#OnThisDay in 2⃣0⃣1⃣9⃣ we visited Tanzania to face Simba SC in a friendly 🇹🇿
An unforgettable experience sharing football and friendship with our Tanzanian friends ❤️🤍
Kuna hii kauli huwa inatolewa sana humu " EPL huwezi kupewa space kama hiyo hata kidogo "
Nafikiria hii clip ingekuwa ya ligi nyingine na sio EPL narrative yake sijui ingekuwaje na hiyo space anapata M. Fernandes 😀😀
Good players mara nyingi wanajua kutafuta spaces na kupata time uwanjani bila kujali ligi gani
@George_Ambangil@ThomasThom74127 lakini wao psg & barca wanasaidia na team ilivojengwa kuanzia wanavo press na wana defend as a unit sie ni kama kuna kuwaga na space kubwa balaa
@ThomasThom74127 PSG nani ni namba 6 ? Au Barca ? 😀ukipata all actions midfielder ni bora sana kuliko specialist ( sio mbaya pia ukipata specialits namba 6 ila wapo wachache sana ambao wazuri )
Iraola kafanya kazi yake , sasa kocha mwingine yoyote mzuri akifanikiwa kumpata Alex Scott , na akaendeleza pale alipoishia Iraola .... Mama Mia 🙌🏻🙌🏻.!
All phase midfielder
Nina changaoto ya Sikio linauma mpaka kwenye taya za meno nazo zinauma, natumia dawa ile ya Maji naweka asubuhi na usiku ila bado haijasaidia 🥹
Kuna dawa nyingine ambayo inaweza saidia msaada 🙏🏻
Sababu ya ukatili wa Samia Suluhu, Tundu Lissu hajahudhuria hospitali mwaka mzima kwaajili ya check-up anazofanya kila baada ya miezi mitatu. Tunajua lengo ni kumdhoofisha kiafya na/au kukusudia kumuuwa. Endeleeni. Haitakuwa business as usual I promise!
@LifeofSteph_1@BrownGudluck@BesteNicolas Hauwezi kuona 68k utaona game za premier league zote ila uefa inabidi 118k compact plus game kubwa wanaweka 222 ambayo ipo compact plus
Biashar ya banda umiza ina hela san imagine game moja buku Watu 200 wakilipa bukubuk una laki 2 na hio ni mechi moja tu.jumamosi kunakuwaga na mechi 3 hadi 4 hapo unapiga kama laki 8 hivi jumapili pia mechi kiba
Kwa mwezi hukosi milion 4 hadi 5 dstv unalipia elfu 60 Azam 30k tu✍️
I really loved how the whole team went over to encourage Thiago Pitarch after that mistake he made. Thins will give him much confidence going forward.
He had a very great game against man city. x.com/baller_1908/st…
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 211
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross examination Shahidi wa kificho P9
Mhe. Lissu: Waambie majaji kama tutafanya vurugu na kuuvuruga uchaguzi huo kama yapo kwenye maelezo yako…nasubiri jibu shahidi!
Shahidi wa kificho P9: Hayapo
Mhe. Lissu: Uliendelea kusema, alisema lazima tukichafue, kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : kweli.
Mhe. Lissu: hayo maneno yapo au hapo.
Shahidi wa kificho P9 : sasa mbona unarudia maswali. hayapo.
Mhe. Lissu: Twende kwa yaliyotokea 22 April 2025, ulisema siku hiyo ulipigiwa simu na polisi kwenda Kituo cha Polisi Mwanjelwa.
Shahidi wa kificho P9 : Kweli
Mhe. Lissu: Sasa soma pale palipoanzia na leo Tarehe 22 April 2025 mpaka nitakapokwambia basi…
Shahidi wa kificho P9 Anasoma…
Mhe. Lissu: Kwenye hiyo sehemu kuna sehemu kumeandikwa kituo cha polisi Mwanjelwa.?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli haijaandikwa
Mhe. Lissu: Na ukasema ulipofika walisema wanataka kukuhoji tena kwa matukio yaliyokuleta hapa.
Shahidi wa kificho P9: Kweli.
Mhe.Lissu : Waambie kama hayo maneno yapo kwa tukio lililokuleta hapa.
