Global Impact Transformation

291 posts

Global Impact Transformation banner
Global Impact Transformation

Global Impact Transformation

@globalimpactt

Founder @marthanghambi | Driving equity, resilience & innovation | Empowering communities through tech and inclusive development

Dar es Salaam, Tanzania Katılım Ocak 2025
36 Takip Edilen302 Takipçiler
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
GIT tunawekeza kimkakati katika kuwajengea vijana ujuzi wa uongozi wa kibiashara ili kuwawezesha kuwa wabunifu wa ajira, wachochezi wa ukuaji wa uchumi, na viongozi wa mabadiliko endelevu. Kupitia Midahalo ya Vijana, tunaunda jukwaa shirikishi linalowaunganisha vijana na maarifa, mitandao, na fursa halisi. Mwaka 2026, tunapanua wigo kwa kufikia makundi mbalimbali ya vijana na kuwaunganisha kidijitali kwenye majukwaa yatakayotoa madarasa huru, yakiruhusu ujifunzaji unaofikika popote na wakati wowote. Kwa kushirikiana na wadau na wafadhili, dhamira ya GIT ni kuwezesha vijana kupata jukwaa huru la fursa likiwaunganisha moja kwa moja na uwekezaji, ajira binafsi, na teknolojia za kisasa ili kuharakisha safari yao kuelekea kujitegemea na mchango chanya katika maendeleo ya jamii. #GITImpact #Youth #Tanzania #Africa
Global Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet media
Indonesia
0
0
1
9
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
𝐉𝐚𝐧𝐚 𝐢𝐥𝐢𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐬𝐢𝐤𝐮 𝐲𝐚 𝐤𝐢𝐩𝐞𝐤𝐞𝐞 𝐧𝐚 𝐲𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐦𝐚𝐟𝐚𝐧𝐢𝐤𝐢𝐨 𝐦𝐚𝐤𝐮𝐛𝐰𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐒𝐨𝐤𝐚 𝐥𝐚 𝐖𝐚𝐧𝐚𝐰𝐚𝐤𝐞 𝐌𝐤𝐨𝐚 𝐰𝐚 𝐃𝐚𝐫 𝐞𝐬 𝐒𝐚𝐥𝐚𝐚𝐦. Global Impact Transformation (GIT) tulijivunia kuwa sehemu ya wadhamini wa Fainali ya Ligi ya Wanawake, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wetu, Bi. Sylivia Mkomwa, alipata heshima ya kushuhudia fainali hizo sambamba na viongozi wa Soka la Wanawake @Ireneishengoma Pongezi za dhati kwa uongozi wa soka la wanawake Mkoa wa Dar es Salaam kwa uendeshaji wa Mashindano haya na timu ya 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐭𝐞 𝐏𝐫𝐢𝐧𝐜𝐞𝐬𝐬 𝐤𝐮𝐭𝐰𝐚𝐚 𝐔𝐛𝐢𝐧𝐠𝐰𝐚 𝐰𝐚 𝐋𝐢𝐠𝐢 𝐲𝐚 𝐖𝐚𝐧𝐚𝐰𝐚𝐤𝐞 𝐌𝐤𝐨𝐚 𝐰𝐚 𝐃𝐚𝐫 𝐞𝐬 𝐒𝐚𝐥𝐚𝐚𝐦. Pia, Pongezi kwa 𝐌𝐛𝐚𝐠𝐚𝐥𝐚 𝐐𝐮𝐞𝐞𝐧𝐬 kwa kushika nafasi ya pili, na 𝐑𝐚𝐧𝐠𝐢 𝟑 𝐏𝐫𝐢𝐧𝐜𝐞𝐬𝐬 kwa kushika nafasi ya tatu. Tunazipongeza timu zote tatu kwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kwa Wanawake (WRCL 2026). GIT tunaendelea kuonesha dhamira ya dhati katika kusapoti michezo, hususan kwa wanawake, kwa kuhakikisha wanapata elimu ya kujitambua, kujiamini, na kupambana na ukatili wa kijinsia ndani na nje ya uwanja wa michezo. Pamoja, tunaijenga jamii salama, yenye usawa, na inayothamini vipaji vya wanawake. 