioni kupitia matatizo ya Chadema (kesi za wanachadema) tena bila chadema yenyewe kushirikishwa. Jiulize kwa mabilioni haya wanayopokea kutokana na migogoro nchini, Wanaharakati hawa watapenda kuwepo na maridhiano ya kisiasa nchini? Hawa nchi ikiwa tulivu maana yake unawakosesha ulaji huu. Najaribu kufikiria zile kelele zao enzi za maridhiano ya Chadema na Serikali zilikuwa na maana kubwa sana kwao. Wakati wa Uchaguzi ndani ya Chadema, kulikuwa na nguvu kubwa ya Wanaharati wengi wao wasio wanachadema wakishinikiza mabadiliko ya uongozi ndani ya Chasema na kukawa na tuhuma kwamba makundi ya Wanaharakati hawa yaliingilia uchaguzi huo kwakutumia Mabilioni hayo ya Wazungu ambayo yaliombwa na wanaharakati hao chini ya Maria Sarungi kupitia Nairobi Kenya wakisema lengo lao ni kusaidia kutoa elimu ya demokrasia na utawala bora nchini kumbe kazi yake ilikuwa kuingilia siasa za vyama na kuchochea migogoro katika vyama vya upinzani. Kwa ripoti hii ya Shrika hili la Ford Foundation sasa naanza kuamini Uchaguzi ule uliingiliwa, na tujiulize hawa Wanaharakati wanapata wapi nguvu za kuendesha harakati hizi katika mataifa ya Afrika Mashariki? Ikumbukwe Mwaka jana 2024 Rais wa Kenya Wiliam Ruto alilishutumu shirika hili la Ford Foundation kwa kufadhili maandamano ya Gen Z. Sasa Wanaharakati wa Kenya wanavuka mpaka na kuja Tanzania wanasema sie tumelala ngoja watuamshe, Binafsi sina tatizo nao kuamshwa ni jambo jema sana, Tatizo langu ni haya malipo ya mabilioni wanayolipwa hawa ndugu zetu yana nia njema kwa Taifa letu? Ingia kwenye tovuti ya shirika hili usome ripoti ya mwaka ikionyesha watu wenu wanavyovuna mabilioni huko…. fordfoundation.org/work/our-grant… Na Yericko Nyerere







Aiseee hii kweli FUNGA KAZI… Mwanza Mna sifa sana 😳






Mgombea Uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Salum Mwalim Juma October 27,2025 amehitimisha kampeni Za kuomba ridhaa kwa wananchi wa Tanzania akiambatana na mgombea mwenza wake Mh.Devota Minja mkutano huo uliofanyika Viwanja vya Tabata Shule,Jimbo la Segerea. Mwalimu amesema kuwa amejipanga kwenda kuongoza nchi bila kuweka visasi kwa viongozi wote waliopo madarakani,Pia Mwalim amesema yupo tayari kuongoza nchi ilikwenda kutatua shida zilizoshindwa kutatuliwa na serikali iliyopo madarakani. #UwakilishiMakini #Chaumma2025





Kuwaambia watu wakiandamana watakufa, wataumia ni kuzidi kuwakosea wananchi!! Kwanini waumie kwanini wafe? Nani atawaua? Maandamano ni haki ya kikatiba, Anayezuia ndio anakiuka katiba!! Anayeua na kuumiza ndio anavunja sheria! Kwanini mnawauzia hofu raia kwa kuwaambia watakufa…..WAKATI BILA MAANDAMANO TU WANAKUFA!! Ukisoma takwimu za idadi ya vifo nchini annually bado ni kubwa sana tu, na vingi hutokea kwa sababu za kukosa huduma,taasisi,idara na utawala bora! Wengi wanakufa kwa kukosa madawa na matibabu hospital na kodi wanalipa! Vifo kutokana na makosa mengi ya jinai Kwa sababu ya ubovu wa mifumo ya haki rushwa na utawala wa sheria!! Vifo vya watu kutekwa, kuuliwa, kupotezwa pasipo kuonekana tena!! TUSIWATISHE WADAI HAKI KWA KUWAAMBIA WATAKUFA AU KUUMIA WAKIANDAMANA, WAKATI WAMEKUWA WAKIUMIA NA KUFA FOR YEARS, BILA HATA KUANDAMANA!!




