COELESTINE MUKELA retweetledi

Ninawatakia Watanzania wote heri ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Muungano wetu ni lulu na urithi wa kipekee tulioupokea kutoka kwa waasisi wetu. Hivyo, nasi tuna wajibu wa kuutunza, kuulinda, na kuuimarisha ili tuurithishe kwa vizazi vijavyo ukiwa salama na imara kama tulivyoupokea.
Ninatoa wito kwa Watanzania kuendelea kushirikiana, kufanya kazi kwa bidii, na kuimarisha uzalendo wetu, ili tujenge Tanzania moja, imara zaidi, yenye umoja na maendeleo jumuishi kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ubariki Muungano wetu.

Indonesia



















































