.
5.7K posts


Sio kila mtu anakuambia ukweli kuhusu Forex…Hii Podcast imenifungu sana Akili.📉
Kama uko kwenye grind ya kutafuta pesa online, hii ni lazima uione 👇
youtu.be/ID3RvR1qJ2A?si…

YouTube

Filipino

@INFLUENCERjr @Adventure_36 Halafu hii heading ya jinsi alivopata 1.7B. Mbona ye alieleza vzur kua sio kwamba zote zilikua zake Bali 1.7B ni mzunguko wa pesa. Unaweza kua na transaction hyo lakin cash balance ikawa 200M au pungufu.
Indonesia

@INFLUENCERjr @Adventure_36 Mimi ctak kuamini kua alianguka sabab ya marafiki . Kuna kitu anaficha ndio maana hakuweka sabab za kwann marafik walikua central. Yote kwa yote tupo vzuri kwenye kumvutia msikilizaji na hakika wengi wanaweza kuwekeza tena kwake wasipokua makini
Indonesia

TAARIFA RASMI KWA WAWEKEZAJI
Ndugu wawekezaji, Natumaini mko salama.
Ninaandika ujumbe huu kwa unyenyekevu mkubwa na uwazi, nikitambua kuwa kwa muda mrefu nimekuwa kimya kuhusu hali halisi ya uwekezaji uliokuwa chini ya usimamizi wangu. Kimya hiki hakikuwa sahihi, na ninawajibika kikamilifu kwa hilo.
Katika kipindi cha shughuli zangu za forex trading na investment management, kulikuwa na upotevu mkubwa wa mtaji uliokuwa chini ya usimamizi wangu. Jumla ya upotevu huu unafikia takribani dola za Kimarekani 750,000 (USD 750,000). Hasara hii ilitokana mambo binafsi ambayo nimeeleza hivi karibuni kwenye podcast.
Ninakiri wazi kuwa kama msimamizi wa fedha hizo, jukumu hili lilikuwa langu, na ninachukua uwajibikaji kamili bila kumlaumu mtu mwingine yeyote.
Kwa kipindi cha takribani miaka sita iliyopita, nilichagua kukaa kimya nikijaribu kutafuta njia ya kurejesha fedha hizi kwa kuoperate private. Hata hivyo, nimegundua kuwa njia hiyo haikuwa sahihi, na uwazi ndio hatua muhimu ya kwanza ya kurekebisha hali hii.
MPANGO WA MBELE!
Ninafanya kazi na mshauri wa kisheria ili kuweka utaratibu rasmi wa kushughulikia deni hili kwa njia ya kisheria na inayolinda maslahi ya pande zote. Lengo ni kuendeleza mpango wa ulipaji wa deni (repayment plan) ndani ya muda maalum (legal proposed kipindi cha hadi miezi 48), ambao utawezesha kurejesha fedha kwa utaratibu unaoeleweka na unaofuatiliwa.
Sambamba na hilo, nitaanza rasmi shughuli za wazi zinazolenga kuzalisha mapato kwa njia halali na endelevu, ikiwa ni pamoja na:
- Mafunzo (training & mentorship)
- Matukio ya kielimu (paid events)
- Huduma nyingine za kibiashara zilizo wazi na zisizo na usimamizi wa fedha za watu moja kwa moja!
Muhimu kufahamu kuwa kwa sasa sitapokea tena fedha za uwekezaji (investment funds) kutoka kwa mtu yeyote.
HATUA INAYOFUATA
Ndani ya muda mfupi ujao, nitawasiliana na kila mmoja wenu moja kwa moja ili:
- Kuthibitisha kiasi husika
- Kujadili mfumo wa ulipaji kadri ya ushauri wa kisheria.
- Kuweka makubaliano rasmi ya kisheria
Ninaelewa kuwa hali hii imeathiri imani, na sina matarajio ya kurejesha imani hiyo kwa maneno pekee, bali kwa vitendo vitakavyoonekana kadri muda unavyoenda.
Naomba uvumilivu wenu wakati nikiweka mfumo sahihi wa kushughulikia suala hili kwa haki na uwazi.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Fransisco G.C (fransiscomagnetics@icloud.com)
Indonesia

