APT0⚡️
17.5K posts

APT0⚡️
@apto96
JournalisT&PR0 || Powered By Arrahman|| ArsenaL FaN || MusliM


Welcome to Mbarali Mbarali ni wilaya inayojulikana kama kitovu cha kilimo cha mpunga cha kisasa nchini Tanzania, hasa kutokana na vipengele hivi:


@AllyAssed13070 Ukifikisha miaka 60 hadi 70 hapo utaelewa faida ya kuwa na watoto



Kamati ya Bunge ya Elimu, Sanaa na Michezo, ikiongozwa na Wajumbe wake Wanu Hafidh Ameir na Babu Tale, ilikuwa sehemu ya historia ya ushindi mkubwa wa Dar City dhidi ya Johannesburg Giants katika michuano ya Basketball Africa League (BAL) 2026. Katika mashindano hayo, Dar City imeandika historia kwa kuwa timu ya kwanza na ya pekee kutoka Tanzania kushiriki michuano ya BAL, na imewashangaza wengi baada ya kuibuka na ushindi wa vikapu 100-70 dhidi ya Johannesburg Giants. Ushindi huo mkubwa haukutarajiwa na wengi, hasa kwa timu inayoshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza na iliyopata nafasi kupitia mfumo wa wild card. Baada ya ushindi huo, Tanzania imeendelea kusifiwa kama taifa linalopiga hatua kubwa kwa kasi katika Sekta ya Michezo, kuanzia Soka, Ngumi hadi sasa Mpira wa Kikapu. Dar City wanatarajiwa kurejea tena dimbani leo saa 10:00 jioni kuikabili Nairobi City Thunder, katika mchezo mwingine muhimu wa kuendelea kuthibitisha ubora wao kwenye mashindano hayo. #MillardAyoUPDATES.




