💪🌍 #GITImpact #TokomezaUkatili #SokaLaWanawake #Tanzania
Global Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet media
Indonesia
0
1
2
14
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
We are proud to partner with Babawatoto Organization to implement the 𝐓𝐮𝐥𝐢𝐧𝐝𝐚𝐧𝐞 (𝐋𝐞𝐭’𝐬 𝐏𝐫𝐨𝐭𝐞𝐜𝐭 𝐄𝐚𝐜𝐡 𝐎𝐭𝐡𝐞𝐫). A grassroots initiative in 𝐊𝐢𝐛𝐨𝐧𝐝𝐨, 𝐊𝐢𝐠𝐨𝐦𝐚, strengthening community-led advocacy and social and behavior change to address gender inequality, prevent gender-based violence, (GBV) and enhancing climate resilience. This initiative is elevating local leadership and advancing sustainable, community-driven solutions. 𝐓𝐨𝐠𝐞𝐭𝐡𝐞𝐫, 𝐰𝐞 𝐚𝐫𝐞 𝐬𝐭𝐫𝐞𝐧𝐠𝐭𝐡𝐞𝐧𝐢𝐧𝐠 𝐜𝐨𝐦𝐦𝐮𝐧𝐢𝐭𝐲 𝐨𝐰𝐧𝐞𝐫𝐬𝐡𝐢𝐩, 𝐝𝐞𝐞𝐩𝐞𝐧𝐢𝐧𝐠 𝐝𝐢𝐚𝐥𝐨𝐠𝐮𝐞, 𝐚𝐧𝐝 𝐚𝐝𝐯𝐚𝐧𝐜𝐢𝐧𝐠 𝐢𝐧𝐜𝐥𝐮𝐬𝐢𝐯𝐞, 𝐫𝐞𝐬𝐢𝐥𝐢𝐞𝐧𝐭 𝐬𝐨𝐜𝐢𝐞𝐭𝐢𝐞𝐬. #GITImpact #TulindaneProject #Tanzania #Africa
Global Impact Transformation tweet media
English
0
1
2
24
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
𝐏𝐫𝐚𝐜𝐭𝐢𝐜𝐚𝐥 𝐬𝐤𝐢𝐥𝐥𝐬 𝐚𝐫𝐞 𝐭𝐡𝐞 𝐟𝐨𝐮𝐧𝐝𝐚𝐭𝐢𝐨𝐧 𝐟𝐨𝐫 𝐛𝐮𝐢𝐥𝐝𝐢𝐧𝐠 𝐚 𝐠𝐞𝐧𝐞𝐫𝐚𝐭𝐢𝐨𝐧 𝐭𝐡𝐚𝐭 𝐢𝐬 𝐞𝐜𝐨𝐧𝐨𝐦𝐢𝐜𝐚𝐥𝐥𝐲 𝐬𝐞𝐥𝐟-𝐫𝐞𝐥𝐢𝐚𝐧𝐭. Through the partnership between Global Impact Transformation (GIT) and Her Initiative under the MSHIKO Clubs 2026 program, we continue to empower students with essential knowledge and practical skills that strengthen their educational, social, and economic capacity while they are still in school. As part of the continued implementation of this program, through a beneficiary of 𝐆𝐈𝐓 𝐂𝐡𝐚𝐦𝐩𝐢𝐨𝐧𝐬, 𝐀𝐧𝐧𝐚 𝐌𝐰𝐚𝐢𝐬𝐚𝐤𝐚, successfully delivered training on liquid soap making to students at 𝗦𝗮𝗿𝗮𝗻𝗴𝗮 𝗦𝗲𝗰𝗼𝗻𝗱𝗮𝗿𝘆 𝗦𝗰𝗵𝗼𝗼𝗹. This training has played an important role in equipping students with income-generating skills, helping them identify opportunities within their communities, and appreciate the value of practical knowledge as a tool for economic empowerment. As the Technical Partner of this initiative, GIT remains committed to reaching more students with diverse skills-building opportunities that will enable them to shape a better future, unlock their potential, and become part of a generation driving sustainable solutions in their communities.