@JohnieZeBest @AmourGingi Ukichart na mtu ukaweka lock, inajificha hata Jina lake kwa contact halionekani na hata akikutext hakuna wala taarifa ya kwamba amekutext. Ni had ukumbuke kwamba ulimlock
Indonesia

Unataka kusema James Temba alikuwa amelewa akakatwa kichwa na mvua?
MK47TA@MK47TA
Aisee pole sana kwa familia yake, kiukweli hiki kipindi cha mvua tunapaswa tuwe na tahadhari sana hususani kwa ndugu zetu wenye matatizo ya afya ya akili bila hivyo itatugharimu sana. Hata unywaji pia tupunguze kwa tahadhari za kiusalama hali za mvua hizi kimazingira hayako sawa
Indonesia

@PresenterNoah @Fefe_doll Kwa sababu yeye ndie msanii wa nyakati zote hadi dunia itakapokwisha
Indonesia

Mahakama ya Shanzu, Mombasa nchini Kenya imepanga Juni 17, 2026 kuanza kusikiliza rasmi Kesi ya Ubakaji inayomkabili Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva, Sefu Shaban maarufu kama Matonya.
Hatua hiyo imekuja baada ya kesi hiyo kutajwa leo na kuahirishwa hadi Juni 3, 2026 kwa ajili ya kutajwa tena, baada ya kukamilishwa kwa baadhi ya stakabadhi muhimu kutoka pande zote mbili ambapo hatua za awali za Kisheria zinaendelea kabla ya kuanza kwa usikilizwaji rasmi wa shauri hilo.
Matonya alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Aprili 9, 2026, akikabiliwa na shtaka la ubakaji linalodaiwa kutokea Aprili 7, 2026 katika eneo la Josy Joka Apartments, Kaunti ndogo ya Nyali ambapo anadaiwa kumuingilia kimwili Mwanamke aliyetajwa kwa herufi J.G bila ridhaa yake.
Mbali na shtaka hilo kuu, msanii huyo pia anakabiliwa na shtaka mbadala la kushika sehemu za siri za mtu mzima bila ridhaa ambapo Mahakama ilimpa dhamana ya Shilingi 500,000 za Kenya (takribani Shilingi milioni 10 za Tanzania), kwa sharti la kuwa na mdhamini mmoja Raia wa Kenya mwenye uwezo huo huo.
Aidha, Passport yake imeamriwa kubaki Mahakamani, huku mamlaka za uhamiaji zikipewa taarifa ili kumzuia kusafiri bila kibali ambapo Upande wa mashtaka uliomba kuwekwa kwa masharti magumu zaidi ya dhamana, ikiwemo kuzuiwa kusafiri nje ya nchi bila kibali maalum, wakati upande wa utetezi uliomba masharti nafuu, ukisisitiza kuwa mshtakiwa yuko tayari kushirikiana na Mahakama.
#MzawaUPDATES

Indonesia

Msanii wa Bongo Fleva, Seif Shaban maarufu kama Matonya, leo Aprili 29, ameachiwa kwa dhamana kufuatia kesi ya ubakaji inayomkabili ikimkabili nchini Kenya, baada ya Mahakama kuridhia dhamana hiyo ambapo ataendelea kuwa huru huku kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa.
Kupitia chapisho aliloweka kwenye mtandao wake wa Instagram, Matonya amesema:
“Kwanza nimshukuru Mungu, leo nimepata nafasi ya dhamana na kuwa nje nikiwa katika Mahakama ya Kenya. Pia niwashukuru Watanzania wote kwa dua na maombi yao, pamoja na ndugu zangu Wakenya kwa kuniombea. Naishukuru familia yangu kwa kupambana hadi hapa tulipofika, pamoja na wadau wote tuliokuwa tunafanya nao kazi.”
Aidha, Matonya amesema hatakuwa tayari kulizungumzia suala hilo kwa sasa kwa kuwa liko Mahakamani ambapo ameongeza kuwa waliotekeleza jambo hilo wanajua walichokuwa wanakifanya na malengo yao.
#MillardAyoUPDATES
Indonesia

