Edwin F.M@EdwinMjeru
“Social comparison” ni changamoto yetu kubwa hasa vijana katika zama hizi za mitandao.
>Inatengeneza presha ya ndani ya kutaka vitokee papo kwa papo bila kuipa muda na mchakato nafasi.
>Inatia wengi presha ya kufanya vitu kwa kujaribu ‘ku-fit in’ na siyo kufanya kwa sababu za msingi.
>Inadunisha uwezo kwa baadhi ya watu kwa kujihisi tu wao siyo bora au hawana uwezo kama akina fulani.
>Ni chanzo mojawapo cha matatizo ya afya akili, kwani husababisha msongi wa mawazo kwa kujihisi umechelewa, una gundu, au hauwezi ku-make.
Na madhara mengine kede kede.
Muhimu: Acha kujilinganisha na watu wengine katika namna hasi. Hata ufanikiwe kiasi gani, hata upate pesa au mali kiasi gani siku zote kuna mtu atakuwa juu yako, na kukuzidi.
Kwa hiyo, tembea kwa spidi yako, na kwenye mwelekeo na barabara yako.
Kikubwa una MALENGO na ‘You are making a progress’.
Keep going.
EFM.