Global Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet media
English
0
2
4
32
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Mkurugenzi Mtendaji wa @globalimpactt Bi. @sylvia_mkomwa akiwa nchini Ethiopia, Addis Ababa, kushiriki katika 𝐌𝐤𝐮𝐭𝐚𝐧𝐨 𝐰𝐚 𝐕𝐢𝐨𝐧𝐠𝐨𝐳𝐢 𝐕𝐢𝐣𝐚𝐧𝐚 𝐧𝐚 𝐌𝐚𝐚𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐨 𝐀𝐟𝐫𝐢𝐤𝐚 (AYLDC) 2026, ameendelea kuiwakilisha Tanzania 🇹🇿 katika majukwaa ya kimataifa yanayochochea maendeleo endelevu. Katika mwendelezo wa mkutano huo, amefanikiwa kufanya mazungumzo na 𝐁𝐚𝐥𝐨𝐳𝐢 𝐰𝐚 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 𝐧𝐜𝐡𝐢𝐧𝐢 𝐄𝐭𝐡𝐢𝐨𝐩𝐢𝐚 𝐧𝐚 𝐌𝐰𝐚𝐤𝐢𝐥𝐢𝐬𝐡𝐢 𝐰𝐚 𝐊𝐮𝐝𝐮𝐦𝐮 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐔𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐰𝐚 𝐀𝐟𝐫𝐢𝐤𝐚 (𝐀𝐔), 𝐌𝐡𝐞. 𝐈𝐧𝐧𝐨𝐜𝐞𝐧𝐭 𝐒𝐡𝐢𝐨, ambapo walijadiliana na kutoa mrejesho kuhusu maendeleo ya mkutano huo pamoja na mchango wake katika kuimarisha ushiriki wa vijana katika ajenda za maendeleo barani Afrika. Mazungumzo hayo yameonesha umuhimu wa ushirikiano wa kimkakati kati ya taasisi, serikali na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha kuwa sauti na suluhisho za vijana zinapewa nafasi katika ngazi za juu za maamuzi. Kupitia ushiriki huu, GIT inaendelea kuthibitisha nafasi yake kama mdau muhimu katika kuendesha ajenda za maendeleo kimataifa, hususan barani Afrika, kwa kuunganisha wadau, kukuza ubunifu wa vijana, na kusukuma mbele utekelezaji wa suluhisho zenye matokeo chanya na endelevu kwa jamii. #GITImpact #AYLDC2026 #Tanzania #Africa
Global Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet media
Indonesia
0
2
4
79
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Kama sehemu ya dhamira yetu endelevu ya kuwawezesha wanawake na vijana nchini Tanzania, @global_impact_transformation inajivunia kushirikiana kwa karibu na 𝐌𝐚𝐚𝐟𝐢𝐬𝐚 𝐌𝐚𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐨 𝐲𝐚 𝐉𝐚𝐦𝐢𝐢 pamoja na Benki ya @crdbbankplc katika Mkoa wa 𝐌𝐭𝐰𝐚𝐫𝐚, ili kuimarisha na kusaidia vikundi vya wanawake kupitia fursa jumuishi za kiuchumi. Ushirikiano huu unaakisi dira yetu ya pamoja ya kujenga jamii imara kwa kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha, kujenga uwezo, pamoja na kuendeleza shughuli za kujipatia kipato kwa njia endelevu. GIT itaendelea kushirikiana kwa karibu na washirika wa maendeleo ili kupanua wigo wa msaada huu kuvifikia vikundi vingi zaidi kwa kutoa suluhisho bunifu katika maeneo ya 𝐮𝐣𝐚𝐬𝐢𝐫𝐢𝐚𝐦𝐚𝐥𝐢, 𝐭𝐞𝐤𝐧𝐨𝐥𝐨𝐣𝐢𝐚, 𝐧𝐚 𝐮𝐨𝐧𝐠𝐨𝐳𝐢 kwa manufaa ya muda mrefu. #GITImpact #Wanawake #Vijana #Tanzania #Africa
Global Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet media
Indonesia
0
2
3
20
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
GIT inatambua umuhimu wa jitihada za pamoja katika kulinda na kuhifadhi mazingira yetu. Kupitia mshikamano na ushirikiano wa wadau mbalimbali, tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli na endelevu. Kuelekea tarehe 28 Machi, 2026, wadau wote wa mazingira tunakutana Mbali Beach – Mbezi Beach kwa ajili ya zoezi la usafi na bonanza la wanamazingira. Usipange kukosa. Uwepo wako ni sehemu ya mabadiliko tunayoyahitaji. 🌱🌊 #GITImpact #BeachCleanUp #Partinership #Tanzania
