Iamcactus
2.5K posts


#TajiriLakihaya Jana tulikua tunakumbushana tu ili tuwe Sawa! Sasa VIJANA Naomba tujadili issue kamili- najua wengi mnaogopa kujadili hii mada Kwa kuogopa matusi na hata usipate support yoyote… Ila lazima tulijadili hili Kwa maslahi mapana ya Sisi vijana na kizazi chetu cha kesho… Kuzidi kufunguliwa kwa Betting Companies kila uchao na hata hii ya juzi ilioleta kelele humu si hatua ya maendeleo, ni kengele ya hatari kwa kizazi chetu vijana. Kamari haitujengei vijana uwezo, haitupi ujuzi, wala haitengenezi thamani kwenye uchumi. Inauza ndoto ya ushindi wa haraka, lakini ukweli wake ni mzunguko wa hasara, madeni, utegemezi na kuvunjika kwa maisha. Tunaambiwa ni ‘AJIRA’, lakini ni ajira ya aina gani inayotegemea watu wengi kupoteza pesa zao ili wachache wanufaike? Huu si uchumi jumuishi,ni mfumo unaonufaisha kampuni huku ukiwaacha vijana wakizama kwenye hasara. Na ndio maana kampuni za kamari kila siku zinaongezeka lakini vijana BADO tupo kwenye umasikini ule ule Miaka nenda Miaka Rudi💔 Athari zake zipo wazi; Madeni yanayokua kimya kimya,Msongo wa mawazo na hata uraibu wa kamari, Kupotea kwa muda na nguvu ambazo zingetumika kujenga maisha,Kupungua kwa tija kwa vijana waliopaswa kuwa nguvu kazi ya taifa nk. Serikali haiwezi kusema inajali vijana huku ikiendeleza mazingira yanayowasukuma kwenye utegemezi wa BAHATI badala ya juhudi na ubunifu. Hii si sera ya maendeleo, ni kuruhusu kizazi kipotee polepole. Vijana tuamke. Hakuna ‘shortcut’ ya mafanikio kwenye kamari. Waliopo juu ni wachache wanaotumika kama matangazo,lakini maelfu wako chini wakipoteza. KAMARI sio ajira, ni mtego unaowalenga vijana moja kwa moja. Tunauziwa ndoto za ushindi wa haraka, lakini uhalisia ni madeni, utegemezi, msongo wa mawazo na kupoteza kabisa mwelekeo wa maisha. Serikali haiwezi kwa mkono mmoja kuzungumzia kuwawezesha vijana, halafu kwa mkono mwingine kufungua milango ya kamari inayowapumbaza na kuwavuta kwenye utegemezi wa bahati. Hii si sera ya maendeleo,ni kulea utegemezi. Vijana tuamke. Hakuna utajiri wa mkato kwenye kamari! waliowanufaika ni wachache sana, na wengi wanabaki na hasara, maumivu na muda uliopotea. Taifa haliwezi kujengwa kwa tiketi za bahati nasibu. Tunahitaji ajira halisi, elimu bora na fursa za uzalishaji,sio kamari. Tunahitaji uwekezaji kwenye elimu ya vitendo, ujasiriamali, viwanda na teknolojia,not betting. Taifa haliwezi kujengwa kwa kubeti,linajengwa kwa kuzalisha💯💯 Serikali ifikirie upya,hatuwezi kujenga taifa kwa kuwapa vijana ndoto za mkato zisizo na kesho💯💯 Serikali haipaswi kulea kizazi kwa bahati nasibu badala ya fursa halisi. Vijana tuamke,hii si njia ya mafanikio💯💯























