Edgar Mkosamali retweetledi
Edgar Mkosamali
335 posts

Edgar Mkosamali
@EMkosamali
ACT Shadow Minister For Mineral Resource & Mining. Advocating for Better Policies that Will Impact Lives of Tanzanians From Godly Given Wealth
Singida Tanzania Katılım Mart 2022
155 Takip Edilen780 Takipçiler
Edgar Mkosamali retweetledi
Edgar Mkosamali retweetledi

Chama cha ACT Wazalendo kimeeleza kuwa kinamkumbuka Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis kama Kiongozi wa kiroho, mwenye utu, asiyejikweza na aliyeguswa na madhila na umaskini wa watu, akipenda kuona dunia ikichukua jitihada za makusudi kuondoa umaskini miongoni mwa jamii ya binadamu.
Kiongozi wa Chama hicho Bi. Doroth Semu ameeleza kuwa @ACTwazalendo inamkumbuka Papa Francis kama kiongozi mnyenyekevu, aliyetumia muda wake mwingi kama kiongozi katika kutafuta haki na amani katika mataifa mbalimbali duniani hasa Afrika.
"Uongozi wake ulijidhihirisha kuwa wa watu wote bila kujali mipaka ya imani, bali alitanguliza ubinadamu kwa watu wote." Imesema taarifa ya Kiongozi wa ACT Wazalendo.
ACT Wazalendo imetoa pia pole kwa waumini wa kanisa katoliki Tanzania na kote duniani kwa msiba huo wa Papa Francis, wakieleza kuungana na wote walioguswa na msiba huo kumuombea kheri kwa Mwenyenzi Mungu aipokee roho yame na kuiwema mahali pema peponi

Indonesia
Edgar Mkosamali retweetledi

Zanzibar’s VP: Angolan authorities' actions tarnish the spirit of African Union thecitizen.co.tz/tanzania/news/…
English
Edgar Mkosamali retweetledi

Kuahirishwa kwa Mechi ya Simba na Yanga, Bodi ya Ligi Kuu Ijitafakari
Uamuzi wa kamati ya uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) kuahirisha mchezo namba 184 kati ya Young Africans (Yanga SC) na Simba SC uliokuwa uchezwe tarehe 08 Machi 2025, haukuzingatia hasara mbalimbali zilizotokana na kuahirishwa kwa mchezo huo, ikiwemo nafasi ya mashabiki, wafanyabiashara, warusha matangazo, wapenzi wa soka, na maendeleo ya soka nchini kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ibara ya 55 (2) inatoa jukumu kwa Bodi ya Ligi kusimamia ligi kuu na kuhakikisha timu zinaheshimu sheria, kanuni na maamuzi ya TFF. Kanuni namba 15 (3) inasisitiza kuwa ratiba ya ligi itatangazwa na Bodi ya Ligi na itabadilishwa tu kwa dharura au sababu za msingi. Hata hivyo, Bodi ya Ligi imekuwa ikibadili ratiba mara kwa mara bila dharura wala sababu za msingi, jambo linalosababisha hasara kubwa kwa wadau.
Kuahirishwa kwa mchezo kulitokana na madai ya timu ya Simba SC iliyozuiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja kama kanuni na taratibu za mchezo wa Soka zinavyoeleza, aidha upande wa Yanga SC katika taarifa yake rasmi kwa umma ilieleza inatambua mechi ipo palepale na kwamba haitakuwa tayari kucheza mechi hiyo siku nyingine.
ACT Wazalendo inaona mwenendo huu wa Bodi ya Ligi umejaa malalamiko kutoka kwa wadau wengi, kwa kuwa imekuwa ikiongozwa na utashi wa timu hizo za Kariakoo, jambo linaloharibu taswira ya ligi yetu, heshima ya Tanzania kisoka, na kuleta hasara kwa wadhamini, mashabiki na wafanyabiashara.
ACT Wazalendo inaitaka Bodi ya Ligi iliyopo madarakani kujitafakari kama inafaa kuendelea kusimamia ligi kuu ya Tanzania au inapaswa kujiengua.
Pili, ACT WazalendoTunaitaka Bodi ya Lingi kuendesha ligi kwa kuzingatia na kusimamia sheria na kanuni bila uonevu wala upendeleo kwa timu yoyote.
Tatu, Bodi ya Ligi ichukue hatua za haraka na za haki kwa mujibu wa kanuni ya 31 (1.1 hadi 1.8), ikiwa ni pamoja na adhabu kama vile kupoteza ushindi, kushushwa madaraja mawili, kutozwa faini ya Milioni 3, na kutopata gawio la mchezo husika.
Nne, TFF ifanye tathmini ya madhara yote yaliyotokana na kuhairishwa kwa mechi hii na waathirika wote walipwe fidia.
Mwisho, ACT Wazalendo inataka kuona Mpira wa Tanzania unaendelea kukua, kupata heshima na kusaidia kukuza uchumi wa mtu mmojammoja, vilabu na Taifa kwa ujumla, hatutafumbia macho matukio yote yatakayohatarisha shabaha hiyo.
Imetolewa na
Ndg. @Monalisandala1
Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
09 Machi 2025.
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
@SimbaSCTanzania @YoungAfricansSC @tplboard @Tanfootball @ACTwazalendo