Global Impact Transformation tweet media
Indonesia
0
2
2
46
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Kushirikisha jamii katika midahalo ya Ujenzi wa Amani ni msingi muhimu wa kujenga na kudumisha amani endelevu. Midahalo hii huwezesha makundi mbalimbali kama vijana na wanawake kushiriki kikamilifu katika kujadili changamoto na kubuni suluhisho za pamoja. GIT inaendelea kuimarisha jitihada hizi katika mikoa ya pembezoni mwa mipaka ya nchi, kwa kuwezesha jamii kujenga uelewa, kuhimiza mazungumzo ya amani, na kuimarisha mshikamano kwa maendeleo ya taifa. #GITImpact #Amani #Tanzania #Africa
Global Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet media
Indonesia
0
1
2
20
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Utekelezaji wa 𝐌𝐚𝐥𝐞𝐧𝐠𝐨 𝐲𝐚 𝐌𝐚𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐨 𝐄𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐯𝐮 (𝐒𝐃𝐆𝐬) ni nguzo imara na njia sahihi ya kufikia mafanikio ya kweli katika jamii zetu. Kupitia juhudi hizi, tunajenga msingi wa ustawi, usawa, na maendeleo jumuishi kwa vizazi vya sasa na vijavyo. @global_impact_transformation inaendelea kusukuma ajenda hii kwa kuwafikia makundi mbalimbali ya jamii. Mfano hai ni kikundi cha kina mama cha TUPAMBANE Women’s Group kilichopo Mtwara, ambacho kinajihusisha na utengenezaji wa nishati safi ya mkaa mbadala pamoja na biashara ndogo ndogo wakitekeleza kwa vitendo 𝐒𝐃𝐆 𝟏 (𝐊𝐮𝐭𝐨𝐤𝐨𝐦𝐞𝐳𝐚 𝐔𝐦𝐚𝐬𝐤𝐢𝐧𝐢), 𝐒𝐃𝐆 𝟕 (𝐍𝐢𝐬𝐡𝐚𝐭𝐢 𝐒𝐚𝐟𝐢 𝐧𝐚 𝐍𝐚𝐟𝐮𝐮), 𝐧𝐚 𝐒𝐃𝐆 𝟏𝟑 (𝐇𝐚𝐭𝐮𝐚 𝐳𝐚 𝐊𝐮𝐤𝐚𝐛𝐢𝐥𝐢𝐚𝐧𝐚 𝐧𝐚 𝐌𝐚𝐛𝐚𝐝𝐢𝐥𝐢𝐤𝐨 𝐲𝐚 𝐓𝐚𝐛𝐢𝐚𝐧𝐜𝐡𝐢). Kama GIT, tunaamini kuwa uwekezaji kwa jamii ni uwekezaji kwa mustakabali bora. Tunaendelea kushirikiana, kuwezesha, na kuhamasisha ili kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma katika safari ya maendeleo endelevu. #GITImpact #Women #NishatiSafi #Tanzania #Africa
Global Impact Transformation tweet media
Indonesia
0
2
3
44
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Our Executive Director @MkomwaSylvia @globalimpactt had the honor of attending the Her Impact Gala yesterday as a special guest hosted by @ahda_africa The evening was a powerful celebration recognizing inspiring young female leaders selected through a nomination process, alongside distinguished senior women leaders and supportive male allies. As we continue to commemorate International Women’s Day, we remain committed to championing women’s leadership, amplifying voices, and creating opportunities for the next generation of changemakers. We extend our appreciation to the organizers for creating such a meaningful platform to celebrate impact, leadership, and collaboration. Together, we continue to build a future where women and girls thrive. #HerImpactGala #InternationalWomensDay #GITImpact #Tanzania