@millardayo Line imeenda mala pesa ikaonekana inatoka . How itoke kwenye laini mpya ilihal ya kwake wameenda nayo
Filipino

Mwanamke mmoja Mjane Mkazi wa Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora, Fatma Nassoro, ametapeliwa zaidi ya Shilingi milioni 40 na Watu wanaodaiwa kujifanya watoa huduma ya ‘lipa namba’, fedha ambazo ni sehemu ya mirathi aliyoachiwa na marehemu Mume wake.
Tukio hilo limetokea baada ya Watuhumiwa hao kufika katika eneo la biashara la Mwanamke huyo wakidai kumsaidia kuunganisha huduma ya malipo ya kielektroniki, ndipo walipofanikiwa kupata namba yake ya siri na hatimaye kuhamisha fedha hizo kutoka kwenye akaunti yake.
Aidha, Jeshi la Polisi Mkoani Tabora limethibitisha kuwakamata Watu watano kuhusiana na tukio hilo, ambapo Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, SACP Richard Abwao, amesema Watuhumiwa hao wamekamatwa Babati Mkoani Manyara walipokuwa wakijaribu kutoroka baada ya kufanya uhalifu huo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha Watuhumiwa hao wanarejesha fedha hizo haraka iwezekanavyo kwa Mwanamke waliyemtapeli fedha zake za mirathi na sheria ichukuliwe kwa dhidi yao ili iwe fundisho kwa wenye tabia kama hiyo. #MillardAyoUPDATES
Indonesia

@MarekaMalili Na kabla ya kukimbilia mwanza , akiwa amepanga nyumba kijitonyama dar , alipaa case ya kudhurum hyo nyumba . pia akiwa stand za mabas mnazi mmoja , alidhurumu pesa mkurgenz wa Nyatco transport- Dar Lusaka miaka ya 2002 akaambiwa achague kulipa au kama mji
Indonesia

@mfinanga_rm Wamesema hawahusiki....vijana inaonekana waliuana wenyewe.
Hatuna serikali sisi.....basi tu
Indonesia

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limewakamata Watu 37 kwa tuhuma za makosa ya kimtandao ikiwemo kutoa vitisho na kutumia lugha chafu mtandaoni, hatua ambayo imeelezwa kuwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usalama wa kidijitali katika Jiji la Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aprili 27, 2026, Watuhumiwa hao wamekamatwa Aprili 20, 2026 katika eneo la Ubungo kufuatia operesheni maalum iliyotegemea taarifa kutoka kwa Wananchi na Wadau wa usalama, ambapo baadhi yao wamebainika kuwa Wafanyakazi wa Kampuni zinazotoa huduma za mikopo kwa njia ya mtandao.
Aidha, baadhi ya Watuhumiwa waliotajwa ni pamoja na Renatus Mujwahuzi maarufu Migeyo Mkazi wa Mbezi Beach, Odilia Oswin maarufu Ngunga Mkazi wa Goba Njia Nne pamoja na Theresia Brastius maarufu Kanu Mkazi wa Mtoni Kijichi huku wengine 34 wakiendelea kushikiliwa na kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Pamoja na hayo, Polisi Kanda Maalum Dar es salaam wamesema wanaendelea na hatua za kisheria dhidi ya Watuhumiwa hao, huku wakisisitiza dhamira yao ya kudhibiti vitendo vya kihalifu mtandaoni vinavyoathiri ustawi wa Jamii na usalama wa raia, na kutoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa taarifa za vitendo vya kihalifu ili viweze kufanyiwa kazi kwa haraka na wahusika kufikishwa Mahakamani kwa mujibu wa sheria zilizopo Nchini. #MillardAyoUPDATES

Indonesia



















