Wazaa
3.1K posts




Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imefuta (imeondoa) zuio (injunction) lililotolewa na Mahakama Kuu (Masjala ya Dar es Salaam) Juni 10, 2025 na Jaji Hamidu Mwanga (ambaye ndiye aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo). Zuio lilikuwa linazuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya shughuli zozote za kisiasa, kutumia mali zake, kushiriki katika shughuli za chama hadi kesi ya msingi isikilizwe na kumalizika. Kesi (Civil Case No. 8323 ya 2025) ilifunguliwa na Said Issa Mohamed (Makamu Mwenyekiti wa Freeman Mbowe) pamoja na wenzake wawili (waliohusishwa na mgawanyo wa mali za chama kati ya Bara na Zanzibar). Walidai kuna mzozo wa ndani kuhusu mali na uongozi wa CHADEMA. Jaji Mwanga alitoa amri ya muda (interim injunction) ikizuia chama kufanya shughuli zozote za kisiasa na kufungia mali zake ili kesi yao isikilizwe. Amri hiyo ilikuwa ilikuwa ya muda wa siku 14 mwanzoni, lakini iliendelea kuwepo kwa miezi mingi (hadi karibu mwaka mmoja). Hadi kufikia leo April 15, 2026 ni jumla ya siku 310 tangu kuwekwa zuio hilo haramu kabisa. CHADEMA ililalamika kwamba: Zuio lilikuwa kali sana na liliathiri haki yao ya kufanya siasa. Jaji Mwanga alikiuka taratibu za haki ya kusikilizwa (right to fair hearing). Zuio lilikuwa limezidi muda unaoruhusiwa kisheria. Mahakama ya Rufaa iliyoketi Dodoma ilianza kusikiliza maombi ya marejeo (revision) Machi 24, 2026. Leo (Aprili 15, 2026) jopo la majaji limetoa maamuzi yake na kufuta zuio hilo lililowekwa na Jaji Hamidu Mwanga. CHADEMA sasa iko huru kuendelea na shughuli zake zo za kisiasa, mikutano, kampeni na matumizi ya mali yake bila kizuizi hicho. Hivyo shughuli ya kushughulika na Serikali katili ya CCM inaanza pale ilipoishia. Kesi ya msingi (mgawanyo wa mali) itarudi Mahakama Kuu ya Tanzania, lakini kwa jaji mwingine (sio Jaji Hamidu Mwanga tena) kuamua suala moja tu la msingi, kama kesi hiyo ililetwa ndani ya muda au vinginevyo.. Hakuna zuio la kufanya shughuli za kisiasa kwa CHADEMA. Chama chetu kiko huru kutoka katika minyororo ya ukatili wa Serikali katili ya CCM. CHAMA kitatoa taarifa rasmi kwa umma na kueleza vizuri. NB; Siku 310 za CHADEMA gerezani, ‘vyama mpango wa kando’ wa CCM hawajafanya hata kongamano la jando na unyago. Tumerudi, tupatane kwa ground tuwaoneshe kazi inavyofanywa. PEOPLE’S POWER. MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.





🚨 Kai Havertz set for spell on sidelines with muscular injury. Problem expected to keep 26yo Arsenal forward out of #AFC games against Brentford + Tottenham Hotspur but hoped not to be serious issue for Germany international. W/ @gunnerblog @TheAthleticFC nytimes.com/athletic/70389…