Global Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet media
English
0
1
2
20
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Jiunge nasi tarehe 14 Machi 2026 katika Fukwe za Mbezi Beach – Kwa Zena, Dar es Salaam kwa ajili ya zoezi maalum la usafi wa fukwe, tukilenga kulinda mazingira ya bahari na kuhamasisha uwajibikaji wa pamoja kwa jamii yetu. 🌊♻️ Tukio hili litaleta pamoja wadau wa mazingira, taasisi binafsi, vyombo vya habari pamoja na wananchi, katika kushiriki shughuli mbalimbali zitakazofanyika siku hiyo, ikiwemo: 1.Zoezi la pamoja la Usafi 2.Uhamasishaji na uhifadhi wa Mazingira ya Bahari 3.Bonanza la Michezo lenye kuhamasisha masuala ya utunzaji wa Mazingira pamoja na ugawaji wa zawadi 4.Uzinduzi wa kipindi cha Mazingira Mubashara yatakayofanyika moja kwa moja kutokea eneo la tukio. 5.Burudani nyingine nyingi Unaanzaje kukosa? Muda wako ni sasa jiunge nasi tuifanye Fukwe zetu kuwa safi na salama kwa kizazi cha sasa na kijacho. Kauli mbiu: “Fukwe Safi, Bahari Salama, Jamii Imara.” #GlobalImpactTransformation #GITImpact #BeachCleanup #Tanzania
Global Impact Transformation tweet media
Indonesia
0
2
3
32
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Yesterday, our Founder @MarthaNghambi participated in the 𝐂𝐨𝐧𝐯𝐞𝐫𝐬𝐚𝐭𝐢𝐨𝐧 𝐂𝐢𝐫𝐜𝐥𝐞 𝐨𝐧 𝐄𝐧𝐬𝐮𝐫𝐢𝐧𝐠 𝐚𝐧𝐝 𝐒𝐭𝐫𝐞𝐧𝐠𝐭𝐡𝐞𝐧𝐢𝐧𝐠 𝐀𝐜𝐜𝐞𝐬𝐬 𝐭𝐨 𝐉𝐮𝐬𝐭𝐢𝐜𝐞 𝐟𝐨𝐫 𝐀𝐥𝐥 #Women and #Girls held at the International Labour Organization Office (ILO) during the 70th Session of the Commission on the Status of Women (CSW70) in New York. The dialogue convened practitioners and advocates committed to advancing inclusive, accountable, and gender-responsive justice systems that uphold the rights, dignity, and protection of women and girls. Conversations like these are critical in strengthening global collaboration to address structural barriers that continue to limit access to justice for many women and girls, particularly those in marginalized and underserved communities. At Global Impact Transformation, we remain committed to advancing initiatives that strengthen justice, equality, and protection for women and girls, while amplifying the voices of communities working toward inclusive and resilient societies. #CSW70 #GITImpact #AccessToJustice
Global Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet media
English
1
4
5
44
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Are you passionate about advancing gender equality and strengthening communities? Global Impact Transformation is seeking a 𝐆𝐞𝐧𝐝𝐞𝐫 𝐚𝐧𝐝 𝐂𝐨𝐦𝐦𝐮𝐧𝐢𝐭𝐲 𝐃𝐞𝐯𝐞𝐥𝐨𝐩𝐦𝐞𝐧𝐭 𝐎𝐟𝐟𝐢𝐜𝐞𝐫 based in Kibondo, Kigoma to support community led initiatives that promote women’s empowerment, youth engagement, and inclusive local development. 📍 Location: Kibondo Kigoma (𝑨𝒑𝒑𝒍𝒊𝒄𝒂𝒏𝒕𝒔 𝒎𝒖𝒔𝒕 𝒃𝒆 𝒃𝒂𝒔𝒆𝒅 𝒊𝒏 𝑲𝒊𝒃𝒐𝒏𝒅𝒐) 📩 Send your CV to: career@globalimpacttransformation.org ⏰ Deadline: 15th March 2026 𝑬𝒎𝒑𝒐𝒘𝒆𝒓𝒊𝒏𝒈 𝑪𝒐𝒎𝒎𝒖𝒏𝒊𝒕𝒊𝒆𝒔 𝑻𝒓𝒂𝒏𝒔𝒇𝒐𝒓𝒎𝒊𝒏𝒈 𝑳𝒊𝒗𝒆𝒔.
