James Mbowe
2K posts


Nichukue nafasi hii kipekee kuwapongeza @airtanzania kwa namna wanavyo badili ratiba za ndege mara kwa mara. Mfano leo ndege ya Air Tanzania iliyokuwa iruke kwenda Kigoma saa 5:40 imesogezwa mpaka saa 9:30 sababu wanasema ni Operation yaani siyo hata kwamba hali ya hewa ni mbaya au ndege mbovu bali ni sababu za Uendeshaji. Yaani mnaacha Abiria wanatoka majumbani usiku wanawahi Airport alafu kwa Urahisi kabisa bila Aibu mnatangaza ni sababu za kiuendeshaji. Kwa kweli kutoka Moyoni niwapongeze sana hii inaonyesha ni kwa jinsi gani Shirika letu linavyowajali wateja wake. Kuna mtu aliwahi kuniambia Kirefu cha ATC ni Anytime Cancelation, sasa nimeanza kumwelewa.


Indonesia

Shirika la umeme @Tanescoyetuna wananchi wa Tunduma wamewakosea nini mbona swala la kukatwa kwa umeme huku limekuwa extremely? Au usikute hawa wanahesabika kama wazambia! Hebu fikiria uchumi bila Nishati ya uhakika, mnachochea sana watu watafute bar zenye Generator wachaji simu wakati wanachaji simu na wenyewe wanatumia muda huo huo kujichaji 😭😭
Indonesia

Rais wa Baraza la Maaskofu nchini, Askofu Wolfgang Pisa O.F.M. Cap, amekanusha vikali taarifa iliyotolewa na jeshi la Polisi kwamba Katibu Mkuu wa Baraza hilo Fr.Dr.Charles Kitima (PhD) alikua anapata kinywaji kabla ya kushambuliwa.
"Hakuna baa katika eneo aliloshambuliwa Fr.Kitima na hivyo hakuwa anapata kinywaji kama inavyoelezwa. Pale ni mgahawani. Kusema mtu alikua anakunywa saa zote hizo si kweli. Tunaandaa taarifa kamili, tutaitia itakapokua tayari" Amesema Askofu Pisa.

Indonesia

Mambo haya yataendelea mpaka lini? Who is next? Kwanini uonevu huu ni kwa Viongozi wa Chadema tu? Au Chadema siyo watanzania? Hivi mtu kama @hechejohn akiitwa Polisi atakaidi kuja? Utaratibu uliotumika kumkamata Tundulisu naona ndio huo huo umetumika kumkamata Heche, ingawa Lisu mlimwacha akamaliza mkutano safari hii Makamu amekamatwa hata kabla ya kuhutubia. Mambo haya yanatia hasira sana. Free Tundulisu Free Heche. Kiwango cha chuki kinachojengwa kwenye Mioyo ya watu ni kikubwa sana.
Indonesia


























