Philipo Kirumba
5.9K posts









Ndugu wanachama wa CHADEMA na Wapenzi wa Demokrasia Nchini. Chama chetu kimefunguliwa rasmi kufanya shughuli za siasa. Hii ni fursa muhimu katika kuendelea na mapambano ya haki, uhuru na uwajibikaji katika Taifa letu. Lakini ukweli usioepukika ni huu hatuna ruzuku hata ya SENTI MOJA. Hii ina maana kwamba uhai, nguvu na uendelevu wa CHADEMA uko mikononi mwetu sisi wenyewe. Hatuna budi kuchukua jukumu. Hatuna budi kusimama. Hatuna budi kuchangia. Kila Mwanachama na kila mpenda Demokrasia ana wajibu wa moja kwa moja, kuchangia CHADEMA. Usione mchango wako ni mdogo. Usisubiri mwingine achukue nafasi yako. Kila senti unayotoa ni nguzo ya kusimama kwa chama hiki. Tujenge utamaduni wa kuchangia bila kusukumwa. Tujenge tabia ya kusaidia chama kila wakati. Hapo ndipo tutakapopata uhuru wa kweli wa kisiasa na kiutendaji. Mimi nipo, na nimeanza. Na wewe pia ni wakati wako sasa. Chukua hatua. Anza kuchangia. Simama na CHADEMA. Kwa pamoja, tutakijenga chama imara na Yaifa lenye HAKI. Tuchange tu kwa namba maalumu za CHAMA na Akaunti za Benki ili kujenga uadilifu wa Taasisi Imara. Mikakati zaidi inakuja baada ya vikao kuanza. Asanteni.

