Global Impact Transformation tweet media
English
0
2
1
42
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Mwezi huu wa Wanawake, tunajivunia kusherehekea nguvu, uthabiti, na mchango mkubwa wa wanawake katika Mikoa ya Mtwara, Tanga, Bagamoyo na Dar es Salaam. Kupitia programu za uwezeshaji za GIT, wanawake hawa wanabadilisha maisha yao na kuleta mabadiliko chanya katika jamii wakiongoza, wakibuni, na kuhamasisha kizazi kijacho. Ujasiri na mchango wenu ni msingi wa maendeleo endelevu. Tunawaona, Tunawasherehekea na Tunasimama nanyi. #GITImpact #WomensEmpowerment #Women #Tanzania
Global Impact Transformation tweet media
Filipino
0
1
1
48
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Afisa Programu wetu, @anisa_biagio alitembelea Taasisi ya Ustawi wa Jamii na kukutana na Serikali ya Wanafunzi @iswoso_official katika kuendeleza ajenda ya uwezeshaji wa vijana na wanawake. Katika kikao hicho, Serikali ya Wanafunzi walitambulisha rasmi wazo lao la #UstawiLadiesGala jukwaa maalum linalolenga kutambua na kusherehekea vijana wanawake wanaoleta mchango mkubwa katika uongozi, ujasiriamali, maendeleo ya jamii na nyanja nyingine mbalimbali. GIT tunaendelea kuunga mkono na kushirikiana na vijana katika kuibua na kuendeleza mawazo yenye tija kwa jamii. Tunaamini katika kukuza vipaji, kutambua ubora, na kuwawezesha wanawake vijana kuwa vinara wa mabadiliko. #GITImpact #WanawakeKatikaUongozi #ULAGA #Tanzania
Global Impact Transformation tweet media
Indonesia
0
3
3
130
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Jamii zetu zina nguvu ya kuleta mabadiliko ya kweli. Kupitia usafi wa fukwe na urejeshaji wa maeneo yaliyoathiriwa na taka za plastiki, tunalinda uhai wa viumbe wa baharini, tunatunza afya zetu, na tunarejesha hadhi ya mazingira yetu. Kila kipande cha plastiki kinachoondolewa ni hatua moja mbele kuelekea mwambao safi na salama kwa kizazi cha sasa na kijacho. Mwaka huu, GIT tunaenda kuzindua mfululizo wa shughuli shirikishi zitakazowaunganisha vijana, wanawake, na viongozi wa jamii kuchukua hatua kwa vitendo dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi. Huu ni wito kwa kila mmoja wetu kushiriki, kwa sababu mazingira ni jukumu letu sote, na mabadiliko yanaanza na wewe. #GITImpact #BahariYetuWajibuWetu #Youth #Women #Tanzania
Global Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet media
Filipino
0
2
2
51
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Yesterday, our Board Chair, Mama Shamim Khan, also Chair of JUWAKITA, held a strategic and impactful meeting with the International Religious Peace Academy (IRPA) from #SouthKorea, promoting interfaith dialogue and collaboration. We look forward to translating this dialogue into tangible actions and sustained, long-term collaboration.
Global Impact Transformation tweet media
English
0
1
1
20
Global Impact Transformation
Global Impact Transformation@globalimpactt·
Tarehe 19/02/2026, mjadala mpana na wa kuvutia umefanyika katika Mnada wa Kishapu, ukilenga kuibua na kujadili kwa kina masuala ya ukatili wa kijinsia unaoendelea kuathiri jamii. GIt tunatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na timu iliyopo mkoani katika kuratibu na kuendesha kampeni hii. Majadiliano haya yanaendelea kufungua nafasi salama ya wananchi kushiriki uzoefu wao, kujifunza, na kuhamasishana kuchukua hatua dhidi ya ukatili wa kijinsia. GIT tunaunga mkono kikamilifu jitihada hizi na tunaendelea kusapoti kwa karibu utekelezaji wa kampeni hii kwa lengo la kujenga jamii salama, yenye usawa na inayolinda haki za kila mmoja. Cc: @wildaftz #GITImpact #EndGBV #Community #Tanzania #Africa
Global Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet mediaGlobal Impact Transformation tweet media
Indonesia
0
2
2
53