Malesho retweetledi
Malesho
2.3K posts

Malesho retweetledi
Malesho retweetledi
Malesho retweetledi
Malesho retweetledi
Malesho retweetledi

@Mwinshehe07 @CrownMediaTZ Jamaa hana point ya msingi kabisa, huyu cross examination ya lissu au kibatala lazima wampepeee😁😁😁😁😁
Indonesia
Malesho retweetledi

Jemedari hajataka unafiki wa juma kusifia sifia zile taarifa zilipostiwa na media Jana kuhusu Rio 😂
📸 @CrownMediaTZ
Indonesia
Malesho retweetledi
Malesho retweetledi
Malesho retweetledi
Malesho retweetledi
Malesho retweetledi
Malesho retweetledi

02
Hata kabla ya sheria nyingi kuandikwa,dhamiri tayari ilikuwa imeanza kushtaki.
Ndiyo maana ukweli mkubwa ni huu:Unaweza kuwadanganya watu kwa muda.Unaweza kuikwepa sheria kwa muda.Lakini ni vigumu sana kuikwepa dhamiri yako mwenyewe milele.
Kwa sababu dhamiri ya mwanadamu…ni mahakama ambayo haifungwi milele.
Kuna watu wanatembea huru leo,
lakini akili zao zimekuwa magereza yao.
Watu waliovikwa medali,
waliosifiwa majukwaani,
waliosalimiwa kwa heshima kubwa—
lakini usiku wanashindwa kulala wakiteswa na kumbukumbu
ambazo hawawezi kuzizika.
Kwa nini?
Kwa sababu kuna tofauti
kati ya kile kilicho halali
na kile kilicho sahihi mbele ya ubinadamu.
Mtu anaweza kuwa anafuata amri…
lakini bado akawa anasaliti utu wa mwanadamu.
Historia imejaa askari waliokuja kukiri baadaye:
“Tulikuwa tunafuata maagizo.”
Lakini dunia imejifunza kwa uchungu:
uovu hauwi haki
kwa sababu tu umeamriwa na mamlaka.
Na leo hii,
onyo langu linaenda kwa kila kiongozi,
kila taasisi,
kila afisa,
na kila mwanachama anayelinda mfumo bila kuhoji:
Tusijenge taifa
ambalo utii ni muhimu kuliko dhamiri.
Kwa sababu taifa likifika hapo,
watu huacha kutetea ukweli
na kuanza kutetea mamlaka.
Na mamlaka yanapoanza kuogopa uwajibikaji, kufichiana
(cover-up)huanza.
Na cover-up inapoanza,
haki huanza kufa.
Na haki ikifa,
taifa linaweza kuonekana lina amani kwa nje
lakini ndani linaoza taratibu.
Ndugu watanzania wenzangu
Taifa lenye afya si taifa lisilo na wakosoaji.
Taifa lenye afya
ni taifa ambalo ukweli bado unaweza kupumua.
Uzalendo si kulinda makosa.
Uzalendo wa kweli
ni kulipenda taifa lako kiasi cha kuthubutu kukemea
kile kinacholiharibu.
Watu hatari zaidi katika jamii yoyote
sio tu wale wanaofanya maovu
bali wale wanaoyahalalisha,
wanaoyatetea,
au wanaonyamaza
kwa sababu wahusika ni “wa upande wao.”
Leo nauliza:
Tunataka kuwa taifa la namna gani?
Taifa linalotawaliwa na hofu?
Au taifa linalotawaliwa na haki?
Taifa la watu wanaotii bila kufikiri?
Au taifa ambalo dhamiri bado ina thamani?
Kwa sababu ipo siku,
vyeo vitaondoka.
Serikali zitabadilika.
Vyama vya siasa vitapita.
Lakini historia itabaki.
Na historia haina huruma
kwa viongozi waliochagua mamlaka
kuliko ubinadamu.
Tusije tukawa taifa
linalozika ukweli kwa kina sana
mpaka vizazi vijavyo virithi ukimya wetu kama mateso yao.
Kwa sababu…
Hatia haina kaburi.
Rev Peter Simon Msigwa
Iringa
Indonesia
Malesho retweetledi

