king kinya
8K posts

king kinya
@king_kinya
Mr King Kinya.Editorial cartoonist.

KIUMBE HUYU NI MZIGO. Mtu ‘anayejiita mbunge’ anasema Serikali ya CCM imeongeza bei kidogo sana ya mafuta kulinganisha na Kenya. Huyu mtu hajajishughulisha vya kutosha. Huwezi kulinganisha uchumi wa nchi na nchi kwa kutaja tarakimu tu. Kulinganisha uchumi wa Tanzania na Kenya anatakiwa kutumia vipimo viwili vikuu ambavyo ni; GDP per Capita (Pato la Taifa kwa kila kichwa) na GDP per Capita PPP (Pato la Taifa kwa kuzingatia Uwezo wa Kununua - Purchasing Power Parity). Zingatia hivyo. 1.GDP Per Capita (Nominal); Hiki ni kipimo cha thamani ya fedha ya bidhaa na huduma zote zinazozalishwa nchini, ikigawanywa kwa idadi ya watu katika nchi. GDP (pato la Taifa) inatumia viwango vya soko vya kubadilisha fedha (USD). Hii hutumia viwango vya soko vya kubadilisha fedha (market exchange rates). Tofauti na Tanzania ambayo uchumi wake unategemea zaidi rasilimali za asili (kama madini), Kenya imejenga msingi wake katika sekta ya huduma na ubunifu. Kenya ni kiongozi wa kidijitali barani Afrika, jambo lililoipa jina la utani la “Silicon Savannah.” Mapinduzi ya huduma za kifedha kwa njia ya simu yalianzia hapa. Nairobi ni makao makuu ya makampuni makubwa ya teknolojia duniani (Google, Microsoft, na Amazon) yanayofanya shughuli zake katika bara la Afrika. Benki za Kenya (kama Equity na KCB) zimepanuka na kutawala soko la kanda ya Afrika Mashariki na Kati, zikiwa na matawi nchini DRC, Rwanda, South Sudan Uchumi wa Tanzania kwa sasa unapitia kipindi cha mpito ambapo matokeo yake katika thamani ya sarafu na soko la kimataifa yanachukua muda sana kuonekana. Tanzania inasafirisha madini ghafi. Thamani kubwa ya soko inabaki nchi za nje ambako madini hayo yanasafishwa na kutengeneza bidhaa za mwisho. Thamani halisi inayobaki ni asilimia ya mirahaba na kodi, wakati thamani kubwa ya soko la madini hupimwa masoko ya hisa ya kimataifa (London au Toronto). Uchumi wa Tanzania una sehemu kubwa sana ya sekta isiyo rasmi inayozalisha fedha nyingi, lakini hazionekani kwenye takwimu rasmi za thamani ya soko la kidunia. Kwa wastani, raia mmoja wa nchi ya Kenya anaonekana kuzalisha thamani ya fedha karibu mara mbili ya raia mmoja wa Tanzania katika soko la kimataifa. 2.Purchasing Power Parity (PPP); Hiki ni kipimo cha “uwezo wa kununua.” Kinarekebisha tofauti za gharama za maisha na bei za bidhaa kati ya nchi hizi mbili. Kwa mfano, kama $1 inaweza kununua mikate miwili Tanzania lakini kwa bei hiyo, unaweza kununua mkate mmoja tu nchini Kenya, PPP inazingatia ukweli huo. Kenya ina kipato kikubwa, gharama za maisha ni kubwa. Tanzania ina gharama ndogo za maisha baadhi ya sekta (vyakula vya asili na baadhi ya huduma za kijamii). Kenya ina sekta ya huduma (Banking, Tech, Tourism) iliyoendelea zaidi, ambayo huzalisha thamani kubwa ya fedha. Tanzania inategemea zaidi Kilimo na Madini. Kenya imekuwa kitovu cha kibiashara (Regional Hub) kwa muda mrefu, jambo linalovutia makampuni mengi ya kimataifa kufanya uwekezaji mkubwa Kenya. Kwa sasa nchini Kenya, bei za mafuta zilizotangazwa na Mamlaka ya Kudhibiti Nishati na Petroli (EPRA) zinazotumika hadi Aprili 2026 kwa Mombasa; Petroli (Super Petrol) KSh 189.60 kwa lita (Tsh3,771. Dizeli (Diesel) KSh 173.10 kwa lita (Tsh 3,452). Mafuta ya Taa (Kerosene) KSh 163.00 kwa lita (Tsh 3,253). Hizo habari lita moja ya mafuta ya petroli Kenya inauzwa Tsh 5,450 ametoa wapi? Au amesogezewa kipeperushi na KIHONGOSI kutoka ma’group yao ya WOSAPU? Mtu ambaye anayejiita ‘mbunge wa CCM’ alitakiwa apitishe ubongo wake maeneo hayo, halafu ajenge hoja zake. Vinginevyo ni MPUMBAVU mwenye ujasiri.




Mafuta yapo hadi ya July. Je, nini kilichosababisha leo mafuta yapande bei? Au storage?


Hakuna kitu nakichukulia kwa uzito mkubwa sana kama ripoti ya CAG.. HUWA SINAGA MZAHA KABISA NYAKATI KAMA HIZI NA UGOMVI WANGU NA WAKUBWA HAWA SIKU ZOTE UNAANZAGA KWENYE RIPOTI YA CAG.. Kama hatujajifunza kuwa yaliyotokea 29 Oktoba 2025 ni sababu ya mambo haya ya wizi wa mali za umma na watu kukwapua mihela basi hatutakuwa na akili tena ya kuelewa... CAG tuwekee ripoti online... kwa ukamilifu tuanze kusoma wenyewe na kujua cha kusema kwa watanzania..Atakayechukia achukie tu . We dont dont anymore to sympathise na MAJIZI..

























