#PICHA: Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza Rio Ferdinand amewasili Tanzania kwa mwaliko maalum wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Paul Makonda.
Hizi ni picha ya jinsi hali ilivyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam leo May 19,2026.
#MillardAyoUPDATES
🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄
Aliyekuwa mwanasheria msomi wa Yanga SC SIMON PATRICK ameandika Haya kupitia mitandao yake ya Kijamii.
“Maamuzi ya kupeleka Derby uwanja wa Mej. Jenerali Isamuhyo - Mbweni ni ushindi wa Yanga na Simba kufanikiwa kuwa juu ya vyombo vya mpira wa Tanzania na kielelezo cha UDHAIFU wa viongozi wa soka nchini jambo lililolelewa kwa muda mrefu.”
“Derby hii ni urithi wa taifa la taifa letu, kitendo cha kuruhusu mchezo huu kuupelekwa Mbweni ni kuwakosea heshima mashabiki wa mpira, kwani uwanja huo ni mdogo sana kwa derby ya kariakoo.”
“Kwa trend hii, sitashangaa derby ijayo tukiambiwa inapigwa Avic Town na inayofata tukaambiwa inapigwa Bunju.”
Mungi ibariki Tanzania🇹🇿.”
NB: Tulilinde taifa letu, sis sote ni ndugu🙏🏿"
#MeaMswahiliUPDATES
Bei za mafuta zimeshuka kwa kasi katika Soko la Dunia huku hati fungani zikipanda na masoko ya hisa yakiongezeka baada ya makubaliano ya usitishaji vita kwa wiki mbili unaohusisha Iran kuchochea hali ya matumaini sokoni huku Wawekezaji wakifurahia uwezekano wa kuanza tena kwa usafirishaji wa mafuta na gesi kupitia Mlango wa Hormuz.
Rais wa Marekani, Donald Trump alisema mwishoni mwa Jumanne wiki hii kuwa amekubaliana kusitisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa wiki mbili na kuongeza kuwa makubaliano ya amani ya muda mrefu yako katika hatua za maandalizi.
Iran ilisema itasitisha mashambulizi yake ikiwa mashambulizi dhidi yake pia yatasimama na kwamba usafiri salama kupitia Mlango wa Hormuz utawezekana kwa wiki mbili kwa kushirikiana na Jeshi la Iran.
Masoko ya dunia yamekuwa yakitetereka tangu Marekani na Israel zilipoishambulia Iran mwishoni mwa Februari hali iliyosababisha Tehran kufunga kwa kiasi kikubwa Mlango wa Hormuz ambayo ni njia muhimu inayotumika kusafirisha takribani asilimia 20 ya mafuta na gesi ya dunia. #MillardAyoUPDATES.
🚨 OKELLO ANAWANYAMAZISHA WAKOSOAJI! 🔥
Baada ya hat-trick ya assist zake leo dhidi ya Pamba Jiji, kiungo mkabaji wa Yanga SC Allan Okello ametoa kauli kali:
“Nilijua nitarudi kwenye ubora wangu, lilikuwa ni swala la muda tu. Nilikuwa naona maneno watu wakiniita Tepsi, sijui maana yake ni nini ila nimewanyamazisha. Na bado nitafanya kilicho bora zaidi, sijui Buba.”