Shahidi wa kificho P9 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako jana, ulisema nilihojiwa na mtu mmoja na mwingine alichangia kwa kuniuliza maswali mbalimbali, waeleze majaji kama hayo maneno yapo katika maelezo yako?
Shahidi wa kificho P9 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Niliona clip ya Tundu Lissu ndio nikaanza, waeleze hayo maneno kama yapo katika maelezo yako.
Shahidi wa kificho P9 : hayapo.
Mhe. Lissu: Sijamalizana na wewe, nataka ukitoka hapa ukawaeleze Mapolisi kwamba kule hakufai!
Watu wanacheka: 😂😂😂😁
Mhe. Lissu: Ulisema mimi kama mwananchama wa CHADEMA nilishawishika na kwamba nitafanya uasi, hayo maneno yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P9: Yapo.
Mhe. Lissu: Sasa nataka uwaambie majaji kwamba wewe ni Mwanachama wa CHADEMA au sio?
Shahidi wa kificho P9 : Mimi sio mwanachama wa CHADEMA.
Mhe. Lissu: Kwenye maelezo yako na ushahidi wako wa jana, ulisema mwaka 2024 ulivutiwa na sera na kuamua kuwa mwanachama wa CHADEMA, kweli au sio kweli?
Shahidi wa kificho P9 :Kweli.
Mhe. Lissu: waambie majaji wafuasi wa CHADEMA huwa wanaandikishwa wapi.
Shahidi wa kificho P9: sifahamu.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama wafuasi huwa wanatambulishwa wapi.
Shahidi wa kificho P9: Sijui
Mhe. Lissu: Waeleze kama huwa wanaalama usoni?
Shahidi wa kificho P9: Hapana
Mhe. Lissu: Na ulisema baada ya kuwa mfuasi ulishiriki katika matembezi ya amani, kweli au sio kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli
Mhe. Lissu: Waambie waheshimiwa kama ulijiandikisha sehemu yoyote?
Shahidi wa kificho P9 : Hapana
Mhe. Lissu: Sasa shahidi hukuwahi kujiandikisha popote, huna alama yoyote kuwa ni mfuasi wa CHADEMA, waeleze majaji wataamini vipi kwamba wewe ni mfuasi wa CHADEMA?
Shahidi wa kificho P9 : Mimi sijui hilo ni suala la amani.
Mhe. Lissu: Unasema tulihamasishwa kushiriki kongamano la vijana lililopangwa kufanyika Mbeya, waambie kama uliwahi kupewa mualiko wowote hata wa simu?
Shahidi wa kificho P9 ; hapana sikupewa mualiko wowote.
Mhe. Lissu: kama kiongozi wa chama aliwahi kukufata ili kukupa taarifa ya kongamano.
Shahidi wa kificho P9 : hawakunifata.
Mhe. Lissu: Kama hawakukufata inamaana hawakujui.
Shahidi wa kificho P9 : Sio lazima wanijue wote.
Mhe. Lissu: Kwa maelezo yako ya ushahidi ya jana, umesema ulisoma VETA Mbeya kati ya 2008-2010 ulipohitimu, kweli au sio kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama umewasilisha cheti cha kuhitimu?
Shahidi wa kificho P9 : sijawasilisha kwasababu hakina umuhimu.
Mhe. Lissu: wataaminije? Kwasababu maneno matupu hayavunji mfupa.
Mhe. Lissu: Umesajiliwa kama fundi umeme wa majumbani na viwandani.
Shahidi wa kificho P9 : Ndio nimesjiliwa.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama umeleta hati ya kusajiliwa?
Shahidi wa kificho P9: Hapana.
Part 212 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 210
Anaendelea Mhe. Lissu na Cross Examination.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji naomba shahidi apewe kielelezo D13
Mhe Lissu: Jana kwenye ushahidi wako uliulizwa unaishi wapi na ukasema unaishi katika Halmashauri ya Mbeya, kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli.
Mhe. Lissu: Naomba uangalie maelezo yako, nenda palipo andikwa makazi usome pameandikwa makazi yako wapi?
Shahidi wa kificho P9: Pameandiwa Mwakibete.
Mhe. Lissu: Kwenye mstari wa kwanza kabisa sema palivoandikwa hapo? Kwamba unaishi?
