Sabitlenmiş Tweet
MZALENDO🇹🇿
4.5K posts

MZALENDO🇹🇿
@automatic_head
MZALENDO HALISI/ hard worker// Simba sport club🦁 & real Madrid fans
TANZANIA Katılım Nisan 2024
2K Takip Edilen1.8K Takipçiler
MZALENDO🇹🇿 retweetledi
MZALENDO🇹🇿 retweetledi

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 170
Shahidi wa kificho P6: Akasema tutawanyike na atapanga tarehe nyingine ya mkutano huo.
Wakili: Huyo Makamu Mwenyekiti ni nani?
Shahidi wa kificho P6: Ni Mh. Heche.
Wakili: Tar. 18/04/2025 nini kilitokea?
Shahidi wa kificho P6: Nilipokea taarifa kuwa tarehe 20/04/2025 siku ya pasaka kutakuwa na matembezi ya hiyari ambapo katika matembezi hayo yataambatana na kuvalia tshirt zilizoandikwa agenda ya No Reforms: No Election ili kuendeleza agenda ya Chama.
Wakili: Kingine kilichoendelea?
Shahidi wa kificho P6: Ukafanyika utaratibu wa kuzipata tshrit na tunachangia elfu 10 ndipo zitasafirishwa hadi kutufikia.
Tukaambiwa hadi kufikia tarehe 20 basi tutakutana kwa ajili ya matembezi hayo ya hiari.
Wakili: Tar. 20/04/2025 kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Tulijikusanya kwa ajili ya matembezi ya hiari kila mmoja alipata tisheti yake na tukakubaliana jioni majira ya saa 10 ndio matembezi ya hiari yatafanyika.
Wakili: Ulipata wapi hizo taarifa:
P6: Group la Siasa Yetu.
Wakili: Matembezi mlikubaliana mkutane wapi?
Shahidi wa kificho P6: Songea Mjini kwa Disi Kitimoto na ilipofika majira ya saa 10 huku tukiwa na bodaboda huku tukisubiri wengine. Mimi nilikuwa kwenye muonekano wa kuvaa tshirt iliyoandikwa agenda ya No Reforms: No Election.
Wakili: Nini kilitokea?
Shahidi wa kificho P6: Wakaja Polisi wakajitambulisha kwa ghafla kuwa wanatokea kituo cha Polisi Songea na wakatuambia tunahitajika kituo cha Polisi Songea kwa ajili ya mahojiano.
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P6: Walitukamata na kutupeleka kituo cha Polisi Songea na wakatuhoji kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali.
Wakili: nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P6: Wakasema tutatoka kwa dhamana lakini tulihitajika kwenda kuripoti ofisi ya RCO.
Wakili: Tarehe 25/04 nini kiliendleea?
Shahidi wa kificho P6: Tuliripoti Ofisi ya RCO tumuelezee kilichotokea hadi kufika sehemu hiyo.
Wakili: Mhe. Jaji ndio hayo kwa shahidi huyo.
Watu wanashangaa sasa huyu shahidi sijui alikuwa anazungumza nini na kinasaidia nini kwenye Uhaini ni Maajabu, ngoja Tunasubiri aanze kuulizwa maswali hapa.
Jaji Ndunguru: Vipi mshitakiwa tukupe nafasi ujikusanye vizuri?
Mhe. Lissu: Mh. Jaji huyu shahidi nilishajiandaa nae toka juzi.
Sasa shahidi sijui wewe ni Kaka au Dada lakini naomba ujibu maswali yangu sawa?
Shahidi wa kificho P6: sawa.
Mhe. Lissu: Uliandika maelezo Polisi?
Shahidi wa kificho P6: Sijaelewa swali.
Mhe. Lissu: Kitaeleweka tu. Jibu swali langu Bwana.
Shahidi wa kificho P6: niliandika
Mhe. Lissu: Ukionyeshwa hayo maelezo yako utayatambua?
Shahidi wa kificho P6: ndio.
Mhe. Lissu: Ulisaini?
Shahidi wa kificho P6: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Mh. Jaji naomba aonyeshwe maelezo yake.
Shahidi wa kificho P6: Nimeyapata na ndio maelezo yangu niliyoandika Polisi Songea.
Mhe. Lissu: Je yana sahihi yako?
Shahidi wa kificho P6: sahihi yangu ipo ndio.
Mhe. Lissu: Ni maelezo ya Tar. 25/04/2025.
Shahidi wa kificho P6: Sioni hiyo Tarehe.
Mhe. Lissu: Angalia juu mwanzoni, anamsomea hilo eneo.
Shahidi wa kificho P6: Sijayaona hayo maelezo.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji nataka ku impeach huyu shahidi, nitamsomea maelezo yake, anamsomea hapa.
Mimi ni mkazi wa Bombambili, kazi yangu Bodaboda na kituo changu ni miembeni.
Ilipofika mwaka 2025 nilimfuata Katibu wa Vijana Essau Chiza alinikaribisha kwenye Chama na kunifanyia mpango wa kadi ya Chama.
Nakumbuka tarehe 04/04/2025 niliona mtandao wa youtube hotuba ya Lissu iliyokua inahusu uchaguzi 2025 iliyokuwa ikihamaisha uasi. Ilinipa moyo wa kijasiri wa kutaka kuvuruga uchaguzi.
Nikamtafuta Essau Chiza ambae ni Katibu kunipa mipango mingine ikiwemo ziara ya Mwenyekiti Taifa.
Anaendelea kumsomea maelezo yake yote hapa.
Part 171 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Filipino
MZALENDO🇹🇿 retweetledi

