-Yanga kabla hawajamdai Oruma Bilioni 10 kwa kuwachafua wamemtaka awaombe radhi pamoja na Efm na TVE kushusha post zote zinazoonekana matamshi yake yaliidharirisha Yanga.
Ningekuwa mimi Oruma ningewaomba radhi hadharani kabisa...Tena ningerekodi video clip ya kuwaomba radhi na kuipandisha Mtandaoni
Kwanini...?
1)Yanga wanaweza kushindwa kesi ya Morrison ila kesi ya hivi hawashindwi nakuambia...wote tunajua!
2) Kwenye hii Nchi linapokuja suala la Simba na Yanga hata wakili wako anaweza kukusaliti akaacha kutokea Mahakamani ukaishia jela!
3) Tuhuma za Kuihusisha Yanga na rushwa/upangaji wa Matokeo haijaanzia kwa Oruma, Mamlaka inajua lakini wa kuthibitisha hayupo...Suala la kipa wa Tabora United liliishaje?
4) Kuomba radhi hata bando la jero haliishi...Aombe radhi...Yanga ni wakubwa sana kwenye hii Nchi...Hawezi kutoboa japo kila mtu anajua alichosema Oruma ndio ukweli wenyewe!
Nafunga hizi Story siziongelei tena ✍️
@jeju_julius Kuna watu wanaingiza drinks fake i mean drinks zilizotengenezwa viwanda bubu na watu wanatumia
Pia utumiaje mbovu wa soft drinks, pombe na energy drinks
Kuna baadhi ya madogo mkisikia wamepotea msiwatufute wa kwanza huyu..nawahakikishia asipoomba msamaha ndani ya masaa 24 kitachomkuta asilalamike kumtafuta mwanasheria kama haamini subirini.
Mdau anasema klabu ya yanga iachane kabisa na Wilson Oruma, jambo hili linaweza kupelekea kufika Fifa na kuanza kufukua makaburi.
Mdau anasema ukosoaji wa matokeo katika michezo ni jambo la kawaida, anaenda mbali zaidi na kusema namna michezo ambayo klabu ya yanga inalalamikiwa ni mingi, amegusia mchezo wa yanga dhidi ya Singida baadhi ya wachezaji kuto kucheza na hata wa mbeya City nao kutokucheza.
Ameenda mbali zaidi kugusia sakata lililomwondoa Patrick Osems ndani ya Singida black Star's akisisitiza huo ni mtego,🙄
Anasema jambo hili linaweza kupelekea kufichuliwa kwa mambo mengi zaidi ikiwemo la kudhamini vilabu, jambo ambalo linaweza kupelekea Fifa kuanza uchunguzi na kupelekea hatari mbaya 🙌🙌
Amemnukuu Wilson Oruma mwenyewe kuwa anaushahidi, manake amejipanga kwa lolote, na vile vile amegusia kauli ya kocha aliyefukuzwa mbeya city Mecky Maxime jambo linaloongeza utata.
🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄
“Kama Viongozi wanataka kuwapeleka wachambuzi mahakamani nadhani na sisi wachambuzi tujiandae kuwafungulia mashtaka ya Upangaji wa matokeo,Betting nk.
Hakuna aliyesalama sana kwenye mpira Wetu Kama vipi funikeni kombe mwanaharamu apite.
Tena sasa hivi Ndio balaa,tunajuana guys.”
- Juma Ayo, Mtangazaji na Mchambuzi wa CrownFM.
#MeaMswahiliUPDATES
“Kwenye hili jambo nabaki kusema ukweli kwamba Singida hawana malengo yoyote kwenye ligi yetu zaidi ya kutaka kuinufaisha Yanga tu”
🗣️Wilson Oruma
Wilson kavaa mabomu anachimba ukweli, lakini ameshasema Ushahidi anao hivyo mnaopinga mje na hoja za msingi.
@RevocatusMagum1 Jamaa anachoongea kina ukwel ndani yake
1. Angalia mechi za azam zote
2. Anglia mechi za simba zote
3. Anglia mechi za yanga zote
Kuna utofauti ukubwa sana vijana wanaojielewa saiv hawafatilii hizo hizo mechi hakuna radha ya mpira halisi.
🚨Haya ni maneno ya mchambuzi Wilson Oruma
“Nina ushahidi mwingi kwenye mechi za Yanga lakini naamua kunyamanza kimya na kwa namna hii tunayoenda nayo Mamlaka zisipokua makini mpira wetu unaenda kuangamizwa moja kwa moja”
🗣️ Wilson Oruma
Hivi mtu anapata wapi ujasiri wa kuongea kitu kama hicho?
Je? inawezekana ni kweli Yanga wananunua mechi hawezi kuongea tu bure✍️
@RevocatusMagum1 Bodi ya ligi na TFF wanatakiwa kullichukulia hili jambo seriously, then lipelekwe Takukuru, hizi ni tuhuma ambazo zimesemwa zina ushahidi, Takukuru na jeshi la polisi haliwezi kuanzia kuchukua hatua kuanzia hapa?
Mabroo wote mnao tusisitiza tuoe mabikra shikamooni🙌🏽
Mabroo wote mnao tuonya zidi ya hawa madem ma-degree holder shikamooni🙌🏽
Leo nimetambua mabroo mnatupenda 😁😁🙌🏽
🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄 || Mshambuliaji kijana wa Kitanzania, Selemani Mwalimu Abdala (20), anatarajiwa kuondoka ndani ya kikosi cha Simba SC mwishoni mwa msimu huu baada ya muda wake wa mkopo kufika tamati. Kwa mujibu wa takwimu kutoka mtandao wa Transfermarkt, Mwalimu alijiunga na Wekundu wa Msimbazi kwa mkopo wa mwaka mmoja mnamo Agosti 23, 2025, akitokea klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco. Mkataba wake wa mkopo unatarajiwa kuisha rasmi Juni 30, 2026, ambapo mchezaji huyo atalazimika kurejea nchini Morocco kuitumikia klabu yake mama ambayo bado ana mkataba nayo wa muda mrefu hadi mwaka 2029.
Katika kipindi chake akiwa na Simba, Mwalimu ametoa mchango wake hususan katika michuano ya kimataifa ambapo amecheza jumla ya michezo saba ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) na kufanikiwa kufunga mabao mawili. Licha ya umri wake mdogo, mshambuliaji huyo wa zamani wa Fountain Gate ameweza kuonyesha uwezo wake wa kupambana uwanjani, jambo lililomfanya kuwa mmoja wa wachezaji tegemeo katika safu ya ushambulizi. Kuondoka kwake ni pigo kwa Simba inayojipanga kwa msimu ujao, huku mashabiki wakisubiri kuona kama uongozi utafanya jitihada za kumwongezea mkopo au kumsajili jumla kufuatia kiwango alichokionyesha.