




DAUDI M. MACHABA
488 posts

@daudiMachaba
Guild President KIUT 2024/2025 | Pharmaceutical Technician | BPharm candidate | QPPV | Public Health Advocate | Leader & Researcher in Health Policy.



















Salim, nadhani ni muhimu katika chambuzi kama hizi kutotazama tu China kama mtoaji ( donor ) kwa Tanzania ( receiver ). Naelewa hii ni njia nyepesi kueleweka na mfumo wetu wa kiuchambuzi ni kuonyesha kuwa nchi zetu zinapokea tu. Ni muhimu sana kuonyesha China imepata nini kutoka Tanzania. Mfano; 1. Tanzania imeipa heshima China kwa kuwa mstari wa mbele kabisa kuhakikisha China inapata kiti chake katika Umoja wa Mataifa. Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim ndiye aliongoza jitihada hizi akiwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. China walimpa Nishani ya Juu kabisa kutambua mchango wake huo. 2. Tanzania inanunua bidhaa kutoka China. Ni soko la bidhaa na huduma za China. Mwaka 2023 Tanzania ilitumia Usd 8B ( shs trilioni 20) kununua bidhaa kutoka China. Hii maana yake ni kuwa Watanzania wanawaweka makazini wachina. Ukitazama ni kiasi gani China inanunua kutoka Tanzania utaona ni USD 450M tu, karibu 5% tu ya kile tunachoagiza kutoka China. Ni muhimu sana uchambuzi uweke hizi 'facts' wazi ili kuonyesha kuwa sio China inayotupa tu sisi zawadi. Tunapeana. Wanatujengea TAZARA lakini licha ya faida watakayopata lakini pia tunanunua bidhaa za viwanda vyao na kuwapa ajira watu wao. Na kadhalika. Nakupongeza unaifanya @CrownMediaTZ kuwa chombo cha masuala mazito. Hiki ni kitu tumekuwa tunakikosa katika radio zetu na hata vituo vya televisheni. Hongera sana











Congratulations, @DocFaustine, on your election to serve as the next @WHOAFRO Regional Director — it is a great privilege, and a very great responsibility. I and the entire @WHO family in Africa and around the world will support you every step of the way. #RC74AFRO
