Mr David
11.3K posts


@DavidDruv @Mwanahalisitz @ACTwazalendo @zittokabwe Ni kweli mie mtoto maana kipindi nameplate mama ako ww ulikuwa bado hujazaliwa
Filipino
Mr David retweetledi

Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo @ACTwazalendo Zitto Kabwe @zittokabwe amesema kuwa mfanyabiashara Harbinder Singh Sethi amemfungulia kesi kwa tuhuma za kumkashifu kupitia sakata la IPTL maarufu kama sakata la ESCROW kupitia maandiko yake kwenye mitandao ya kijamii.
“kesi nimefunguliwa na mtu anayeitwa Bwana Habinda Sin Seth kuwa nimemkashifu na kumshushia heshima mbele ya jamii kwa vile eti nimezungumzia sakata la IPTL mbali na mambo mengine nimlipe mabilioni.” amesema Zitto.
Indonesia
Mr David retweetledi

Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo na mtaalamu wa uchumi, Zitto Kabwe, ametoa onyo kali kwa watu wote- ndani na nje ya Serikali wanaojihusisha au kupanga kumsaidia mfanyabiashara Harbinder Seth katika madai yanayohusiana na fedha za umma zilizotokana na sakata la IPTL na Akaunti ya Tegeta Escrow.
Akizungumza na wanahabari siku ya Jumapili Mei 18, 2025 mkoani Dar es Salaam, Zitto amesema, “Yeyote serikalini, yeyote yule au nje ya serikali, ambaye kwa namna yoyote ile anasaidia au yuko kwenye mpango wa kuchota fedha za umma ili kumpatia bwana huyu Seth, ataanguka na bwana huyu. Katika historia ya IPTL tangu wameanza, hajawahi kupona mtu, mtu yeyote ambaye amejihusisha na IPTL tangu mwaka 1995 awe ni Waziri, awe ni Katibu Mkuu, awe ni nani, hajawahi kupona, kwahiyo watu wajiepushe na hili jambo”.
Zitto amefafanua kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania kupitia Kesi Namba 90 ya Mwaka 2018, kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati dhidi ya Harbinder Seth, ilifikia Makubaliano ya Maelewano (Consent Decree). Kupitia kesi hiyo, Bwana Sethi alikubali kusaini Hati ya Fidia (Deed of Indemnity), akiahidi kuilipa Serikali fidia ya hasara iliyoletwa na maamuzi ya mahakama za kimataifa dhidi ya Tanzania na TANESCO – maamuzi ambayo yanaifanya Tanzania kudaiwa mabilioni.
Katika makubaliano hayo, Mahakama ilieleza wazi kuwa Sethi hana na hatakuwa na madai yoyote dhidi ya Serikali na anapaswa, pamoja na PAP, kulipa fidia hiyo. Hata hivyo, Zitto alieleza kuwa hadi leo, utekelezaji wa maamuzi hayo halali bado haujafanyika.
“Kuitwa mwizi si tusi, bali ni sifa anayostahili. Huyu ni mtu ambaye tayari ana hukumu ya jinai kichwani kwake, lakini amepewa uhuru wa kudhihaki Watanzania na kodi zao,” alisema Zitto kwa ukali.
Aidha, Zitto amefichua kuwa Sethi alikubali makosa ya jinai ya uchotwaji na utakatishaji fedha kupitia makubaliano ya Plea Bargain na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), ambapo aliahidi kulipa zaidi ya shilingi bilioni 26 kwa Serikali. Hadi sasa, amerejesha milioni 200 pekee, huku zaidi ya miaka minne ikiwa imepita tangu apate uhuru wake kwa masharti.
Zitto pia alieleza kuwa kampuni ya Eurasia Holdings, ambayo ilikuwa mbia katika IPTL, imefungua kesi ya kutaka kampuni hiyo ifutwe rasmi (winding up petition), jambo linalozua maswali makubwa kuhusu hatma ya fedha za umma zinazodaiwa kufidiwa na PAP na Seth.
Katika hatua nyingine, Zitto ameibua mgongano wa madai kati ya Seth na TANESCO. Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ukurasa wa 35 na 36, Sethi anadai TANESCO shilingi bilioni 211. Hata hivyo, TANESCO inadai kuwa Seth ndiye anayedaiwa, kwa kuwa katika makubaliano na DPP alikubali kuilipa TANESCO dola za Marekani milioni 148, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 400.
“Kwa hiyo hata tukikubali madai yake, bado TANESCO inamdai zaidi ya anavyodai. Hivyo ni wazi kuwa yeye ndiye mdaiwa, na si TANESCO,” amesema Zitto.
Zitto amesisitiza kuwa madai hayo, pamoja na ushahidi uliopo kwenye nyaraka rasmi za Serikali, vinaweka bayana kuwa hakuna msingi wowote wa kisheria au kisiasa kwa yeyote kumsaidia Seth katika kujinufaisha kwa fedha za umma.
“Ninafurahi kuwa kesi hii inakwenda mahakamani. Huko ndiko tutakapoweka ukweli wote hadharani. Tutautaja mzoga huu mahakamani na kuhakikisha unafukiwa moja kwa moja,” amehitimisha Zitto, akimaanisha kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa dhidi yake na Seth.