Anaandika Askofu Bagonza
RAIS SAMIA KABADILISHA MWANDISHI WA HOTUBA?!
Nimemsikia Rais Samia Suluhu akiwahutubia mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania. Hotuba yake imepiga hatua moja mbele. Ni kama Rais Samia “ameishavua nguo lakini anaogopa kuoga maji”. Ama maji yana moto sana au ni baridi sana. NAMPONGEZA mwandishi wa hotuba. NAMPONGEZA Rais kwa kuwa mwaminifu wa kusoma kilichoandikwa. Pamoja na pongezi hizo, Rais akipenda azingatie haya:
1. Mabalozi alioongea nayo jana ndio aliwauliza WHO ARE YOU? Bila shaka sasa anajua WHO ARE THEY?. Asirudi nyuma. Kwao na mabalozi ni Mtaa wa MTAKUJA. Tunatibiwa kwao, hawatibiwi kwetu. Umaskini Jeuri uliondoka na Kambarage. Hizi ni enzi za Diplomasia. Balozi Kombo ajipime.
2. Rais amesema “Sauti za Watanzania Zimesikika kupitia Uchaguzi”. Ni asilimia 2 tu zilimkataa Rais wetu. Sasa nauliza, MARIDHIANO na DIALOGUE ni vya nini?
Rais ajue kuna kitu hakiko sawa eneo hili. Hata shetani hafurahishwi na matokeo ya uchaguzi huu. Rais akikubali atakuwa mnufaika wa kwanza.
3. Ili sauti hizo ziweze kusikika ilibidi watu wengine wazuiwe kugombea. Ilibidi vyama vingine vifungiwe kufanya kazi. Ilibidi chama tawala kiende likizo na “vyombo” viongoze badala ya “kuongozwa”. Kama kuna mtu anamsahaulisha Rais wetu ukweli huu, hamtendei haki na analichukia taifa letu.
4. Rais amesema “Tulichofanya tarehe 29 Oktoba kilikuwa muhimu”. Siku hiyo vilitokea vitu viwili vikubwa. Watu waliandamana wakavuruga uchaguzi. Cha pili watu walikufa wengi. Serikali inaogopa kusema wangapi na waliofiwa wanaogopa kusema. Umuhimu wa tulichofanya siku hiyo ni upi?
5. Rais amesema kilichotokea siku hiyo “Watanzania sivyo tulivyo”. Hawa waliofanya ni wa taifa gani? Sasa Dialogue ya nini ikiwa sivyo tulivyo?
6. Rais ametoa pole kwa kukata internet na ameomba radhi. Akaahidi kuwa jambo hilo halitarudiwa tena. VEMA. Lakini kukatika kwa internet kuliruhusu mambo mengine kufanyika. Kuna vifo, kuna vilema, kuna hasara za kiuchumi. Mwandishi wa hotuba awakumbuke hawa safari ijayo. Uhai ni bora kuliko internet.
7. Taifa letu ni kubwa sana. Si rahisi kuliongoza kwa mfumo mmoja usio na ukaguzi (checks and balances). Ikiwa hata rais anaweza kudhibitiwa na mfumo, waliobaki wana nafuu gani? Mabalozi wanajua haiwezekani. Kama rais anataka “Maendeleo Endelevu”, afanye kisichotegemewa na kisichoweza kutamkwa na washauri (Mzee Mpango na Rafiki yangu Majaliwa). Extra ordinariness is needed because we messed extra ordinarily!
8. Watu wanaotetea HAKI hawako huru mitaani. Ama wako kaburini, Safe House, Nje ya nchi au Mahabusu. Namshauri Rais afanye “uasi”. Afungulie walio mahabusu na Safe House. Arudishe walio ukimbizini (Mabalozi wanawajua kwa kuwa ndio wamewapa ukimbizi). Waliokufa watajwe tumalize matanga. Rais atashangaa atakavyokubalika hata kama hatakuwa salama. Mlinzi wa kweli wa Rais ni wananchi. Kwa sasa wananchi WAMENUNA. Zingatia.
9. Mh. Rais ajue: Hatua zilizochukuliwa Oktoba 29, kuna watu hawaonekani. Ni jukumu lake kutoa hesabu. Namsihi akubali kuna kitu HAKIKWENDA SAWA. Awajue, awape pole, nao awaahidi kuwa haitatokea tena. Familia zionyeshwe walipo au walikotupwa. Taifa litapona na Rais atapona. Taifa gonjwa haliwezi kuwa na Rais mzima. Kama hajui, basi sasa ajue kuwa ANAUMWA kwa sababu Taifa linaumwa.
10. Ugonjwa wa Taifa unaongezwa na watendaji wanaomdanganya Rais. Kundi la pili ni la machawa. Makundi haya 2 yanaharibu jitihada za rais kuliponyesha taifa. Eti Mheshimiwa Rais, ili kukukosoa wewe inabidi mtu awe tayari kukaa jela miezi 6? Wewe ni malaika? Serikali yako ni sawa na Mungu? Usitafute mchawi.
Wajaluo sijawasahau: Ninaandaa shindano la Mjaluo mweupe wa mwaka 2026. Mshindi atazawadiwa Kamongo mwekundu.