Shahidi wa kificho P9 : Pameandikwa Mwakibete lakin nilihojiwa Mbeya.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kwamba haya maeneo huwa yanatangazwa kwenye gazeti la serikali na waziri wa TAMISEMI
Shahidi wa kificho P9 : sifahamu
Mhe. Lissu: Umeonyesha gazeti la Serikali linaloonyesha Mwakibete ni Mbeya,?
Shahidi wa kificho P9; Hapana.
Mhe. Lissu: unafikri unaandika andika tu unaingizwa chaka na mapolisi na wewe unaandika tu.
Mhe. Lissu: Uliulizwa unafanya shughuli gani na ulisema unafanya kazi ya fundi umeme na kazi zako unafanya katika Halmashauri ya Mbeya, kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli
Mhe. Lissu: Angalia maelezo yako unafanya kazi gani?
Shahidi wa kificho P9 : Mkulima
Mhe. Lissu: Kazi ni mkulima hapa unajifanya fundi umeme, lugha gongana.
Watu wanacheka: 😂😂😂😂
Mhe. Lissu: nyie Waha wa kigoma wajanja sana nyie na mimi napenda watu wajanja kama wewe.
Mhe. Lissu: Uliulizwa unakumbuka kitu gani kilikukuta 2024, ukasema nilivutiwa na sera za CHADEMA na nikawanafatilia matangazo, mikutano n.k haya sasa soma maelezo yako mjanja wa Jiji la Mbeya…😁
Mhe. Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji hayo maelezo uliyosoma hapo kama yapo na ulivyosema jana
Shahidi wa kificho P9 : Hayapo
Mhe. Lissu : Uliandika kwa mapolisi wakakupuuza wakaandika ya kwao.
Mhe. Lissu: Katika matukio mengi uliyofatilia ulitaja matembezi ya yaliyoongozwa na Lissu yalianzia Uyole, na Heche Isanga, mwambie jaji kama Mhe. Heche yupo katika maelezo kayo
Shahidi wa kificho P9: Nilieleza ni Mnyika sio Heche.
Mhe. Lissu: Jana ulisema Heche alianzia Isanga, unataka niwasumbue majaji wakusomee ulichokisema??
Shahidi wa kificho P9: inawezekana nilikosea
Mhe. Lissu: Kazi yangu ni kukamata watu waongo kama wewe.
Shahidi wa kificho P9 : Hiyo unasema ww
Mhe. Lissu: ndio nasema.
Mhe. Lissu: Ulisema mnamo tarehe 3 April 2025 ukiwa nyumbani kwako wakati unaperuzi mitandao kupitia simu yako aina ya Samsung 8 pro, kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : kweli
Mhe. Lissu: Angalia maelezo yako waeleze majaji kama kuna mahala popote ulikua unaangalia mitandao kupitia aina ya Samsung 8 pro.
Shahidi wa kificho P9: hayajaandikwa.
Mhe. Lissu: Asante, mmeuzwa na mapolisi.
Mhe. Lissu: Ulisema kwamba uliingia kwenye mtandao wa instagram na ili uweze kuimgia instagram lazima uwe na simu janja, account na bundle, hayo maneno yapo au hayapo.
Shahidi wa kificho P9 : hayapo.
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako jana ulisema wakati unaingia kwenye instagram uliona video ya Tundu lissu na ukasema huo mtandao umeusahau.
Shahidi wa kificho P9 : Ndio nimeusahau.
Mhe. Lissu: Kama umesahau inamaana, kwenye maelezo yako utakua umeandika.
Shahidi wa kificho P9: Sasa wewe unaniuliza mambo waliyoniuliza mawakili.
Mhe. Lissu: Jibu swali langu. Unanifundisha namna ya kukuhoji?
Shahidi wa kificho P9 : Ndio hakuna
Mhe. Lissu: Uliulizwa muonekano wa Tundu Lissu, ukasema alikua ukumbini alivaa kombati za kaki za chadema na tshirt nyeusi na bendera ya taifa na rangi za CHADEMA, kweli si kwei?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli
Mhe. Lissu: Sasa waeleze waheshimiwa majaji kama yapo katika maelezo yako.
Shahidi wa kificho P9 : Hakuna
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako jana uliulizwa alisema atauzuiaje ukasema tutafanya vurugu na kuuvuruga uchaguzi huo.
Shahidi wa kificho P9: Kweli
Part 211 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.