Indonesia

@TanganyikaOne @Mwanahalisitz @ACTwazalendo @zittokabwe Watoto wa juzi mna viburi vya kifala. Zitto Kabwe amekuwa mstari wa mbele kuyasema na kufichua ubadhilifu juu ya haya mambo tangu akiwa bungeni. Vinuka mkojo hamuelewi hili
Indonesia

@Mwanahalisitz @ACTwazalendo @zittokabwe @zittokabwe zama zako zimekwisha sasa ni muda wa kulipia ufisadi wako na jinsi ambavyo ulikuwa unanufaika na wizi na ufisadi serikali kwa kutulizwa...ww leo ndo unakuja kusema utasema maovu yote ya Seth baada ya kukufungulia mashitaka??seriously??ungekuwa mzalendo ungesema mapema
Indonesia
Mr David retweetledi

Aliyeona kama gazeti la @MwananchiNews online wamepost kipande japo cha sekunde 1 ya hotuba ya Boni Yai. Anitumie tafadhari.
Indonesia
Mr David retweetledi

DAR: Kiongozi Mkuu Mstaafu wa Chama cha #ACTWazalendo, Zitto Kabwe amesema amefunguliwa kesi na Harbinder Singh Seth akidaiwa kumkashifu mtu huyo na kumvunjia heshima mbele ya jamii wakati Zitto alipozungumzia sakata linalohusu Kampuni ya Ufuaji Umeme ya IPTL
Zitto ambaye amesema anashutumiwa akidaiwa kutoa kauli ya kukashifu na kumchafua Sethi kupitia ukurasa wake wa X, amesema “Nipo tayari kwa kesi, nitaweka ukweli wote wazi na mwisho kufukia kabisa huu mzoga unaoitwa Sakata la IPTL.”
Ameongeza “Ninampongeza sana (Sethi) na kumshukuru kwa ujasiri wake wa kunishtaki kwasababu kesi hii itatoa fursa ya kumaliza jambo hili lililoweka wingu kwa muda mrefu sana katika Taifa letu."
Soma jamii.app/ZittoKabweMei18
#JamiiForums #JFMatukio
Indonesia
Mr David retweetledi

Mwami @zittokabwe amefanya press conference muda mchache uliopita na kudai kuwa ameshtakiwa na Harbinder Singh Sethi wa IPTL, hii ni kutokana na chapisho lake aliloandika kupitia mtandao wake wa X kuhusu kuibuka tena kwa sakata la IPTL kwenye ripoti ya CAG.

Filipino

@Jambotv_ @zittokabwe ww ni mpuuzi..sana unaanza kudeal na Seth.. wakati pesa inayoendelea kupigwa na ikulu na genge lake ni mara 50 ya pesa ya escrow
Indonesia
Mr David retweetledi
Mr David retweetledi

Zitto ashtakiwa kwa andiko la IPTL mwananchi.co.tz/mw/habari/kita…
HT
Mr David retweetledi

@zittokabwe Nakuamini sana brother sasa nimuda wako wakurudi bungeni ili ukatutetee sasa japo nitawamisi na akina @godbless_lema @HecheJohn @TunduALissu @kafulila_david nyie ndio mlio kuwa mnatutetea sana bungeni na mlikuwa wapinzani wa kweli
Filipino
Mr David retweetledi

@zittokabwe Ninaomba Mungu akupeleke Bungeni... nakusihi sana ongeza ulinzi binafsi.. I know there're several illegal deals that has been done in 5yrs.. tukianza na JNHP,SGR,ATCL, na Tannesco. Ni kipindi hiki makundi dhalimu hayataka kuona ukiwa hai.. hivyo ikiwezekana nenda manda magere .
Indonesia
Mr David retweetledi
Mr David retweetledi

Leo Mei 18, 2025 Katibu Mkuu Kiongozi wa @ACTBarazaKivuli, Ndugu @idrisa_kweweta amechukua fomu ya kugombea Ubunge w Jimbo la Kilwa Kusini. Fomu hiyo amekabidhiwa na Katibu wa Jimbo la Kilwa Kusini, Ndugu Twahir Bingwe.
#MuhuniHasusiwi
#OperesheniLindaDemokrasia
@ACTwazalendo




Indonesia

CHADEMA waumbuana.
CHADEMA waanikana.
CHADEMA wakataana.
CHADEMA wageukana.
CHADEMA wasalitiana.
CHADEMA wanyukana.
CHADEMA yapukutika.
CHADEMA yaparaganyika.
CHADEMA yasasambuka.
CHADEMA yachanika.

MwanaHabari@MwanaHabariNews
"Msajili wa Vyama Vya Siasa amempangia Lembrus Mchome Apartment huko Masaki na Serikali imempa walinzi wa kumlinda kila mahali anapoenda."-: #Boniyai
Indonesia
Mr David retweetledi
Mr David retweetledi