Indonesia
MZALENDO🇹🇿 retweetledi
MZALENDO🇹🇿 retweetledi
MZALENDO🇹🇿 retweetledi

Nimesoma MJADALA wa Mwakinyo kuhusu Tshirt yake binafsi nishaandika maoni yangu jana usiku na leo asubuhi.
Mimi nimempongeza kwa alichofanya na msimamo wangu utabaki hivyo. Na msingi wa MSIMAMO WANGU ni katika hizi nyakati za GIZA kufanya alichofanya japo hata kwa kidogo mimi naamini ni KIKUBWA SANA KWENYE SAFARI YA KUPIGANIA HAKI.
Ndiomaana kuna msemo tunasema “Asante Mungu hata kwa hiki KIDOGO, tumeambiwa tushukuru kwa kila jambo maana tukishindwa kushukuru kwa kidogo hata kikubwa tutashindwa kushukuru”.
Watu wangapi maarufu hata KUTAJA JINA “TUNDU LISSU” hawajawahi na kuogopa WAKOLONI WEUSI watawafikia.
Watu wangapi hata kuenda mahakamani kwenye kesi ya Lissu wanaogopa kwa kuogopa WAKOLONI WEUSI watawafikia.
Wote mashahidi kesi ya LISSU kila mtu nchi nzima alikuwa anafuatilia, wengine wakaishia kuandika kwa mafumbo kuonyesha kumkubali LISSU, ila Mwakinyo alisema hadharani na kumpongeza bila kuogopa WAKOLONI WEUSI WATAMFIKIA.
Mimi maoni yangu yapo vile vile kwa alichofanya jana kuweka picha ya Tundu Lissu kwenye Flana yake nyuma ni ushindi MKUBWA kwa wapigania haki—hata kwa hicho kidogo sisi tunashukuru maana wapo wengi wanaogopa na wameshindwa ila yeye kaweza kufanya kwa udogo ule na ukubwa ule ASANTE CHAMPEZI.
NB: HATA UFANYE NINI CHINI YA JUA BINADAMU WATAONGEA—HIYO NDIO ASILI YETU.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎

Indonesia
MZALENDO🇹🇿 retweetledi

‼️🔥TUMESHINDA‼️
Kama Taifa tumelipa gharama kubwa ila TUMESHINDA - tumeushinda udhalimu wa miongo mitano ya CCM
Ule moshi wa Mwenge tuliyosema ni uchawi wa kutuloga umeshindwa na kulegea!
Kilichobaki ni CCM kupambana mitandaoni kufanya spinning ili tusimalize kazi ndogo iliyobaki! Na kutumia trauma ya mauaji ya Oktoba kutuahidi mauaji zaidi - jambo ambalo hawawezi TENA!
Ewe mtanzania! Usiseme Tutashinda, sema TUMESHINDA na tujipige kifua kwa ushindi!
Mungu ametufikisha pakubwa tutoe shukrani na tumalize kazi ndogo iliyobaki! Hakuna kurudi nyuma wala kukwama!
Tanzanians have finally broken the CCM grip on power as the party and its leaders grapple with a new vibrant citizenry that no longer buys in to the false narrative of “peace and stability” and instead demand Justice, Accountability and Truth!
This has come with a huge price tag of #TanzaniaMassacre by Suluhu and her murderous cabal but we only have the last stretch to complete the transformation of this great nation ✊🏽
#Tumeshinda🇹🇿 #WenyeNchiWananchi #SamiaMustGo #J1

Filipino

RT @mangekimambi: @SuluhuSamia umefanya propaganda wiki nzima kuwahadaa Watanzania kuwa Marekani inakusapoti mtu ambae umeua wananchi ili u…
Indonesia
MZALENDO🇹🇿 retweetledi

MZALENDO🇹🇿 retweetledi

FAMILIA YANGU,
Kiongozi leo muda wa saa 11 Usiku polisi wamevamia nyumbani kwangu Baada ya kunikosa wamepiga watoto na kukamata Familia yangu yote,
Waliokamatwa
1.kelin Benedictor Jafety mwanafunzi wa kidato cha pili Mtoto.
2.Eliud Thobias Moyi mwanafunzi wa chuo cha vita umeme Mtoto
3.Elias Sebastian Maya mwanafunzi darasa pp2 mtoto miaka 5
4.Asteria Sebastian mtoto miaka 3
5.Mama grand wifi yamgu
6.Mama Vijinia wifi jirani
7.Thabiza binti wa kazi
8.Siwema Jakobo Mdogo wangu
Kiiufupi wamekamata familia yore iliyokuwepo nyumbani na wamewapiga ili waseme mama yao yuko wapi
Neema Steven Chozaile
Mwenyeki chadema Jimbo la geita Vijijini
9/12/2025

Indonesia
MZALENDO🇹🇿 retweetledi
MZALENDO🇹🇿 retweetledi
MZALENDO🇹🇿 retweetledi

TUPATE COMMENTS ZA KUTOSHA KUWAONYESHA WAKOLONI WEUSI #Disemba9Tunatoka #D9
REPOST 500
#MD9
#Disemba9Tunatoka
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎

Filipino
MZALENDO🇹🇿 retweetledi

Read - and watch - our full Tanzania investigation edition.cnn.com/2025/11/21/afr…
English
MZALENDO🇹🇿 retweetledi
MZALENDO🇹🇿 retweetledi

Wakili Barnabas Nyalusi na Mjumbe wa Baraza la Uongozi @TanganyikaLaw amekamatwa leo asbh Mkoa iringa ni miongoni mwa mawakili wanaowatetea wenye kesi za uhaini mpaka sasa tuhuma hazijawekwa wazi.

Indonesia
MZALENDO🇹🇿 retweetledi

Tanzania Nchi yetu.
Nchi iliyopendwa na kuwa kumbilio la wote walioteswa Duniani, Nchi iliyotoa hifadhi kwa wapigania Uhuru na haki Duniani.
Nchi iliyomficha Mandela asiuwawe na Makaburu, ikatoa hifadhi kwa wapigania uhuru wa Afrika kusini, Angola, Zimbabwe.. Nchi iliyompa baba wa demokrasia ya Kenya Raila Odinga Paspoti ya kusafiria awe salama kukimbia Utawala wa mabavu.
Leo tumegeuka kichekesho cha Dunia, viongozi wabovu wasiochaguliwa wanaharibu na kuondoa sifa nzuri Mwalimu aliyoijengea Nchi yetu.. tena wanafanya haya kwasababu binafsi na mambo yao..
Tumeingia kwenye trend ya Nchi za kidkteta, zisizoaminika na zinaongelewa vibaya kila sehemu..
Hatutakubali watu wachache waharibu na kuchafua taswira ya Nchi yetu kwasababu na maslahi yao binafsi.
Filipino