Indonesia
Edgar Mkosamali retweetledi

Ngome ya Wanawake ya ACT Wazalendo imempa tuzo ya heshima Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu Prof. Assad na Rais Mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Mstaafu Tanganyika (TLS) Fatma Karume kutokana na mchango wao kwenye kupigania haki, uwazi, uwajibikaji na usawa katika jamii.
Tuzo hizo zimetolewa kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Indonesia
Edgar Mkosamali retweetledi

TUNATAKA UCHUNGUZI KUTEKWA KWA METHOD DAMIAN
Huyu ndio Ndg. Method Damian Kumdyamka aliyetekwa tangu Februari 28, 2025 Sinza Dar es Salaam . Leo ni siku ya nne tangu atekwe hakuna hatua yoyote ya maana iliyochukuliwa na vyombo vya usalama.
@tanpol wapo kimya, ndugu, jamaa na marafiki wanalia, hawajui wafanye nini. Waziri Kivuli wa ACT Wazalendo @hassandahlia7
ameonya kuwa Jeshi la Polisi linapaswa kutambua kuwa Watanzania hawatakubali kuishi kwa hofu kila uchao huku dola ikiendelea kuzembea kuwalinda au wao ndio wahusika?
@ACTBarazaKivuli @zittokabwe @AdoShaibu @SemuDorothy @MchinjitaIR @MtuturaAbdallah


Indonesia
Edgar Mkosamali retweetledi

Kiongozi wa Chama cha @ACTwazalendo, Ndugu, @SemuDorothy amefanya uteuzi wa Kamati ya Kuunda Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2025
1. @Immamvula-Mwenyekiti wa Kamati
2. @idrisa_kweweta -Katibu wa Kamati
Wajumbe
1. Dkt. @DrBSanga
2. Prof. Omar Fakih
3. Mary Mongi
4. @AMtutura
5. @PavuAbdallah
6. Edgar Mkosamali
7. @abdulnondo2
8. @CornelySinta
9. @SeifhSuleiman
10. @ayo_shangwe
11. Humphrey Mrema
12. @Mbaralagande
Sekretarieti ya Kamati
1. @Mshengahussein
2. @JasperKido
3. Jackline Prosper Ndonde
4. Said Mahalifa

Indonesia
Edgar Mkosamali retweetledi

Ninawatakia kila la kheri chama cha demokrasia na maendeleo @ChademaTz katika mkutano wao mkuu leo . Mkutano huu ni muhimu kwa ustawi wa chama hicho na mwenendo wa demokrasia nchini. Aidha mwenendo wa minyukano ya kisiasa miongoni mwa kambi kuu zinazowania nafasi ya kuongoza chama hiko unaweka rehani uwezo wa kufanya kazi pamoja baada ya uchaguzi. @ACTwazalendo imekuwa kimbilio mara zote kwa wahanga wa demokrasia . Tunawakaribisha wale wote wanao ona safari yao ya kidemokrasia inahitaji jukwaa jipya. Karibuni @ACTwazalendo yenye tunu ya uongozi wa pamoja, uwazi na mijadala ya masuala.
Indonesia
Edgar Mkosamali retweetledi
Edgar Mkosamali retweetledi

"Tanzania sasa hivi. Ukisema ukweli wanakuteka."
Katibu Mkuu wa @ACTwazalendo
@AdoShaibu
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
Indonesia
Edgar Mkosamali retweetledi

Edgar Mkosamali retweetledi

@ExMayorUbungo Ikiwa Serikali ya CCM haina majibu kuhusu utekaji na mauaji ya watu,
Ikiwa Serikali ya CCM haichukui hatua dhidi ya utekaji na mauaji ya watu,
Ikiwa imeshindwa kukomesha vitendo vya utekaji na mauaji ya watu,
Maana yake Serikali ya CCM ndio mhusika mkuu wa vitendo hivyo.
Indonesia
Edgar Mkosamali retweetledi

