
Evance Fredrick
1.3K posts

Evance Fredrick
@evance_fredrick
Businessman /Veterinarian/ Preacher/Human right officer


VIDEO: Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam imeagiza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukabidhi nyaraka muhimu za kiofisi kwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar Said Issa Mohamed na wenzake wawili, nyaraka zitakazowasadia kwenye marejeo ya hoja mbalimbali kufuatia kesi ya madai inayohusu CHADEMA kuitenga Zanzibar iliyofunguliwa Mahakamani hapo Uamuzi huo umetolewa leo, Jumatatu Septemba 29.2025 na Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza kesi hiyo ya madai namba 8323/2025 iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed na wenzake wawili, ambapo nyaraka zinazopaswa kuwasilishwa na CHADEMA ndani ya siku 14 ni pamoja na tamko la mali za chama, taarifa za fedha za Benki ya NBC (NBC Bank statements) na taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za chama hicho, zote ni kuanzia mwaka 2019 hadi 2024 Akifafanua kuhusu uamuzi huo mbele ya wanahabari, Wakili Hekima Mwasipu amesema sambamba na chama hicho kupewa siku 14 za kuwasilisha nyaraka hizo, waleta maombi wamepewa siku tisa (9) za kazi za kupitia nyaraka, na kisha Mahakama itaendelea na kesi hiyo Oktoba 30.2025.











Kuna moto special kwa mtu aliyeanzisha ACT wazalendo 🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻😂😂😂😂😂


























