mujun katikabakama
2.7K posts

mujun katikabakama
@mujun77
Mwenye kutawala akisikiliza uongo watumishi wake wote watakuwa waovu Mithal 29:12








#KENYA: MKUU WA POLISI AKAMATWA BAADA YA KUWAACHIA WASHUKIWA WA MAANDAMANO KENYA Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Central nchini Kenya, Chief Inspector Dishen Angoya, amekamatwa kwa tuhuma za kuwaachia washukiwa 64 waliokuwa wamekamatwa wakati wa maandamano ya kupinga ongezeko la bei ya mafuta yaliyoikumba nchi hiyo. Polisi nchini Kenya wanasema Angoya anachunguzwa kwa madai ya kutumia vibaya madaraka baada ya kuwaruhusu washukiwa hao kutoka mahabusu bila idhini halali kufuatia vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano hayo. Kukamatwa kwake kunakuja wakati Kenya ikiendelea kushuhudia mvutano mkubwa baada ya maandamano yaliyovuruga shughuli za usafiri na biashara katika maeneo mbalimbali nchini humo kutokana na kupanda kwa gharama ya mafuta. Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya Kipchumba Murkomen amesema watu wanne walifariki dunia, zaidi ya 30 kujeruhiwa huku washukiwa 348 wakikamatwa wakati wa maandamano yaliyoripotiwa katika kaunti kadhaa nchini humo. Wakati huo huo, maafisa wa upelelezi wanaendelea na uchunguzi kuhusu tukio la kuchomwa moto kwa gari linalodaiwa kumilikiwa na mwanasiasa wa chama tawala cha UDA wakati wa vurugu zilizotokea katika eneo la Thika Road.




















