Medy uliniambia nisiogope, na kwamba kila mtu ataonja mauti, lakini sikujua mwisho wako utakuwa wa namna hii.!
Fikiria mdogo wako uliyekuwa naye na kuishi naye miaka 66 leo ameshindwa Kukutambua kwa kukutizama uso wako.
Kama siyo ile alama yako ya mguuni huenda familia yako,ndugu zako na sisi marafiki zako tungekuacha ukazikwe na Jiji.
Maharamia wamekuua kweli, wamekuumiza sana, Wamekushambulia sana, Wameharibu uso wako wote ambao mara zote ulijaa tabasamu.
Hawakuridhika wakakumwagia tindikali ili Dunia isikutambue tena..!
Sasa roho zao zimefurahi nafsi zao zimeridhika kukuona ukiwa mwili mtupu usio na pumzi,Hujawahi kuwatendea baya lolote,kosa lako ni kuwa mwanachama wa CHADEMA.
Tutakutana tena Mbinguni Kamanda.

Filipino

@AdoShaibu Tulia hawezi kuwa spika wa Bunge la wananchi Bali spika wa serikali.....
Aliletwa na muhimili wa serikali kuja kilitawala Bunge kwa maslahi ya serikali.
Hawezi kuwa spika wa maslahi ya umma abadani
Indonesia

DK. TULIA UMETUANGUSHA WANAFUNZI WAKO
Dk. Tulia ni Mwalimu wangu. UDSM alinifundisha Sheria za Mirathi (Probate and Admnistration of Estate). Ninachoweza kusema anavyopambana kuikingia kifua Serikali kwenye suala la utekaji badala ya kuiwajibisha; AMETUANGUSHA Wanafunzi wake.
Mahusiano baina ya Mwalimu na Mwanafunzi ni ya kudumu. Hakuna linaloweza kuyabadili. Mwalimu ni Mwalimu milele na Mwanafunzi ni Mwanafunzi milele.
Mara nyingi, walimu huwa na fahari wanafunzi wakipata mafanikio makubwa kwenye taaluma, kazi na masuala mengine ya kimaisha. Wanafunzi nao ni hivyohivyo, hufurahia mafanikio ya walimu wao.
Kuchaguliwa kwa Spika Tulia kuwa Spika wa Bunge, wanafunzi wake wengi kulitupa furaha ambayo ingezidi maradufu kama angekuwa Spika wa viwango.
Kwa kinachoendelea kwenye suala la utekaji, niseme bayana kuwa badala ya kutufanya wanafunzi wake tutembee kifua mbele, yeye amechagua kutuangusha.
Rai yangu kwake; kama hajali kutimiza wajibu wa kikatiba na kisheria wa Bunge ambao ni kuisimamia na kuiwajibisha Serikali, basi angalau amuogope Mungu na kusimamia kiapo cha kazi yake!

Indonesia
Edgar Mkosamali retweetledi

Tuzungumzie suala la "KUFUATA MATAKWA YA SHERIA ZA NCHI".
Barua hii ya ZUIO kwa ACT-Wazalendo, mmetumia sheria ipi? Au mtaikana si yenu? Maana, vifungu mnavyotakiwa kuvifuata katika kushughulika na mikutano ni; 43 - 46 vya Sheria ya Jeshi la Police, 11 (1) & 11(7) vya Sheria ya Vyama Vya Siasa na Katiba ib. 20(1).
Sababu ya KUZUIA mkutano kwa "MAELEKEZO" imetamkwa kwenye kifungu kipi cha sheria?
USHAURI: Ili kuondoa SINTOFAHAMU, next time muwe mnataja na kifungu cha sheria kinachowapa mamlaka ya kufanya maamuzi fulani. Vinginevyo, mnachokifanya ni SIASA, kitu ambacho askari amekatazwa KIKATIBA na kwenye PGO.
Toeni HAKI SAWA kwa kuzingatia ib 13(1) ya Katiba ya nchi.
Mwisho, kisheria hamna mamlaka ya kujihusisha na MIKUTANO YA NDANI. Tusiende huko.
#BabaMwita 🎤


Indonesia
Edgar Mkosamali retweetledi
Edgar Mkosamali retweetledi

VIDEO:
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Padri Dkt. Charles Kitima ametoa wito kwa serikali kupitia TAMISEMI (Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika baadaye mwaka huu kuhakikisha yale yote yaliyojitokeza kwenye uchaguzi kama huo mwaka 2019 hayajirudii tena kwa kuwa kwa kiasi kikubwa uchaguzi huo ulirudisha nyuma nguvu ya demokrasia nchini
Padri Dkt. Kitima ametoa rai hiyo wakati alipofanya mahojiano maalum na Jambo TV hivi karibuni
Indonesia