01 one of two
“Dhamiri ni mahakama ambayo haifungwi milele.” na hatia haina kaburi,
Kuna wakati ni hatari sana kwa taifa lolote…
Pale ambapo ukimya unaanza kuwa salama kuliko ukweli.
watu wanapoanza kunong’ona gizani
mambo ambayo walipaswa kuyasema hadharani.
Na historia imetufundisha jambo moja la kuogopesha sana ,
Serikali zinaweza kuficha mafaili,
zinaweza kuficha ripoti,
zinaweza kunyamazisha mashahidi,
zinaweza kuwaogopesha wakosoaji
lakini hatia haina kaburi.
Hata kama uhalifu, kosa, au tendo ovu limefichwa, limezikwa, limefunikwa, au limesahaulika na jamii — hatia yenyewe haifi kirahisi.
Mtu anaweza kuficha ushahidi.
Serikali inaweza kuwanyamazisha mashahidi.
Historia inaweza kupindishwa.
Lakini ndani ya dhamiri ya mwanadamu, hatia inaweza kuendelea kuishi kwa miaka mingi.
Huendelea “kumsumbua” mtu kupitia kumbukumbu, ndoto, hisia, na mateso ya ndani ya nafsi kutokana na uovu alioutenda kinyume na ubinadamu.
Kwa sababu dhamiri ya mwanadamu ni mahakama ambayo haifungwi milele.”
Mtu anaweza kuukwepa mkono wa sheria…anaweza kuficha ushahidi…anaweza kunyamazisha mashahidi…anaweza kutumia mamlaka, pesa, propaganda, au nguvu kufunika ukweli…
Lakini ndani ya nafsi yake mwenyewe, bado kuna mahakama nyingine inayobaki wazi:Dhamiri.
Na tofauti na mahakama za dunia:• dhamiri haihitaji polisi,• haihitaji jaji wa nje,• haihitaji ushahidi wote hadharani.
Inajua ukweli hata pale dunia nzima inapodanganywa.
Ndiyo maana watu wengi wanaonekana kuwa na nguvu nje —lakini ndani wanaishi na hofu, hasira, usingizi mbaya, au amani iliyopotea.
Historia ina mifano mingi sana.
Mfano wa kwanza:
Baadhi ya wanajeshi waliowahi kushiriki vita vya mauaji ya raia duniani walinusurika kisheria, lakini miaka baadaye walikiri kuwa walikuwa hawawezi kulala usiku.Walikuwa wakisikia sauti za waliouawa kichwani mwao.Sheria iliwaacha huru.Lakini dhamiri iliendelea kuwafunga.
Mfano mwingine:
Katika tawala nyingi za kiimla duniani, viongozi waliotesa wananchi waliweza kuzima vyombo vya habari, kufunga wapinzani, na kuogopesha taifa lote kwa miaka mingi.Lakini wengi wao waliishi maisha ya mashaka makubwa:• waliwaogopa hata marafiki zao,• waliwaogopa walinzi wao,• waliishi wakihamisha walinzi kila mara,• wengine walikufa wakiwa na paranoia na upweke mkubwa.
Kwa nini?Kwa sababu ndani yao walijua ukweli ambao propaganda haiwezi kuufuta.
Hata katika maisha ya kawaida:Mfanyabiashara anaweza kudanganya watu na kupata pesa.Mwanasiasa anaweza kusema uongo na kushangiliwa.Kiongozi wa dini anaweza kuhubiri haki huku akiishi kinyume chake.Mtu anaweza kuonekana “amefanikiwa” mbele ya jamii.
Lakini kuna tofauti kubwa kati ya:kuwa huru nje…na kuwa huru ndani.
Ndiyo maana baadhi ya watu wana kila kitu:• pesa,• mamlaka,• ulinzi,• umaarufu…
Lakini hawana amani.
Kwa sababu dhamiri inapofungua kesi dhidi ya mtu,hakuna usingizi wa kutosha,hakuna pombe ya kutosha,hakuna sifa za kutosha,na hakuna propaganda ya kutosha inayoweza kuifunga kabisa.
Biblia pia inaonyesha hili.
Baada ya Kaini kumuua Abeli, Mungu alimwambia:“Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka ardhini.”
Filipino
Malesho retweetledi
Malesho retweetledi

Leo na kesho tuhakimishe #FreeTunduLissu inatrend
Andika post, weka picba weka hashtag nq share, repost kila post hata za zamani za Lissu
Tuwe serious people! Siku 405 ??!!

Filipino
Malesho retweetledi
Malesho retweetledi
Malesho retweetledi

















